Friday, January 1, 2010

Them, I & Them ....WE ARE THE WORLD (Reggae Tribute)....Luciano

Image from www.westindiantimes.net
Leo ni Ijumaa ya kwanza ya mwaka 2010. Basi ni mwaka nitakaoanza na ujumbe zaidi ya maneno. Na kama ilivyo ada ya siku za Ijumaa ninakuwa na kipengele cha I & THEM ambacho huzungumzia Reggae katika jamii.
Basi na tuuanze mwaka kwa kukubali kuwa SISI NDIO ULIMWENGU na lolote tufanyalo lina athari katika ulimwengu wetu. Ina maana hakuna linalotokea ambalo si zao la matendo yetu. Kwa maana nyingine ni kuwa ILI KUIBADILI DUNIA TWASTAHILI KUBADILIKA SISI WENYEWE.
Kama nilivyosema kwenye salaam zangu kwa bloggers, tunahitaji kuwa watoaji hasa kwa jamii tunayoamini ina uhitaji. Kama walivyotunga wenye wimbo kuwa "We are the ones who make a brighter day. So lets start giving"
Na ndio maana katika kuuanza mwaka, nakuburudisha naye Luciano katika kibao hiki WE'RE THE WORLD ambacho ni marudio ya wimbo ulioimbwa na mkusanyiko wa wasanii maarufu duniani mwaka 1985 katika kuchangisha pesa za kusaidia wenye uhitaji barani Afrika.
NB: Sikiliza ubora wa uimbaji na vyombo bila kupoteza "ladha" ya wimbo wa awali.
Luciano ni zaidi ya msanii. Nina albamu zake 20 zenye zaidi ya nyimbo 400 lakini sijachoka kumsikiliza na haishi kunishangaza kwa uwezo wake.

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Albert Kissima said...

Ni kipengele kizuri kitujuzapo ni nini maana ya muziki na faida yake ktk jamii. Kipengele hiki binafsi chanihamasisha sana katika uchambuzi mzuri wa muziki kuanzia maudhui na uwakilishwaji mzima wa kazi hizi za fasihi.

Hongera kaka, na nakutakia wewe,familia yako kwa ujumla na wanablog wote mwaka mpya wenye mafanikio tele, amani, upendo na furaha.

Mija Shija Sayi said...

Mwaka huu lazima tufanye kweli.
Asante kwa kutochoka kutukumbusha.

Baraka na amani iwe kwako.