Sunday, February 14, 2010

Kweli twatofautiana kuwaza

Hii ya kwanza imenipambia wiki yangu. Kuona namna ambavyo wenye DHAMANA YA KUITANGAZA NCHI KWA USAHIHI wanaweza kuwa POTOSHO LA KUTUPWA kwa wanaopenda kujua ukweli wa nchi yetu. Nilipokuwa Facebook, nikatembelea ukurasa wa Uncle John Kitime na kukutana na maelezo haya ya aibu juu ya Ubalozi wetu hapa nchini Marekani. Ukiweza fuatilia maelezo yake nawe ujiulize WALIWAZA NINI kuandika UONGO HUU?
Maelezo ya Uncle John yanasema "Umekosa website za vichekesho? Basi google Tanzanian Embassy USA, kisha fungua ukurasa wa Embassy of Tanzania, fungua About Tanza...nia, halafu fungua People and culture hapo ndo utajua kumbe Ze Comedy wako wengi. Je ulijua kuwa Zouk na ndombolo ni tradional music wa Tanzania? Je ulijua kuwa Pilau kizungu ni wild rice? Je... ulijua chapati ni bread? Halafu kuna michapo mingine kuhusu mtunzi wa wimbo wa Taifa nk"
Bofya hapa usome kichekesho kisemwacho.
Na huu ndio ubalozi ambao umelalamikiwa kwa wafanyakazi wake "kujifanya" wako busy.
Image from Telegraph.Co.Uk
Juma hili pia tumesikia habari ya tajiri aliyeamua kutoa pesa yake yoote aliyonayo kwa maskini akisema PESA SI CHANZO CHA FURAHA MAISHANI. Akinukuliwa na gazeti la Daily Telegraph, Karl Rabeder amesema "My idea is to have nothing left. Absolutely nothing.... Money is counterproductive – it prevents happiness to come."
M-Australia huyu ameonekana kuwashangaza wengi ambao wameonekana kuwaza kuwa ALIWAZA NINI kufikia uamuzi huu? Lakini mwenyewe kaamua na anaona kuwa huu ndio uamuzi wa busara kufanya. Waweza kusoma habari kamili kumhusu HAPA Na mwisho kwa juma hili ambalo limenifanya kuwaza na kuona ni vema kuwahusisha ni kuonekana kwa video iliyosambaa duniani ukionesha wanajeshi na askari wa Nigeria wakiwaua raia wanaotii amri yao bila ubishi wowote.
Inasikitisha na kukufanya uwaze WALIWAZA NINI kuamua kuwaua ndugu zao ambao wengine ni walemavu? Katika wimbo wake wa VICTIMS, Lucky Dube aliimba akisema "Bob Marley said how long shall they kill our prophets
While we stand aside and look? But little did he know that eventually, the enemy will stand aside and look. While we slash and kill our own brothers knowing that already they are the victims of the situation"
Video ya tukio hilo (AMBAYO INASUMBUA KIDOGO KUIANGALIA) inapatikana HAPA

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

3 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka Mubelwa baada ya kufuata maelekezo yako nilitembelea tovuti hiyo. Ni aibu tupu. Sijui kama wahusika hawalioni kama ni tatizo? Ama wanaliona lakini hawajui kama ni tatizo. Upotoshaji ni jambo baya, lakini upotoshaji unaofanywa na taasisi nyeti ya serikali yenye dhamani ya kunyoosha mambo ni mbaya zaidi.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Usanii ama WIZI MTUPU!

Na kwa sababu hiyo ndo sababu wakenya, waganda, warundi na wanyarwanda wanatutangazia vivutio va utalii tulivonavyo kana kwamba hatuna wataalamu ama tunashindwa kuwatumia :-(

Mie nilidhani kuwa ni katika madini na nishati tu ndo tunaboronga kwa kuwa na mikataba mibovu kumbe na katika maswala mengine ni vihiyo?

aaagh!

PASSION4FASHION.TZ said...

Kweli inasikitisha ni aibu tupu,hivi waliwaza nini?