Sunday, February 21, 2010

Mawazo ni nywele, kila mtu ana yake.......

Suala la mauaji yaliyotokea mkoani Mara yameonekana kutawala habari katika sehemu na majadiliano mbalimbali. Binafsi iliniuma saana kuona watu 17 wakiuawa kikatili. Lakini nilipoona VIDEO ya ripoti yake niliwaza mara kadhaa juu ya walilowaza kabla ya kutenda haya. Niliwaza juu ya wahanga walivyoshituliwa na muingilio wa wauaji hao ndani ya nyumba, walivyolia kuomba msamaha, kulilia uhai wao. Niliwaza kuhusu watoto waliokatishwa maisha yao. Nimewaza na kuwazua lakini bado naishia kubaki na swali kuwa waliotenda haya WALIWAZA NINI?
Ni vipi tunajipoteza katika harakati za kutafuta uwezo wa ajabu uliomo ndani mwetu?
VIDEO ZILIZOPO KATIKA LINK HII YA DADA SUBI (Bofya hapa kuzitazama)ZINA PICHA ZA KUTISHA NA IKIWA HUNA UWEZO WA KUSTAHIMILI TASWIRA ZA MAUAJI, TAFADHALI USIANGALIE
Pole saaana kwa wafiwa!!!

Juzi wakati natembelea ukurasa wa Facebook, nikakutana na ujumbe huu ambao umeandikwa na mtu ambaye hakupenda jina lake lijulikane (Anonymous). Ujumbe huu mfupi na ambao unaweza kuonekana kuchekesha lakini unaonesha kiasi ambacho watu wamechoshwa na siasa za viongozi wetu kiasi cha kuwaombea mambo mabaya. Labda kwa juu juu unaweza sema "huyu ana akili timamu kweli?" lakini binafsi najiuliza ALIWAZA NINI na mangapi mpaka kufikia hatua ya kuunganisha matukio yooote ya mwaka jana na sala zake za mwaka huu? Huyo anon ameandika "Lord! Last year you took my favourite musician Michael Jackson...My Favorite comedian Bernie Mac...My Favorite actor David Carradine...My favorite actress Farrah Fawcett...This year, I just want to let u know my favorite Politicians are KIBAKI,RAILA and RUTO.."- anonymous
ALIWAZA NINIIIIII?????
Huwa nawawaza wanasheria kwa kazi ngumu waliyonayo. Hasa wanapotakiwa kuwatetea wasio na hatia ambao wamewekwa mbele ya mkono wa sheria wakikabiliwa na uwezekano wa kuhukumiwa visivyo. Nawaheshimu pia kwa kujitahidi kuwaondoa kwenye jamii wale watendayo yasiyofaa.
Ninapojiuliza kuhusu kazi zao, ni pale ninapoona wanatetea ambacho machoni mwa wengine ni kama ucheshi katika uhalali na kuonekana kabisa kuwa kinachomfanya (wakili) ajikite humo ni PESA. Huwa najiuliza WANAWAZA NINI kupindisha ukweli kwa kutumia sheria ili MTEJA wao apate anachotaka? Juzi, Tiger Woods "aliomba msamaha" kwa aliyotenda. Na naamini alistahili kuwaomba msamaha wale wanaohusika na licha ya kutosikiliza msamaha wake (labda kwa kuwa hakunikosea), nilishangazwa na press conference iliyofanyika punde baada ya yeye (Tiger) kumaliza. Alikuja wakili wa mcheza filamu za ngono wa zamani akilalamika kuwa hajatajwa kwenye watu waombwao msamaha. Tena wakili anasema kuwa MTEJA wake (ambaye alikuwa akijua kuwa Tiger ameoa) alikuwa akimpenda saana Tiger na kulalamika kuwa aliaminishwa kwamba "she was the only woman in his (Tiger) life other than his wife" kisha akaendelea kusema "Veronica gave up her occupation, her primary source of income, the only source of income as a PORN STAR because Tiger was very jealous and he could not stand the fact of her being with another man"
Hili lanifanya nijiulize kuwa ni kweli kuwa huyu mama (ambaye anatafutwa huko Washington kwa kushindwa kulipa Chlid Support) hana kosa lolote katika hili? Hivi yeye anaamini kuwa anastahili kuombwa msamaha wa kipekee licha ya kuomba msamaha wa juu juu kwa wale alioshiriki kuwaharibia maisha kwa kujiingiza katika mkumbo wa kuwa mmoja wa wengi waliohusiana na Tiger?
Angalia Video nzima hapa chini, labda utapata jibu la swali langu kuwa hawa watu wawili WALIWAZA NINI kwenda mbele ya waandishi na kusema haya?

...Pia wiki hii nimeona bandiko kwa Kaka Michuzi juu ya ajali ya Lori la mafuta na gari ndogo. Kilichonisikitisha ni kuona wananchi wakiendelea kuhatarisha maisha yao kwa kuiba mafuta yanayomwagika, yanayoweza kulipuka na kuleta maafa.
WALIWAZA NINI? Tazama picha hapa chini uwaze. Bahati nzuri hakuna aliyekwenda kuiba mafuta akiwa na sigara mdomoni. Picha zote na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.


***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***


2 comments:

Faith S Hilary said...

I love this week's "waliwaza nini" maana kuna vitu vya kuchekesha na kusikitisha humo humo...

Mie kaka ningependa kucheka tu (it's what I do best lol) na the highlight ilikuwa huyo bi dada porn star aliyelalamika kuwa Tiger hakumtaja yeye kwenye public apology. When I saw this video nilicheka mpaka machozi. Yaani mwanaume mwenye mke na mtoto anakwambia hivyo then with your full human being's mind, you actually BELIEVE it??? Mmh...speaking of attention seekers man...all them women including her.. were suppose to apologise to him privately for ruining his life...anatuaibisha wanawake (girls?) wenzie kuonekana desperate hivi, kwani kuna mwanaume mmoja tu dunia hii...

Na hao wanaoiba mafuta...wasn't surprised maana hicho ndio wanachofikiria watu badala ya kufikiria usalama wao. Ndio yale yale yaliotokea Dar mwaka jana kwenye "shoot out" kati ya polisi na majambazi. Ila najiuliza ni "third world countries" people who do this ama vipi? Maana nilikuwa naangalia kipindi ambapo walionyesha chui katoka alikotoka akaingia mjini, nadhani ilikuwa India. Watu badala ya kukimbia, wamemzunguka chui as if it was a cow or something...Najiuliza tu...

Mzee wa Changamoto said...

This was touchy Dada. Ilikuwa ngumu hata kuikusanya. Lakini ndio mawazo kuwa WALIWAZA NINI? Kakangu Sheby kasema ime-make his day nami nimebarikiwa na hilo.
Lakini huyu mdada wa Tiger amenisikitisha. Yaani anajiona special wakati wako kama 13. Kwa lipi?
Hao wa Tiger wameniacha hoi. Nadhani walitaka kusimulia kifo (wakasahau kuwa ukisimulia kifo lazima uwe umekufa na ukifa huwezi kusimulia anymore)
Ila ni kweli kuwa WALIWAZA NINI?
Sijui nami niliwaza nini kuwaza walilowaza.