Monday, February 22, 2010

Tanzania Yangu....Yenye wabunge wa wananchi wawanyonyao wananchi.

"The wickedman ain't got no love for humanity, yet they got so much love for their vanity. Their need for way is rising high, while the sufferers are left to die (in starvation and hunger). Vote for me i'll set you free, are lies and hypocrices" Nasio Fontaine
Nimeandika nukuu ya Nasio hapo juu baada ya kusoma kwenye mtandao wa gazeti la Mwananchi kuwa Kila mbunge kuvuna Sh 46 milioni za kiinua mgongo. Ni asilimia 40 ya miashara yate ya miaka mitano.(Bofya hapa kuisoma)
Imeeleza kuwa malipo hayo yatafanyika baada ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Julai mwaka huu na pesa hizo zitakuwa kwenye akaunti za wabunge hawa kati Julai na Agosti.
Kwangu mimi, habari hii iko VERY DISTURBING na si kwa kiwango cha malipo, bali uharaka wake ukilinganisha na maelfu ya waTanzania ambao wanasumbulia miaka miiingi kabla hawajapata mafao yao.
Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah (katika toleo la gazeti la Mwananchi), "Mimi si msemaji wa Bunge lakini, kwa kukusaidia tu fedha hizo zitalipwa baada tu ya rais kutangaza rasmi kulivunja Bunge. Wabunge watazikuta fedha hizo kwenye akaunti zao kati ya Julai na Agosti," Yaani ndani ya mwezi mmoja watakuwa wamelipwa pesa zao.
Kinachonichefua ni kuona hawa wabunge wakiwaangalia wazee wetu ambao wameitumikia Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakihaha kupata mafao yao kwa miaka nenda rudi na bila hata aibu watapokea mafao yao muda mfupi baada ya bunge kuvunjwa. Tena si mafao tu, MABILIONI YA SHILINGI ndani ya muda mfupi.
Wabunge wanawaangalia askari (wanaowalinda baadhi yao walalapo kwenye nyumba zao za thamani na ambao ndio tuwategemeao kupambana na rushwa na ufisadi) wakiishi maisha ya dhiki na duni ilhali wao wanakusanya mamilioni kuwawezesha kuhonga wananchi ili kurejea madarakani.
Wabunge wanawaangalia waalimu wakihenya na mazingira duni ya kazi na miezi kede wa kede wakifuatilia mafao yao , ilhali wao wanayakuta ndani ya mwezi mmoja tena kwenye akaunti zao. Ninaye ndugu ambaye ameitumikia nchi kwa uaminifu kwa zaidi ya miaka 30 kama mwalimu wa ngazi ya juu. Amestaafu na kulazimika kutumia zaidi ya mwaka na nusu kufuatilia sehemu ya mafao yake. Mafao yake halali. Na nilipowasiliana naye alinieleza namna ambavyo mwenzao (mfuatiliaji mafao) ameshindwa kuvumilia na kushindwa kumudu gharama za kukaa Dar KUSUBIRI FAILI LAKE LIPATIKANE na hivyo kuna uwezekano akapoteza mafao yote. Hivi inakuwaje wabunge wanapokea mafao haraka namna hiyo ilhali watu ambao wamejulikana kuwa anastaafu wanazungushwa kwa kisingizio kuwa "FAILI LINATAFUTWA". Huyu alitoka Kagera. Mnategemea anaishi vipi "mjini" Dar Es Salaam? Na kwanini mafao yake ayahangaikie na kuyafuata Dar wakati tunasoma kuwa ya wabunge yatakuwa kwenye akaunti zao Julai ama Agosti? Ha hizo pilika za kila siku "njoo" kufuatilia. Hivi WIZARA YA ELIMU INA UKUBWA GANI WA KUSAKA MAFAILI YA WATU KWA ZAIDI YA MWAKA MZIMA?
Najua kuwa wabunge hawajali well being ya wale wanaohangaika kuijenga nchi. Waalimu, watumishi wa ndani (ambao wamewalea wakiwa watoto na bado wanawalelea watoto wao wanapokuwa bungeni), wauguzi na wengine.
Katika wimbo huohuo wa Nasio ameendelea kuwaeleza kuhusu hawa HYPOCRITES kuwa "You talk about this, you talk about that. Poor people just a suffer (are suffering) while you live out FAT.......You living in your false pride and Luxury, while millions (are) dying in their poverty"
Haya ya wanasiasa kuwa na UROHO pia yalielezwa na Culture katika wimbo wake Time is getting harder aliposema "People are Dying,little babies are crying their hearts carries no sympathy. So think about the greedy, they leave nothing for the needy"
Hata MORGAN HERITAGE walisema katika wimbo wao Politician kuwa wabunge wetu "they use us as cones in the game of chase".
Ni hawahawa wabunge walioshindwa kutupa majibu ya maswali yetu yanayoulizwa tangu enzi. Innocent Galinoma kwenye wimbo wake AFRICANS alisisitiza akisema "tell the children the truth...... What's going on with their economy? Rain is falling but there is no food. WHY? Where is Justice? Where is equality? Why there is murder, poverty and blood everywhere? Where is education, medication for my children?"
Shame on them all
Sikiliza wimbo huu NO LOVE wa Nasio ..JIKITE ZAIDI KATIKA MANENO YAKE UKIWEZA



Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA


Tuonane "Next Ijayo"

5 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

First born wa familia yetu alifariki miaka mitatu iliyopita na alikuwa mtumishi wa serikali tena aliyekuwa anakaribia kustaafu. Mpaka leo watoto wake bado wanapigwa danadana. Mara leteni nyaraka hizi kutoka kwa balozi wa nyumba kumi na mkuu wa kitongoji, mara nendeni makao makuu mkaonane na mkuu wa utumishi...Mpaka naona watoto wake sasa wamekata tamaa. Sitashangaa kama kiinua mgongo cha marehemu kilishatolewa na mtu keshajengea banda la kuku tayari. Nimepanga nikienda huko hata kama ni kutinga mpaka ikulu nitatinga ili kujua kinachoendelea kuhusu suala hili. Kumbe waheshimiwa wenyewe haichukui hata mwezi kupata kiinua mgongo chao - ambacho sina uhakika kama wanakihitaji/wanastahili.

Ni yale yale ya mwenye nacho...

Albert Kissima said...

Kwa kweli serikali yaonyesha dharau ya hali ya juu kabisa. Ni ishara ya wazi kabisa kuwa serikali ya Tanzania ni kwa ajili ya wachache.

Nina maswali mawili kwa wabunge.

Wao wanalichukuliaje au wanaliongeleaje hili kwa kuzingatia kuwa wao wanayajua matatizo ya wananchi?(ninategemea hivyo lakini si lazima iwe hivyo). Pili, kiuzalendo,hawawezi kuyakataa hayo mamilioni ili washinikize serikali kushukulikia kwanza madai ya wastaafu,walimu pamoja na matatizo mengine sugu kwa kuzingatia kuwa pesa zao zipo na watazipata tu?

Mzee wa Changamoto said...

Pole saana Kaka Mtondo. Ninaloweza kukutakia ni mafanikio katika hili.
Wenzetu (sorry, najua hawa wabunge si wenzetu) wanainuliwa wasipostahili, lakini wanalofanya halistahili.
Wanasikitisha saaaaana

Kaka Albert. Utu / Uzalendo ndio kitu wasichonacho hawa "waheshimiwa"

Albert Kissima said...

Ni kweli kaka, uzalendo/utu ndio hasa waukosao. Hata sisi wananchi vilevile tunakosa elementi hiyo hiyo. Wakenya wapo tofauti sana na sisi waTanzania. Ni warahisi wa kutetea haki zao kwa mshikamano kwa kuilazimisha serikali kutenda yale wasiyotaka kuyatenda kwa manufaa yao binafsi. Tunaona mpango wa elimu kwa wote nchini Kenya. Kuna ndivyo sivyo ziingilia kati lakini wananchi wamekuwa mstari wa mbele sana ktk kulifuatilia hili na mwisho hata wafadhili wa mradi huu wakagoma kuendelea kuufadhili. Mimi najiuliza sisi watanzania tunatofauti gani na wenzetu waKenya? Unyenyekevu wetu wa kinafiki ndio hasa unaotuangamiza,twalewa na nadharia ya kuwa, nchi yetu ina amani wakati watu wanapigwa danadana kwenye ulipwaji wa mafao,malimbikizo ya mishahara,ubinafsi wa wazi kabisa uonyeshwao na serikali yenye kivuli cha demokrasia,uwazi na usawa wakati ni ya kibaguzi, umasikini,matabaka makubwa kati ya matajiri na walala hoi,na mambo mengine chungu mbovu! Ni masikitiko kwa hakika. Kaka sisi wenyewe(wananchi walalahoi) hatutakuwa wanaharakati wa kweli,ni dhahiri kuwa tutaendelea kunyonywa na kukandamizwa kwa kuzingatia kuwa hata wale tuliowaamini na kuwachagua kama watetezi wetu nao wanatugeuka na kuungana na wanyonyaji kutuvyonza damu kidogo iliyobakia itupayo uhai.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Dkt Matondo, pole sana kwa masaibu hayo.

Kusema ukweli hatuna viongozi bali watawala na wakoloni/wanyonyaji ndani ya ngozi ya 'viongozi'.

Tunazo sheria na sera mbalimbali ambazo hazitekelezeki. Ni rahisi kwa mbunge na waziri kukopa pesa nyingi tu katika mifuko ya pensheni kuliko kwa mlalahoi kupata mkopo toka kwa benki yoyote ile. Na utashangaa kuambiwa kuwa hata ulipaji wao wa mikopo unatia shaka.

Sina hakika kama mwisho unakaribia isipokuwa ninalojua ni kuwa upo mwisho wa yote hayo, nao si mbali sana :-(