Wednesday, February 24, 2010

Wanasiasa wetu na sakata la Ushoga / Usagaji

Image from Queers United Blog
Oktoba 13 2009 Mbunge wa chama tawala cha NRM Mhe. David Bahati aliwasilisha mswada katika Bunge la nchini UGANDA ambao kama utapitishwa basi utawaadhibu MASHOGA NA WASAGAJI walio nchini Uganda na wenye asili ya Uganda kwa adhabu mbalimbali kuanzia kifungo mpaka kifo. Mswada huu umewasilishwa kwa kile kilichosemwa "strengthening the nation’s capacity to deal with emerging internal and external threats to the traditional heterosexual family" na licha ya kuungwa kono na Rais, bado unasubiri mchakato mzima wa kujadiliwa bungeni unaotarajiwa kuanza wiki chache zijazo.
Lakini binafsi napenda kuangalia suala hili kwa JICHO LA NDANI.
KWANZA kabisa niseme kuwa SIUNGI MKONO KWA NAMNA YOYOTE ILE SUALA ZIMA LA TABIA ZA KISHOGA NA USAGAJI lakini bado naamini kuwa baadhi ya WANASIASA (na viongozi wa Dini) wanataka kutumia suala hili kwa manufaa yao binafsi badala ya kuleta SULUHISHO KWA JAMII YETU.
Tuanze kwa kutambua kuwa MASHOGA NA WASAGAJI ni wenzetu, waliozaliwa katika familia ambazo nyingi ni za watu wasio mashoga wala wasagaji. Kwa hiyo kama wamezaliwa katika familia zilizo tofauti na walivyo leo, NI LAZIMA TUJIULIZE kuwa NI WAPI TULIPOJITENGA NAO NA KUWAFANYA / KUWAACHA WABADILIKE NA KUWA WALIVYO?
Sisi kama JAMII TUNA SEHEMU YA LAWAMA kwa kuwa ama hatuwasaidii kutokuwa walivyo, au tunachochea kuwa walivyo hata kama twatenda haya bila sisi kujua.
Suala hili la USHOGA NA USAGAJI halijaanza leo wala mwaka jana ambapo wanasiasa wameonekana kulivalia njuga. Nakumbuka nikiwa mdogo tulisikia utani wa "kushikishwa ukuta huko Lamu" na baada ya kukua na kung'amua nikajua kuwa ni suala la USHOGA NA USAGAJI lakini hakuna aliyethubutu kujadili nasi kuhusu suala hilo mpaka leo hii ambapo mambo yanaonekana kuwazidi nguvu naanza kuwaona WANASIASA wakija na hatua zao za zimamoto ambazo zinafikia hatua ya kuwaadhibu hata wale watakaoshindwa kuwataja mashoga na wasagaji wawaju.
TATIZO KUBWA NI MOJA KWA NCHI ZETU ZA KIAFRIKA.
Hakuna kiongozi anayetaka kujishughulisha na chanzo cha tatizo. Wanakurupuka kwa namna za KUAHIRISHA tatizo na kisha kutumia uhahirisho huo kujipatia kura za kurejea madarakani. Kisha tatizo larejea. Wakati nasikia habari za kile nilichokuja kung'amua kama matendo ya kishoga na usagaji nilikuwa mdogo, na nina imani kuwa walikuwepo mashoga na wasagaji wachache saana ukilinganisha na sasa lakini kile wanachokiita "mila za kiAfrika" ziliwazuia wazazi, walezi na viongozi kujadili ATHARI za kujikita kwenye tabia mbaya kama hizo na matokeo yake ndio tuonayo sasa ambapo tatizo hili LIMEOTA MIZIZI na twasikia harakati za KUWAFUNGA NA KUWAUA. Kisha baada ya hapo?????
Kwa jamii yetu (NA HASA HAWA WATAWALA),kuna haja ya KUANGALIA MAMBO KWA UHALISIA WAKE na kuangalia athari za uwepo na usambaaji wake kwa miaka kadhaa ijayo. Leo hii twasikia Uganda wakipanga kuwafunga na kuwaua mashoga na wasagaji lakini hatujaambiwa kuwa baada ya kufungwa ama kuuawa kuna mikakati gani kuhakikisha kuwa hawatarejea tena... Ama ndio uleee utaratibu wa kisiasa wa TUWAUE KISHA WAJE WENGINE WAJIKUSANYE TUWAUE NA WAJIKUSANYE TUWAUE TENA?
BINAFSI NAPENDEKEZA MAMBO MAWILI KUTENDEKA KABLA SERIKALI HAZIJAANZA KUWAUA HAWA MASHIGA.
Kwanza ningependa Mhe David Bahati (ambaye ndiye aliyependekeza muswada wa Uganda) auambie umma wa Uganda na ulimwengu kuwa wamejiandaa vipi kuhakikisha kuwa wakishawafunga na kuwaua hawa mashoga na wasagaji waliopo nchini Uganda (wanaokadiriwa kuwa 500,000 kati ya milioni 31. Sawa na 1.6% ya wananchi wa Uganda) hakutakuwa na kujitokeza kwa mashoga na wasagaji wapya? Yaani aeleze kuwa kuna hili na hili na hili ambayo yakitendeka yatazuia kujitokeza kwa mashoga na wasagaji wapya. Kama hilo halipo, ina maana litakalotendeka ni kuua waliopo kisha wajikusanye tena wauawe na tena na tena na hapa sheria haitakuwa na msaada kwa mwananchi kwani watu hawa (mashoga na wasagaji) hujiingiza katika tabia hizo kwa sababu tofauti.
Lakini pia ninaweza kuhakikisha kuwa kati ya wabunge wanaotaka sheria hiyo ipitishwe na watu hawa wafungwe ama kuuawa, kuna uwezekano mkubwa kuwa hakuna hata mmoja ambaye ameshakutana na hawa MASHOGA NA WASAGAJI na kujaribu kutafiti sababu za wao kuwa walivyo na pengine kujadiliana namna ya kuwasaidia wabadilike. HAWANA MUDA NAO (kama ambavyo hawana muda nasi). Na pengine (ama kibaya zaidi) ni kuwa hawa wabunge waungao mkono muswada huu upite hakuna hata mmoja mwenye suluhisho la nini kifanyike wakishafungwa na kuuawa hawa waliopo.
Na pili ni kuwa VIONGOZI WETU WANAJITENGA NASI. Wanaishi kwenye "gated communities" tena mbali nasi wananchi. Hawachangamani nasi (labda kwenye matukuio muhimu na ziara za viongozi wa juu) na kwa mantiki hiyo HAWAJUI KEROO NA BUGUDHA ZA MASHOGA NA WASAGAJI (kama zipo) hivyo hawahusiki na karaha za uwepo wao. Kama ni kweli kuwa mashoga hawa wana kero na karaha, ama kama ni aibu kwa jamii, basi ni kwetu sisi tunaoishi, kuchangamana, kushirikiana na kusaidia nao katika maisha ya kila siku. Sasa ni kwanini wasiliweke hili suala la kuwafunga ama kuwaua kwenye KARATASI ZA KURA na wananchi walipigie kura uchaguzi ujao?
Wanajua kuwa katika maisha yetu ya kawaida, MASHOGA NA WASAGAJI wana msaada kuliko WANASIASA WETU na litokeapo tatizo unajua utajaliwa na hawa mashoga na wasagaji kuliko wanasiasa wasio na habari nasi.
Na ndio maana hawataki kuliweka kwenye karatasi za kura kwani wanajua kuwa watu watapinga "zimamoto" yao ya kujitafutia umaarifu.
Labda wawaze kuwa wapo maelfu ya mashoga na wasagaji ambao wanasaka misaada ya namna ya kuondokana na hisia za namna walivyo. Kama inayoonekana hapa chini kwa kijana Joey Heath anayesomea Master of Divinity katika Wesley Theological Seminary, Washington, DC ambaye ni shoga na ambaye amesema amekuwa akiomba Mungu kila mara kuponywa hali u-shoga aliyonayo. Mwenyewe anasema "I would pray every day that God would just heal me of this, this evil part of me, and that this would be just removed and I would be cleansed and made whole again."
Waweza kuBOFYA HAPA kuangalia video hii kama imegoma kuonesha hapa chini.


Na huu ni MTAZAMO wangu kulingana na namna nilionavyo tatizo. Labda namna nionavyo tatizo ndio tatizo

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimeipenda hii habari ya kufunza. Kwanza kabisa mtu huwezi tu kuamua kumuua mtu kwa sababu ni tafauti na wewe, na pia kila mtu amezaliwa kama alivyozaliwa, na halafu huwezi kumbadili mtu kama hujajibali wewe mwenyewe. Inaonekana wanasiasa wetu hawana kazi muhimu za kufanya. Sio kwamba nawatetea mashoga/wasagaji hapana ila wao wapo kama walivyo na hawakuchagua kuwa hivyo na wala sisi hatukuchagua kuwa sisi.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Kama wanasiasa wanatumia fursa hizo kwa kuwatumia wanyonge kupata wanachotaka....

Kwa nini wanyonge wasitumie fursa hizo hizo kugundua kuwa wanasiasa si watu wa kuamini na kuwaondoa madarakani?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ushoga, usagaji nk, wangeichukia rushwa hivyo, sijui ingekuwaje!

Sisulu said...

ngwanambiti bila wana siasa hatupati viongozi!