Wednesday, February 10, 2010

Pale msaidizi umtegemeaye anapohitaji msaada.

Image by Kim Hairston of Baltimore Sun
Kwa wenzetu waishio nchi zenye huduma ya 911 (ifanyayo kazi kama inavyostahili) wataelewa umuhimu wa hawa waokozi. Vikosi vya uokozi na zimamoto vimekuwa msaada wa watu kwenye mambo mbalimbali kuanzia wagonjwa mpaka wadudu na wanyama ndani ya nyumba.
Lakini pia itokeapo dhoruba kama mafuriko ama theluji, basi hawa ndio watu ambao huwezeshwa kufika sehemu zote kutoa msaada.
Sasa leo hii DHAHMA YA THELUJI imeanza kwa kuwatenganisha wakazi wa Dundalk hapa Maryland na waokoaji hao.
Snow iliyomwagika tangu mwisho wa wiki na kuongezeka leo (na inategemewa kuendelea mpaka usiku) imesababisha moto ulioangusha paa la jengo na na kuharibu sehemu ya jengo lenyewe la waokozi hao na pia kuharibu INJINI 2 ZA ZIMAMOTO, MAGARI MAWILI YA MATIBABU, GARI YA KUSAFISHA NJIA NA HUMVEE moja. Moja kati ya injini hizo iliyoharibika kabisa ilinunuliwa wiki iliyopita kwa gharama ya dola laki sita ($600,000)
Naomba na kutumai kuwa wakazi wa eneo hilo hawatapungukiwa huduma wakati huu wa uhitaji kutokana na uharibifu huo.

Video toka WBLTv

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Aise! afadhali ya sisi huku, Poleni sana. Upendo Daima!!