Friday, February 12, 2010

Apumzike pema peponi Mama Saria

Maisha ni mzunguko na kila mtu ana sehemu yake kushiriki. Wapo walioweza kuitwa ndani ya muda mfupi, lakini pia wapo ambao wameweza kuwa sehemu kubwa ya maisha yetu. Wakiwa WAZAZI NA WALEZI wetu na pia mifano katika maisha ya kila siku.
Ni hawa ambao wanatufunza meengi na wanatimiza sehemu kubwa ya maisha yao wakituandaa kuwa WATU BORA MAISHANI.

Ni hawahawa ambao wanakesha na kushinda mchana kutwa wakituonesha mapenzi ya dhati na ambao bila kuchoka wanajitahidi kutuonesha upendo na malezi mema.

Ni hawa ambao HATUTAKI WATUACHE KWANI TWAPENDA UWEPO NA MSAADA NA USHIRIKIANO WAO KWETU.

Lakini ni hawa wanaohitaji kupumzika muda wao ukifika. Na ni hawa ambao wakienda kupumzika, twastahili kuwakumbuka na kuwashukuru na kuwaombea na kuwatakia mapumziko mema.

Leo hii, naungana nawe Kaka Israel Saria katika wakati huu mgumu kumkumbuka Mama mzazi aliyetangulia mbele ya haki. Lakini naamini kuwa amemaliza jukumu kubwa na sasa amekwenda kupumzika, nasi tuliosalia twahitaji kuonesha kile alichokifanya kwa kuenzi wema wake.

POLE SANA KAKA NA MUNGU AKUPE UJASIRI WA KUKABILIANA NA UPYA HUU WA MAISHA

NA KWA MAMA, UPUMZIKE MAHALA PEMA PEPONI

AMEN

3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Pole Bwana Saria. Mama jukumu lake alilitimiza na sasa ameenda kupumzika. Hebu na Apumzike kwa amani. Bado anaishi kupitia kwenu wanae. Endelezeni mema yake na kila siku mtakuwa naye. Amen!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Apumzike kwa Amani! Amina

Yasinta Ngonyani said...

Pole sana kaka Saria na Mwenyezi Mungu akupe nguvu, imani na ujasiri katika kipindi hiki kigumu. Apumzike kwa amani Amina.