Friday, February 26, 2010

Them, I & Them. LUCKY DUBE .........Crime And Corruption

"Do you ever worry about leaving home and Coming back in a coffin, With a bullet through your head. So join us and fight this Crime and Corruption"
Hayo ni maneno ambayo ni kama yalitabiri mauti yake mwenyewe miaka 8 kabla hayajamkuta. Ni kutoka katika wimbo wa Crime and Corruption uliko kwenye albamu ya The Way It Is na ambacho pengine ndicho kilichotokea kuwa maarufu na kutiliwa umakini na walimwengu wengi mara baada ya kifo chake. Sababu kuwa ni namna alivyoeleza matukio yanayomsikitisha na kuendelea kufumbiwa macho na viongozi jamiini mwake. Lucky amewalilia viongozi kuacha kupuuzia hali halisi ya Rushwa na Maovu katika jamii yake na kukutana na wahanga wa matatizo hayo jambo ambalo aliamini labda lingefungua mioyo ya viongozi na kuendeleza kampeni za kupinga mambo hayo. Ukiusikiliza kwa makini, Lucky alianza na swali kwa "waheshimiwa" akitaka kujua sababu hasa inayowafanya wasione ukweli juu ya wakulima na askari wanaouawa kila siku huku wao (viongozi) wakitoa ripoti kuwa hali si mbaya na anawauliza " Is it the bodyguards around you,Is it the high walls where you live,Or is it the men with the guns around you twenty four hours a day;That make you ignore the crying of the people?..."
Ni ukweli ambao aliuimba na kwa bahati mbaya saana ndiyo yaliyomkuta miaka minane baadae pale alipouawa katika aina ya uovu ambao si mgeni na umekuwa ukikemewa saana nchini Afrika Kusini. Aliimba katika kibao hiki juu ya wizi wa magari uliokithiri ambao wakati mwingine unafanyika mchana kweupe tena kwenye barabara kubwa kama Highway 54. Hiyo ni hali halisi ambayo hata baadhi (wengi) ya watu walioihama Afrika kusini wanasema wamekimbia maovu kama hayo na hata Kampuni ka bima ya Hollard Insurance iliamua kutowekea bima magari ya Volkswagen Citi Golf kutokana na kuibiwa sana nchini humo (bofya HAPA KUSOMA)
Lakini kama askari halisi wa Reggae na ambaye alikuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge, Lucky Dube aliweza kuimba haya na mengine mengi katika Albamu yake hii ya The Way It Is ambayo viongozi wengi waliamua na bado wapo wanaofumbia macho huku uovu huu ukiendelea kuziathiri jamii zetu barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

RUSHWA na MAOVU ni kati ya mambo aliyoyapigania saana Lucky Dube, na leo bado vyaendelea KUMUNG'UNYA MATAIFA MEEENGI BARANI AFRIKA.
Kati ya yale yaumizwayo na RUSHWA ni Tanzania Yangu ambayo wananchi wameamua kuona Rushwa kama sehemu ya maisha na njia katisho kupata haki zao ilhali watawala na wenye mamlaka mbalimbali wanatumia Rushwa kama "kijazio" cha mshahara wao.
Is it the bodyguards around you
Is it the high walls where you live
Or is it the men with the guns around you
Twenty four hours a day
That make you ignore the crying of the people
Farmers get killed everyday
And you say it is not that bad
Policemen get killed everyday
And you say it is not that bad
Maybe if you see it through the eyes
Of the victims
You will join us and fight this

Chorus:
Crime and corruption

Do you ever worry
About your house being broken into
Do you ever worry
About your car being taken away from you
In broad daylight
Down highway 54
Do you ever worry
About your wife becoming
The woman in black
Do you ever worry
About leaving home and
Coming back in a coffin
With a bullet through your head
So join us and fight this

Chorus:
Crime and corruption


Blessings
**Them, I & Them ni kipengele kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**

4 comments:

Albert Kissima said...

Natamani kitu kimoja tu! Unyenyekevu /utii unaoonyeshwa na watu wawapo ktk vyumba za ibada, ungeokuwa-practiced hata kwa binadamu wawapo nje ya nyumba hizo,naamini kabisa dunia ingekuwa mahala bora sana pa kuishi. Wauwaji, waendesha maasi,wachawi,majambazi n.k wawapo ktk nyumba za ibada huonyesha utiifu na unyenyekevu wa hali ya juu. Inaonyesha namna walivyojikita ktk imani zao waki-reflect yale wayaombayo kwa Mungu. Hali hii yadhihirisha fika kuwa binadamu wa aina hii hana imani kabisa na binadamu mwenzake bali imani yake kaielekeza kwa Mungu pekee,jambo ambalo binafsi naliona ni tafsiri potofu ya nini hasa lengo la imani za kidini tulizo nazo. Namaanisha kuwa,imani tulizojaaliwa na mwenyezi Mungu tusimrudishie yeye,tuzielekeze ama tuzitumie kwa binadamu wengine. Kwa jinsi mambo ya kiimani yalivyo,si jambo la kushangaa sana pale utakapoona mtu anashambuliwa kwa kuwa tu kalisema vibaya jina takatifu ktk imani fulani,na pia ikaonekana jambo la kawaida kabisa binadamu wa kawaida kufanyiwa unyama wowote na bila hata hatua yoyote kuchukuliwa.


Imani ni tabia,huzaliwa na pia hufa hivyo, viongozi wetu wajenge imani kwa wale wawaongozao,na wale waongozwao vilevile, binadamu kwa binadamu wajengeane imani thabiti kama ile imani iliyopo kati ya wanadamu na Mungu. Tukiweza hili naamini hakutakuwa na rushwa,ufisadi,unyang'anyi,mauwaji ya kinyama n.k. Usawa utakuwepo. Nafahamu ni vigumu lkn kama nilivyotangulia kusema,imani inazaliwa hivyo twaweza kujijengea imani mpya kabisa.


Binafsi nakushukuru sana kaka,kwani kila kukicha unatuonyesha umuhimu wa music ktk jamii. Niseme tu kuwa hata miziki ya bongo fleva,bolingo,zuku,taarabu n.k nazo zikipata mtu wa kuzichambua kama afanyavyo kaka kwa miondoko ya Rege,nayo bila shaka umuhimu wake utaonekana na jamii itatambua zaidi umuhimu wa sanaa hii ya Music na namna sahihi ya kuichambua.

Anonymous said...

Kwangu mimi alikua best singa wa rege nyimbo zake ni nzuri sana maneno yake ya kufahamika na ya ukweli, kwa nini wamemuua binadamu wana roho mbaya jamani.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kwangu mimi Lucky Dube ni mwana reggae bora kabisa wa Afrika na mpigania uhuru makini ajabu. Ndiyo maana nilisikitika sana alipouawa tena kwa sababu za kipumbavu kabisa - gari!

Bwana Kissima - unafiki ni sehemu ya binadamu. Ndiyo maana navutiwa sana na matendo tunayofanya sisi "Homo Sapiens". Inashangaza kama nini kumwona baba askofu amevalia joho linalomeremeta katika "utakatifu" na hata kuungamiwa dhambi - kumbe naye huku pembeni anaendeleza libeneke la kulawiti vivulana vilivyojitolea kutumika altareni! Unafiki umetanda kwa kila binadamu na mimi huwa nauongeza kama sifa mojawapo zinazompambanua binadamu na viumbe wengine. Bwana Kissima, wewe huna kaunafiki japo kadogo? Ati, mabinti wote uliowahi kuwatamkia kwamba unawapenda kiasi cha kuufurisha moyo wako fufufu kabisa na kukuacha ukiwa huna "appetite" ya kula au kulala ni kweli wote ulikuwa unawapenda (kiasi hicho)?

Pengine ni viwango vya unafiki ndivyo vinavyotofautiana kulingana na nafasi ya mtu aliyonayo katika jamii. Kwa hiyo liusaliti la mwanasiasa fisadi anayetiririkwa na majasho jukwaani na kutokwa na mapovu mchafukoge akihubiri usawa na kuahidi vita vikali vya kimsumeno kupambana na rushwa lina athari kubwa zaidi katika jamii kuliko kausaliti kako ka "sili silali" na "Maimuna, naapa uko peke yako mtimani mwangu"

Ndiyo maana naupenda sana wimbo wa "Utanitambuaje Kuwa Nimeokoka" wa Bonny Mwaitege kwani unagusia jambo la msingi sana. Ulokole (au shughuli yo yote) si maneno bali MATENDO. Na kwa kuwa njia kati ya azimio na kitendo ni ndefu hapo ndipo kizungumkuti cha unafiki kinapoanzia.

Hitimisho: Daima mtazame BINADAMU kwa jicho la hati hati hata kama ana cheo cha "Baba Mtakatifu"!

John Mwaipopo said...

naanza kwa kumnukuu dk matondo "...tena kwa sababu za kipumbavu kabisa - gari!". inasemekana hata majahili wale hawakujua walikuwa wanamuwinda lucky dube. eti walihamaki " we have killed the man!"

lucky dube was down-to-earth. ndio maana haishangazi kifo chake kilibashiriwa na nyimbo zake. wimbo mwingine ni crazy world.

like the anonymous above said, lucky dube shall remain high in the reggae business of out time.

unafiki ni sifa ya binadamu. viumbe visivyo binadamu si vinafiki. sidhani kuwa hakuna binadamu asiye mnafiki. binadamu anaweza 'kujinafiki' hata yeye mwenyewe. yafaa ifike sehemu viongozi wenye unafiki unaoonekana kwa macho tuwakatae. hawa ni wale wanapeana madaraka kwa kujuana, wanaopata madaraka kwa pesa, pesa ambazo ama walikwapua katika vihenge vyetu ama vyanzo vyake ni vya utata. tuwakatae viongozi wafitini, wakware, wanapependa sifa, washari, wasio na huruma na walipiza visasi