Sunday, February 28, 2010

Za Kale vs Maisha ya Sasa........KIPIPA AYUBU

Japo kuna kile kiitwacho maendeleo na mabadiliko, lakini si kwa kila kitu kihusucho maisha ya mwanadamu. Baadi ya tabia zimekuwa kero tangu enzi na enzi na nyingine zimekuwa zimekuwa zikiathiri maisha ya wanadamu mpaka sasa.
Moja ya TABIA zisizobadilika ni ile ya BINADAMU "KUENDESHWA" NA KIWANGO CHA PESA WALICHONACHO. Baadhi ya binadamu (na hasa vijana) wamekuwa wakibadilisha mfumo wa maisha kwa kuwa wamepata kiwango kikubwa zaidi ya pesa kuliko walichokuwanacho.
Ni haya ambayo yalikuwepo tangu kale. Ni mtazamo wa "matumizi kulingana na kipato" ambayo yameonekana kuathiri maisha ya wengi na ni maisha haya ambayo hata wasanii wa Orchestra Safari Sound waliyaona na kuyaeleza katika wimbo wao KIPIPA AYUBU.
Ukisikiliza wimbo huu wanazungumza athari za kuzusha sherehe na safari zisizo na malengo ili tu kutumia pesa. Wanamuonya Kipipa ku"chunga rasilimali isitetereke" kwani "ndio msingi wa Maisha".
Lakini pia wanamuomba Kipipa Ayubu kuongeza miradi kwa kuangalia Ufugaji na Kilimo.
Wasikilize wana OSS chini kabisa mwa post hii kujikumbusha miziki yetu ilyopendwa na bado inapendwa kutokana na UJUMBE NA MAFUNZO YASIYOISHA.
UJUMBE NDANI YA WIMBO HUU U-HAI LEO KAMA AMBAVYO ULIKUWA WAKATI UKIREKODIWA MIONGO KADHAA ILIYOPITA. Na ndipo tunapooanisha "Za Kale vs Maisha ya Sasa"
Kumbuka kuwa waweza kupitia matoleo mengine ya miziki ya "Zilipendwa" yaliyowahi kubandikwa bloguni humu kwa kuBOFYA HAPA, ama kupitia mitandao rafiki HAPA na pia kujua tasnia nzima ya muziki na wanamuziki wa Tanzania HAPA

2 comments:

jfk said...

Maadili ya Watanzania wakati ule yaliweza kuhamasisha wasanii kutunga maneno kama yale. Na ushauri kwa watunzi, ili wimbo wako udumu, tunga waza kwanza kabla hujafungua mdomo, usiwe kama kasuku anaesifiwa kwa kujua kusema lakini hakuna anayejali kumsikiliza ana sema nini.

Sisulu said...

naam naiona point mkubwa endelea kutupa changamoto