Tuesday, March 23, 2010

Dunia na maji yake

Picha hii ya maktaba yake mdau John Lukuwi ikimuonesha Rais Jakaya Kikwete akizindua mmoja wa miradi ya maji katika kijiji cha Kishishi wilaya ya Urambo mkoani Tabora
Jana ilikuwa siku ya maji duniani ambapo dunia imekumbushwa namna ambavyo upatikanaji wa maji safi na salama unachangia kwa kiwango kikubwa katika kuyaboresha maisha ya kila siku ya mwanadamu. Kwa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Michigan, 70% ya dunia "imekaliwa" na maji japo bado upatikanaji wa maji safi na salama ni tatizo. Takwimu hizo zasema 97.5% ya maji yote ulimwenguni na MAJI CHUMVO hivyo kuacha asilimia 2.5 tu ya maji yasiyo na chumvi. Na 70% ya hayo yasiyo na chumvi ni barafu ama katika maeneo ya Antarctica na Greenland na asilimia kubwa ya yaliyosalia yamehifadhika kama unyevu wa udongo ama yako kina cha mbali chini ya ardhi na hivyo kutopatikana kirahisi kwa matumizi ya binadamu. Bara la Afrika bado laonekana kuwa na kiwango kidogo saana cha upatikanaji wa maji safi na salama ukilinganisha na mabara mengine na hili laendelea kuwa tatizo kwa wana-Afrika wengi.
Data from United Nations Environment Programme, GLOBAL ENVIRONMENT OUTLOOK
Duniani, mpango wa malengo ya maendeleo kwa karne ama Millennium Development Goals (MDGs) umesema uko katika harakati za kupunguza idadi ya wahitaji wa maji safi na salama kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2015. Hii ni kati ya ile mipango minane iliyopangwa na viongozi wa dunia kuwa imepunguzwa kufikiwa nusu ifikapo mwaka 2015 japo yaonekana baadhi ya nchi za Afrika na hasa kusini mwa jangwa la Sahara ziko nyuma katika utekelezaji wake na haiaminiki kama zitaweza kutimiza lengo hilo la maji safi kufikia mwaka 2015. Lakini bado zipo nchi kusini mwa jangwa la Sahara ambazo zaonesha maendeleo makubwa katika suala la maji na mipango mingine. Feb 27 mwaka huu nilihudhuria Kongamano lililokuwa likijadili suala la MAJI SAFI NA SALAMA KWA BARA LA AFRIKA ambalo lilihutubiwa na watu wengi huku mgeni rasmi akiwa Balozi wa Jamhuri ya Liberia hapa nchini Marekani Mh. Nathaniel Barnes. Katika kuchangia huko, Dr. Carroll A. Baltimore Sr. ambaye ni Makamu wa kwanza wa rais wa Progressive National Baptist Convention, Incorporated (PNBC) alizungumzia uwiano wa gharama za utengenezaji wa maji ya chupa na usambazaji wa maji safi na salama kwa mamilioni ya watu kama asemavyo hapa chini.

Baada ya kongamano hilo, nilifanya mahojiano na Balozi Barnes na kumuuliza (pamoja na masuala mengine ya Afrika) suala la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wote barani Afrika. Tazama majibu yake hapa chini


BLESSINGS
Twahitaji kujitahidi kulipenda bara letu la Afrika lililo na vingi ili liweze kutusaidia.
Mzikilize Nasio akizungumzia upendo wa asili tulionao kwa bara letu la Afrika katika wimbo Africa We Love

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli ukija kwenye jambo la maji, nilikuwa siamini na wanangu walikuwa wananiuliza kila siku "mama lipi ni tatizo kubwa maji au Umeme" nikawa nashindwa kuwajibu mpaka jumamosi iliyopita ilipotokea kuwa hatukuwa na maji nilishindwa hata kunywa chai. Hakukuwa na maji kwa muda wa siku nzima. Na sasa najiuliza masaa 24 tu ilikuwa hivi je kwa wale wasio na maji na hasa maji safi na salama inakuwaje? KWA KWELI MAJI NI UHAI WA BINADAMU.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nayanazidi kupungua. ila mimi niliko kuna maji ya baridi na mengi hajabu. ukitaka kujua tatizo hili tembelea dar, mikoa ya kati uoone, maj ni kama dhahabu ila kwetu ni bidhaa ya kuchezea tu

Sisulu said...
This comment has been removed by the author.
Sisulu said...

soko ambalo halijagunduliwa hapa kwetu afrika mashariki ni maji ni ajabu lakini kweli kuwa jumuiya yetu imezungukwa na maji ya maziwa na mito yanayofanya sehemu kubwa ya maji ya afrika lakini watu bado hawana maji! si Kenya si Uganda si Tanzania! UCHUMI ULIO IMARA hautafikiwa kama nishati hii muhimu haipewi umuhimu wake. si ajabu kupita nairobi ama Dar es saalam na kukuta watu wana chota maji katika bomba lililo katika mitaani- la sivyo wanatwangwa bei za kuwaangusha na wauza maji wajanja. maji ni muhimu..DUNIA NA MAJI YAKE...tuamke...........