Tuesday, March 2, 2010

POLENI WASAFIRI, ATC & WATANZANIA KWA UJUMLA.

Kishaa......... Picha kwa hisani ya mdau ERIC via Michuzi Blog
Niliposoma kuhusu "KUTUA VISIVYO" kwa ndege ya shirika la ndege Tanzania ATC huko Mwanza nilisikitika. Nilisikitika kwa kuwa niliwawaza abiria, wafanyakazi na ndugu na jamaa zao ambao walikuwa na wasiwasi wa hali ya juu kuhusu usalama wao.
Kisha nikawaza kuhusu shirika letu la ndege la ATC.
Hapa kidooogo pakaweka kizunguzungu. Nimewaza kuhusu muda utakaopita kabla ndege hiyo haijarejeshwa angani (kama itarejea) na kwa muda huo ni wangapi wataweza kuendelea kuwa waajiriwa katika shirika hilo.
Baadae nikawawaza waTanzania wenzangu ambao kwa upungufu wa ndege hii (kati ya chache zenye nembo ya ATC) wataathiriwa huduma za usafiri iwe kwa ratiba ama gharama.
NA KWA WOOOTE HAWA NASEMA POLENI.
Na baada ya pole hiyo narejea kwenye swali la NINI KITAFUATA????
Naijua nchi yangu tukufu. Kuna ambayo naweza kuhisi ama "kutabiri" kuwa yatatokea. WANANCHI HAWATAJUA CHANZO CHA TATIZO, VIPI LIMETOKEA, WAPI LILITOKEA, VIPI LINGEWEZA KUEPUKWA NA NANI AMBAYE ANGEWEZA KUEPUSHA NA (kama yupo) ATAKAYEWAJIBISHWA KWA TUKIO HILI
Lakini swali la kwanza ni kuwa UTAFANYIKA UCHUNGUZI?
Uchunguzi ni muhimu kwa kuwa si katika "kumsaka mwenye makosa" bali kujua ni chanzo cha tatizo ambacho wakati mwingine si makosa ya fundi ama mtoa maamuzi.
Kakangu Profesa Matondo aliwahi kuzungumzia TAKWIMU ZA KUSIKITISHA KUHUSU NDEGE MBOVU ZIRUKAZO ANGANI (hapa) na alieleza kuwa ubovu huu si kwa ATC pekee, bali ni ulimwengu mzima. INASIKITISHA.
Ila kuna vitu ambavyo twapaswa kuviangalia kuona namna tunavyoweza kupunguza athari ya kinachoweza kutokea. Ndege tuliyosafiria MZA-BKB ikiwa tayari kutusafirisha Dec '07
"Mko tayari wanandugu?"
1: Uwanja wa ndege wa Mwanza (niseme JIJI LA MWANZA) ni kati ya viwanja vilivyo na idadi kubwa ya ndege za ndani na nje ya nchi aituazo pale lakini ukubwa na ubora wake ni wa kusikitisha. HAULINGANI NA GHARAMA ZA MALI NA WATU WANAOTUMIA MAHALA HAPO.
Zimamoto pekee UWANJA WA NDEGE NDULI IRINGA...Picha kwa hisani ya MATUKIO DAIMA BLOG
2: Vitendea kazi kwenye viwanja vyetu vya ndege ni va kusikitisha. Tarehe 20 Februari, Kaka Francis Godwin aliandika kuhusu VITENDEA KAZI DUNI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA NDULI (irejee hapa) ambapo taswira za kusikitisha zilionesha namna tusivyo tayari kukabiliana na janga lolote katika baadhi ya viwanja vyetu. PrecisionAir ikitua UWANJA WA NDEGE BUKOBA Dec '07
3:
Baadhi ya VIWANJA VYENYEWE ni hatari kwa matairi ya ndege zituazo. Nakumbuka nilipokuwa likizo mwaka Dec 2007, mkuu wa PrecisionAir alisema walikuwa wakifikiria kukatisha safari za Bukoba kutokana na hali ya uwanja. Sikujua walifikia muafaka vipi lakini japo nilisikitishwa na uwezekano wa maamuzi hayo, lakini NILIYAELEWA.
Lakini pia twahitaji kutafuta suluhu na wakati mwingine huja kwa njia iwasikitishao wengine japo ni vema kuwasikitisha walio na hatia kuliko kupoteza maisha yasiyo na hatia.
Natumai wananchi wataelezwa kwanini ilitokea ilivyotokea na kisha kujua ni vipi itazuiwa (kwa uwezo wa mwanadamu0 isitokee tena.
Kubwa kuliko yote TWASHUKURU KUWA HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA.

CHANGAMOTO YETU BLOG YATOA POLE KWA WASAFIRI, ATC & WATANZANIA KWA UJUMLA. Kishaa........... UCHUNGUZI UFANYIKE
BLESSINGS

4 comments:

Anonymous said...

На этом независимом новостном портале вы узнаете, что такое плагин Sape, настройка Wordpess%сайт сателлит. Кроме этого вы найдете для себя еще кое-какие завораживающие секреты успеха. Окунитесь в реальный мир, где электронные деньги становятся реальностью! Мы всегда ради вас приветствовать!

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu hakuna aliyepoteza maisha.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ilibidi wafe, walipona kwa bahati mbaya tu hawa

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kule kwenye blogu ya Florah ilitajwa eti injini ya kushoto ya ndege hiyo iliingiliwa na maji na hivyo kuzimika. Mimi nilijiuliza maswali mengi. Maji hayo yaliingia wakati ndege ikiwa angani au wakati imeshatua? Nimeshawahi kuruka na ndege wakati wa Hurricane moja hapa Florida na siamini kama maji ya mvua yanaweza kuingia kwenye injini na kusababisha izimike. Wahandisi mnajua. Pengine ndege hiyo ilizama katika dimbwi la maji hapo uwanjani kiasi cha maji kuingia katika injini. Kama ni hivi, kwa nini uwanja muhimu kama huu unakuwa na dimbwi la maji?

Hatutajua kilichotokea na hata kama kutaundwa tume, uzoefu unaonyesha kwamba ni kazi bure. Ati, ni kwa nini MV. Bukoba ilizama? Tunajua? Kwa kufichaficha haya mambo tunapoteza nafasi ya kuyazuia hapo baadaye. Pengine wachunguzi wa Boeing wakienda kuiangalia hiyo ndege yao itasaidia.

Kila ajali ya ndege inapotokea huwa ni nafasi ya watengenezaji wake kurekebisha makosa na kuendeleza kuuimarisha usafiri huu wa haraka, maridadi na kusema kweli salama. Tusipoteze nafasi hiyo katika ajali hii...