Thursday, March 4, 2010

Watu hutengeneza pesa,..... japo pesa zathaminiwa zaidi yao.

Kakangu Profesa Matondo amezungumza saana kuhusu "MNYAMA" huyu ajionaye ni kiumbe tawala zaidi duniani ilhali ana UPUNGUFU WA UTAWALA NA MAAMUZI YA KI-UTU. BinAdamu twajisemea kuwa "kiumbe" chenye akili na tunafanya meengi kudhihirisha hili. Na ni katika "akili" hizihizi tunapoonesha kutokuwa na akili kwa kutumia akili kuwafanya wenzetu wasiwe na akili ili tupate tutakacho.
Hapa sitarejea kwenye mjadala wa yatokako maradhi ya kutisha wala kuangalia vitengenezwako VIRUSI viharibuvyo kompyuta zetu kila siku. Sitazungumzia utengenezwaji wa mabomu na mambo kadhaa.
Labda nirejee kwenye makala niliyowahi kuandika March 24 2009 ikisema "Mimi na yeye sote tuko sahihi. Na sote hatuko sahihi" (Isome hapa). Katika "bandiko" hilo nilizungumzia suala la UTU na UHALISI WA MAISHA vinavyoweza kukinzana na kusababisha watu kuwa na usahihi katika upande wowote wa maamuzi. Ni juzi tu nilikuwa nimeketi nyuma ya kiTv changu nikiangalia mambo mbali kisha likaja suala la "gharama za matibabu". Nilipoangalia nikaingiwa na hofu kuhusu tunakoelekea. Na bahati nzuri bado nina kumbukumbu ya ghara halisi za kuzaliwa kwa Pau wangu (ambazo zilizidi dola thelathini elfu) kisha nikawaza. Hivi huduma ya hawa wenzetu huko kwenye vyumba vya upasuaji inapangwa na nani? Ni kweli kuwa wapangao haya wana utu? Ama wanasaka pesa zitengenezwazo na watu? Na hapo ndipo nilipoishia kuwaza kuwa labda mtu atengeneza pesa na kisha pesa hizo zakupangia kiasi cha utu unaostahili kuwa nao.
Tazama hizi video hapa chini toka CNN nawe ujiunge nami kushangaa..




2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

peas, money,, money. tukifa zabakia nyuma

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mfumo wa afya hapa Marekani umevurugika. Ni mfumo mbaya kabisa katika nchi zote zilizoendelea. Ulafi wa madaktari na makampuni ya bima ya afya umetawala. Kama huna bima au uwezo wa kujilipia basi unakufa tu na hakuna anayejali. Ndiyo maana wengi wanakimbilia Kanada na kwingineko.

Nina wanafunzi hapa ambao walifanyiwa matibabu ya meno wakati wakiwa Tanzania kwa sababu ya kuogopa gharama hapa.

Wewe fikiria tu hizo gharama ulizokumbana nazo ($30,000). Unafikiri Tanzania (kwenye hospitali nzuri) zingegharimu kiasi hani? Au Canada?

Obama anajaribu kuleta mabadiliko katika mfumo huu lakini kutokana na misukosuko anayokumbana nayo, mambo ni magumu na sidhani kama atafanikiwa...Na wakati mwingine wanaopinga mabadiliko anayoyapigania ni hao hao masikini ambao hawana bima. Inashangaza sana!