Kule Mtwara kuna mto waitwa LUKULEDI. Yaani Mto Lukuledi. Na hadithi niliyowahi kuipata ni kuwa mto ule uliitwa hivyo baada ya mzungu aliyekuwa ukingoni mwa mto huo (ambaye inasemekana hakuwa akijua kiswahili wala "ki-kwao" kumuona binti akizama na kisha kujitahidi kutotoa sentensi ndefu na kuwaonesha waliokuwepo pale kuwa "look..Lady is drowning" [usiniulize kuhusu usahihi wa Sarufi (grammar)] lakini nilichosimuliwa ni kuwa "look...lady" ndio iliyokuja kuwa "LUKULEDI". Sasa leo nimejiuliza kuhusu huu ufukwe maarufu wa "OSTABEI" uliopo Dar. Asili ya jina hili ni wapi?
Hawa hapa chini ndio Oysters Image from American Feast's Sustainable Food Blog
Na huu hapa chini ndio ufukwe huko Dar ambao waitwa Oysterbay. Image from Webshots
Ninalowaza ni uhusiano wa Oysters hawa na Bay hiyo.
Je! Kuna mwenye taarifa kamili ama usahihi wa kwanini ufukwe huu ulipewa jina la Oysterbay? Ninaamini wengi wa wakazi wa mji wa Dar hawaelewi asili ya jina hili na sitashangaa kama wengi hawafahamu uhusiano wa jina la hao Oyster na Bay hiyo (kama upo ulio halisi kuhusisha kupatikana kwa jina lake)
Leo nimewaza kuhusu hili na kwa kuwa taarifa ama habari nyingi kuhusu mahala, vitu na nchi yetu hazipatikani mtandaoni, nimeona niweke swali langu hapa ili nisaidiwe kuwazua.
Hivi ni Oysterbay ama Oyster Bay? Na asili yake ni nini?? Nawaza tu kwa sauti..NIWAZUE.
Kumbuka hiyo Oysterbay / Oyster Bay iko Dar Es Salaam. Mji aliouimba Ras Nas
Burudika naye hapa chini huku "ukinisakia" jibu
"Tuonane "Next Ijayo"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
kuna majina mengi ya ajabu eti kwa sababu wadhungu walishindwa kuyatamka vyema
kama vile kilimanjaro ni kilimakyaro
kuna sehemu kule moshi wachaga wanaita chekeleni kumbe ni chectrain, kiboliloni ilikuwa mdhungu akisimama pale anasema kibo aloni nk
bwagamoyo wanasema bagamoyo, mwanaumango manelumango nk nk
Post a Comment