Tuesday, April 27, 2010

Pale "KIBAYA" kinapokuwa NGUVU pekee ya kutangaza "UZURI"

Septemba 14, 2009 niliandika kuhusu suala la kile kiitwacho UBAYA na UZURI na nililonena ni kuwa Hakuna kibaya kisicho na uzuri...... Yategemea umeachia wapi kuoanisha na tukio (jikumbushe hapa) na bado naamini hivyo.
Ukweli wa mambo ni kuwa kile kiitwacho KIZURI chatokana na kutoonekana kuenenda sawa na kile kiitwacho kibaya japo si kila kizuri na kibaya vina tafsiri moja katika jamii husika.
Lakini tuachane na tofauti za kijamii.
Lolote liitwalo baya lina funzo zuri ndani mwake hata kama funzo hilo ni kutukumbusha kuwa WABAYA WANGALIPO.
Takribani majuma mawili yaliyopita nilikuwa nasikiliza kipindi cha mahojiano cha FRESH AIR kirushwacho na Redio ya Taifa ya Jamii (NPR) kinachoongozwa na Terry Gross ambaye amekuwa akifanya mahojiano mbalimbali katika kipindi hicho tangu 1987. Katika kipindi hicho ambacho siku hiyo Terry hakuwepo, yalifanyika mahojiano na Frank Meeink (aonekanaye kwenye jalada la kitabu chake) ambaye akiwa na miaka 13 alianza kujitmbua kama SKINHEAD; kundi la watu wawachukiao watu weusi na wayahudi na (wale wawajumuishao kama) watu wa rangi. Alipofikisha miaka 18, akawa "sauti ya kundi hilo" huku akizunguka nchini akitafuta wanachama wapya wa kundi hilo na pia kuendesha kipindi cha Televisheni huko jimbo la Illinois kwa dhamira hiyo hiyo. Baadae alikamatwa na kufungwa kwa kosa la kuteka na kumpiga saana mwanachama wa kundi jingine la Skinhead.
Kwa mujibu wa tovuti yake, "While in prison he befriended men he used to think he hated, men of different races. After being released from prison, Meeink tried to rejoin his old SkinHead pals but couldn't bring himself to hate those whom he now knew to be his friends." (Anzia Dk 19:10 - 24:42)

AUDIO HII NI MALI YA NPR NA IMECHUKULIWA HAPA
Ukisikiliza kwa makini utagundua kuwa Frank aliamini kuwa alikuwa na marafiki waliokuwa wanawaza mamoja. Na aliamini kuwa watu wa rangi nyingine hawakuwa watu na hakukuwa na namna wala haja ya kuwajali. Ni baada ya kufungwa jela na kukutana na huyo kijana mweusi (wa asili ya Afrika) ambaye alionekana kumjali na kuwaza naye kuliko walivyokuwa wale alioamini kuwa wanamuunga mkono. Na baada ya kutoka jela, alijaribu kurejea kwao na akagundua kuwa UBAGUZI hauna mwisho na hata ndani mwao wakaendelea kubaguana kuhusu "uzungu" wao jambo lililomfanya aichukie "jumuiya" aliyoamini ina umoja.
Ni kwa KUFUNGWA JELA kulikomfanya awape nafasi ya pili ya kuwafikiria watu alioamini kuwa HATOWAPENDA MAISHANI na hata alipotoka na kukorofishana na "wabaguzi" wenzake alimpa nafasi mwajiri wa kiyahudi ambaye naye alibadili mtazamo wake kuhusu wayahudi (anzia Dk ya 24:56-27:10)
Leo hii, FRANK MEEINK anajishughulisha na harakati za kueleza ukweli juu ya UMOJA WETU bila kujali rangi za mwili (jambo ambalo alijifunza kwa mara ya kwanza akiwa jela) na baada ya kuona mwanawe akibaguliwa na wanachama wenzake (anzia dk 20:00-24:49).
Tovuti yake imesema "Frank's life stands for tolerance, diversity and mutual understanding in racial, political and all aspects of society. Frank is truly an inspiration in any time of strife and conflict."
Na ni kwa kutumia NGUVU YA UBAYA WAKE WA AWALI, SASA HIVI ANAONEKANA KUWA NA USHAWISHI MKUBWA wa kuwawezesha vijana wengi wenye mtazamo wa kibaguzi kuwa na TABIA NZURI za kuthamini watu wa rangi zote.
Ni hapa unapoona namna ambavyo kile kiitwacho UBAYA kinavyoweza kuwa NGUVU PEKEE ya kusambaza wema.
BLESSINGS.

Labda tujikumbushe aliyoimba MFALME Lucky Dube aliposema Different Colour, One People


JICHO LA NDANI ni kipengele kinachozungumzia mambo mepesi na yaliyo ndani mwetu, ambayo yakiangaliwa vema na kwa tafsiri ama tafakari njema yanaweza ama ndio suluhisho kwa matatizo yetu. Kwa matoleo yaliyopita katika kipengele hiki, BOFYA HAPA

5 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

safi sana, daras zuri

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana mkuu kwa darasa zuri sana

Mzee wa Changamoto said...

Darasa hili lilianzia kwenu Kaka zangu. Mlitangulia kuonesha njia ILIYO SAHIHI nami nikafuata. Ni kwa maoni yenu tunazidi kuwa bora na kwa kukosoa kwenu tunajitahidi kutorejea makosa. Ni kwa kuwasoma tunaerevuka na kushirikiana tunaweza kuwa msaada.
Kwa pamoja tunaweza kuifaa jamii na nawashukuru ninyi kwa kuwa sehemu ya suluhisho gumu kwa jamii yetu.
Blessings

Albert Kissima said...

Niongezee kidogo kama sio kujazia kile ulichoanza kukiongelea.
Uzuri na ubaya havitokei kwa wakati mmoja kwa mtu yule yule bali utaanza ubaya halafu uzuri utafuata na kinyume chake. Ubaya ili uwe na uzuri, hauna budi kuwa na kikomo. La si hivyo ubaya utaendelea kuwa mbaya pasi na kuwa na uzuri.

Pengine ubaya wa mtu fulani wauonao wengine ndio uzuri kwa mtu huyo aonekanaye mbaya, mtu huyu hugundua kuwa matendo yake yalikuwa mabaya baada ya kusimama upande wa uzuri na kutazama upande mwingine na kuweza kuyaona mabaya yake.
Ni mtazamo yangu.

Tmark said...

Safi sana na Leo nilikuwa nikiangalia movie ya kibaguzi duuuh.
Hakika hili ni darasa kubwa broda