Friday, April 16, 2010

Them, I & Them....SOTE NI NDUGU...Innocent Galinoma

Picha na muziki kwa hisani ya INNO
"We share the same BIOLOGY regardless of our ideology. What we really wanna see is LOVE AND UNITY" Luciano
Ndivyo anavyonukuliwa Luciano katika wimbo wake MANKIND ambao amehimiza kutambua undani wa mtu ambao HAUTOFAUTIANI baina ya binadamu. Hili lina umuhimu saana kulitambua kwani ni SULUHISHO kwa matatizo mengi "ya hiari" tuyaonayo sasa. Kutambua kuwa SOTE NI SAWA kutatufanya tujiulize maswali mengi juu ya dhamira ya KUMTESA AMA KUMNYANYASA mwenzako.
Kama binAdam wangetambua kuwa tu wamoja, tu sawa, tu ndugu, basi tutafikiria MAUMIVU wanayopata wenzetu na kuacha kufanya hivyo kwani tutahisi twafanyiwa sisi.
Na kwa Tanzania huu ni mwaka wa uchaguzi. Mwaka ambao tunastahili kuweka maslahi ya nchi na wananchi mbele katika kuwachagua wale ambao watatuwakilisha kueleza matatizo na mahitaji halisi ya mwananchi ambaye hawezi kuonana na wenye mamlaka ama uwezo wa kutoa suluhisho. Hili si jambo dogo na si jambo rahisi pia. Tuna watu ambao (kwa mtazamo wao wa nje) wanaamini kuwa tofauti na wenzgine. Watu ambao wanaweza kujitofautisha na wenzao kwa vitu vya nje kama DINI, RANGI, UMRI, KABILA, MUONEKANO na mengine mengi yasiyotutofautisha ki-uhalisia.
Sisi soote ni waTanzania. Sisi sote tuna mengi makubwa ambayo yanatuunganisha na pia ni muhimu zaidi kuona tunavyounganishwa kuliko tunavyojiaminisha kuwa tunatenganishwa.
Ni hapa ninapojikuta nagota katika wimbo wa Kaka Innocent Galinoma Mfalingundi ambao aliuimba miaka kadhaa iliyopita. Humo amehimiza huu umoja tunaostahili kuutambua kuwa SOTE NI NDUGU.
Amefunza kilichotokea tangu "enzi za mababu" ambako ameendelea kusema "watu tuliishi pamoja kama ndugu. Leo mambo yamegeuka hujui wa kumwamini. Rafiki yako mkubwa aweza kuwa adui, adui yako mkubwa aweza kuwa rafiki"
Ameeleza namna ambavyo UKOLONI umetuaminisha kuwa sisi si watu wamoja. Umetugawa (ili kututawala) na makombo ya akili hizo yakingali yanatutafuna leo hii kwa watu kuuana kwa tofauti ndogondogo.
Lakini haishii kutueleza hali ilivyokuwa na ilivyo sasa, bali anaendelea kutuhimiza kuwa "sisi sote ni ndugu, watoto wa Baba mmoja". Anazungumzia namna ambavyo dini, rangi, na vingine vingi vioneshavyo muonekano wa nje visivyo na nafasi katika maisha yetu.
Waweza kumtembelea Inno na bendi yake katika tovuti yao HAPA (ukifika huko usisite kusikiliza wimbo wa United States of Africa ulioimbwa mwanzoni mwa miaka ya 90 lakini watufaa leo kuliko wakati mwingine wowote).
Msikilize Innocent Galinoma katika kibao chake SOTE NI NDUGU.

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka naupenda sana huu wimbo. Ni kibao kilichonivuta hata nikawa addicted wa reggae. Nakumbuka nikiwa form two' nilikiimba chote kwenye tamasha la shule bila kutumia mento (instrumental)
Huyu jamaa ana akili sana katika tungo zake.
Ile album yake ya Greetings From frica hata leo ukiisikiliza waweza dhani imetungwa jana. Nyimbo zote ni kali balaa.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

laiti kama tungeelewa kwa moyo ukweli huu, mambo yangekuwa si kama yalivo sasa :-(

EDNA said...

Napenda sana kazi za Galinoma.

Yasinta Ngonyani said...

Mwenzenu nimecheza ijumaa yote huu wimbo mpaka nikasahau kuweka maoni yaani we acha tu. Yaani raha kweli maisha na mziki. Ahsante Mube...