Amani, Heshima na Upendo kwenu waungwana nyote.
Kwanza niwaombe radhi kwa kushindwa kuonekana hapa tangu Alhamis. Ni pilika za maisha tuuuu ambazi zilinisonga kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na sasa Jumapili nimepata ahueni. Kwa maana hiyo vipengele vya Them' I & Them na Waliwaza nini havikuweza kuwepo wiki hii. Lakini kuna sababu.
Nilikuwa nashughulikia pilika kadhaa zilizonipeleka mpaka kwenye MAKUMBUSHO MBALIMBALI hapa DC Metro.
Makumbusho hayo yalinifanya nishangae namna ambavyo wenzetu hawa wamekuwa makini kwenye kutunza vile vya kale ambavyo si tu sehemu kubwa ya utalii, bali pia kuwawezesha wajao (watoto na vizazi vijavyo) kujua na kuheshimu walikotoka na hata kuthamini mchango mzima wa waliowafikisha hapo kwa kuangalia walikopitia na walivyopitia mpaka kusika hapo walipo.
Kwetu (Tanzania) ni tofauti saana. Niliwahi kuandika PALE SERIKALI INAPOCHOCHEA UJINGA (hapa) na nazidi kuamini katika hilo kwa kuangalia juhudi za serikali za wenzetu kutunza asili yao ilhali sisi twaikimbia yetu kuwaiga wao (na hatuna dalili ya kufika kwenye u-wao licha ya kuwa tumeshaupoteza u-sisi)
Na wacha niungane nanyi katika taswira hizi za vituo cha makumbusho ya Taifa ya mambo ya anga vya Steven F. Udvar-Hazy na The National Air and Space Museum on the National Mall
Concorde; Max Speed 2.04 Mach 2179 km/h Boeing B-29; "the primary aircraft in the American firebombing campaign against the Empire of Japan in the final months of World War II, and carried the atomic bombs that destroyed Hiroshima and Nagasaki." Lockheed SR-71 Blackbird; "THE FASTEST AIR BREATHING, MANNED JET PLANES IN THE WORLD"
Boeing 707; "served 18 years as a flying test laboratory before it was turned over to the Smithsonian Air and Space Museum in May 1972."
Soma maelezo yake juu.
The Space Shuttle Enterprise (NASA Orbiter Vehicle Designation: OV-101); The first Space Shuttle orbiter. Soma mwenyewe hilo "dubwana" ni nini. Niliposoma maelezo yake nikashituka..
6 comments:
Mie najibu LEBO.... halikosi ukoko.
Duh, nimejionea japo nipo mbali.
Kaka nilianza kupatwa hofu na ukimya wako. Tunashukuru kwa kumbukumbu hii yenye kufundisha.
Kaka wakati huko Amerika watu wanafanya juhudi kuhifadhi mambo ya kale, hapa nyumbani kuna tangazo jipya la kampuni ya simu linalosema, "...achana na mambo ya kale!"
Sijui sasa....!
Hahahaha Kaka Chib.. Naona umeishitukia "Label" ya leo. Thanx Man
Kaka Fadhy hiyo kawaida. Rejea http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/10/serikali-inapochochea-ujinga.html
Ok either I am dumb or I am missing something here...what about the last picture? na kaka chib ndio kanipoteza kabisa!...lol...maybe it is the aviation language which I don't understand...by the way Changamoto CEO mchoyo...picha umetokea mbaaaaliiiii, then only picha ya mwisho ndio umeruhusu ku"click" on it so we can zoom ila nyingine full uchoyo...hahahaha nice to see you back bro! hihihi
Da Mdogo Candy1.
Unajua hatujawasiliana kwa muda na sina hakika kama bado ni "sober-gal" kama awali. Na hivi ni week end, basi "chichemi"
Kaka Chib amejibu JINA LA LABEL ambayo ni JUNGU KUU na yeye kasema "HALIKOSI UKOKO". Got it?
Kwa hilo la picha ya mwisho, kinachoonekana kwenye picha ya pili toka mwisho ndicho chenye maelezo kwenye picha ya mwisho. Kwa maana hiyo, hilo "dubwana" lililosimama kwenye picha ya pili toka mwisho ni WORLD'S FIRST BALLISTIC MISSILE. Kuna mambo mengi yaliyo HALISI kule mfano jiwe halisi toka mwezini na mambo mengine mengi ambayo kwa bahati mbaya mimi kama "mtembezi na mpiga picha" sikuwemo kwenye picha hizo. Lakini "next ijayo" ntarejesha taswira nyingi zaidi.
Much Luv Sissy na shukrani kwa kunikaribisha kurejea. Nawe karibu "maonini" (si unajua imekuwa karibu mwezi tangu uache maoni kokote? Loool)
エロセレブとの出会いを完全無料でご提供します。逆援助で高額報酬をゲットしよう
Post a Comment