Tuesday, May 18, 2010

HATIMAYE NIMEREJEA........Nilikokuwa

Hatimaye nimerejea wanandugu. Nilikuwa nimebanwa na mambo kadhaa na pia JUMAMOSI nilikwenda kushuhudia maonesho ya wazi ya ndege za kivita. Ilikuwa saafi sana japo ilikuwa ngumu sana kwa mimi kupiga picha na kurekodi video.
Lakini kwa sasa FURAHIA TASWIRA HIZI HAPA CHINI
Ndimi mimi ndani ya cockpit ya C-17. Yaani ile phobia aliyoizungumkia Kaka Mtondo HAPA na HAPA ndiyo ilikuwa kinikwaza. Ndege imetulia wala haijawashwa lakini bado ni mtetemeko
Mzee huyu alikuwa rubani wa vita ya pili ya dunia. Ana story huyooooooooooo.
Watu woote "macho juu"
Kisha ikaja "main event" ya Blue angel.
Hii "ndude" ni hatari. Inapiga "rivasi" hewani na kusonga kipembeni pembeni. Inatua na kuondoka wimawima. Iangalie hapa chini.

Hii JETCAR hapo juu nayo ilinogesha maonesho. Inakimbizana na ndege.
Ona ilivyokuwa imeachwa hapa
Halafu ilivyo-catch up hapa. Kumbuka gari ilianza 0mph wakati ndege ilishakuwa kwenye mwendokasi
Hii ilikuwa timu ya GEICO. Nayo ilinogesha
Na hii ndio C-17. Ndege yenye uwezo wa ku-taxi kinyume nyume na kuruka kwenye runway fupi saana. Angalia mwanzo mwanzo wa video hapa chini

15 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kwenye picha ya kwanza nimemwona kepteni Mubelwa Bandio. Ha ha haaaaaa!

Kaka picha hizi kwa mtu anayependa historia, anapata msisimko wa aina yake. Nimeinjoi kana kwamba nami nilikuwepo huko. Ahsante sana kwa taswira hizi.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kila binadamu na upendo wake, madege ya kivita tena!

Koero Mkundi said...

Najiulza kwanini ziwe ni ndege za kivita na zisiwe ni za kubeba abiria?

Hayo maandalizi na mbwembwe zote ni za nini?......

Kaka hayo mambo sio ya kushabikia, mie nikiona mwili wote unanisisimka.....

Egidio Ndabagoye said...

Umenikumbusha vita ya Kagera.Waziba wa Kanyigo walikuwa wanasema wanajeshi wametupiga,wakatuibia na magari yetu 6.
Ilikuwa inashangaza kweli mtu anaesema kaibiwa magari sita huwezi kuamini kwa kuangalia anapolala(nyumba ya nyasi).

Kumbe magari ni baiskeli.

Unknown said...

Hapo kweli mzee nilikosa uhondo. Wafahamu niliitwa kazini ndiyo maana sikutokea. Mwaka ujao lazima nami nitie timu. Kazi nzuri, kweli umewakilisha!! Ahsante bro!

Godwin Habib Meghji said...

Nilipanga kuhudhuria mwaka huu, ila ratiba ikagongana na maafali ya rafiki yangu. Nilikosa mwaka jana na mwaka huu pia. Nitajitahidi mwakani nihudhurie kabla sijahama hii state au kuamua kurudi nyumbani. SHUKRANI KWA TASWIRA

Mija Shija Sayi said...

Ndege kurudi kinyumenyume angani! Hii sijawahi kuona na bahati mbaya sikuwahi hata kufikiria hivyo. Dah!

Safi sana kaka.

Faith S Hilary said...

Personally, it is exciting to see on the pictures and the video you posted ila I am the wrong person to take with on that show. I am absolutely TERRIFIED of these things, one of my greatest fears...long story but that's the thing...this is what watching too much "World's Most Amazing Videos" can do to you! I am just scared it will crash or something etc etc but I am just scared...though it it a great day out and something "out of the ordinary"...na hiyo inayokwenda kinyume nyume, I can't imagine the amount of fuel it loses just by doing that! See the smoke coming out of it? Wow!...I am just saying

Subi Nukta said...

Asante kwa elimu hii Mubelwa.
Hivi, umesoma ile habari ya rubani aliyeongoza ndege kwa miaka 13 bila ya kuwa na 'cheti rasmi'? tehe, nadhani kila fani inaowaendesha fani bila 'cheti rasmi' wengine wanapatia kuliko hata walio na 'vyeti rasmi', naam, pia wapo wanaoboronga.

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Fadhy. Ni kweli kuwa kuna meengi wanayokueleza hao waheshimiwa unapokuwa pale. Ni historia nzuri tuuu.

@Kaka Kamala. Nakubaliana na wewe kabisa kuwa "kila binadamu na upendo wake". Binafsi ni kwa ndege zote japo juzi walionesha za kivita tuu

@Da Koero. Nadhani nimejibu hapo juu kuwa ndege (zikiwa zimetua na kuzimwa) mimi ni rafiki wazo hata kama si za kivita. Maandalizi na mbwembwe ni kuwaonesha wananchi historia yao na pia vitu vipya ambavyo hata wasipooneshwa vitanunuliwa kwa harama zao. Wala sishabikii, bali ninashangazwa.

@Kaka Egidiyo. Hahahahaaaaaaa. Umenikumbusha maswali ya "utaenda mjini kwa gari ama motokaa?" Ni kweli kuwa baiskeli imekuwa ikitambulishwa kama gari kwa hiyo usije shangaa mtu akikwamb ia ana magari manne na Land Rover moja. KARIBU TENA KAKA

@Kaka Mrope. Kweeeeli uli-miss. Lakini wakati mwingi twalazimika "kufanya kitu cha kwanza kwanza" (first thing first) na kazi ilitakiwa ije mbele ya hizi ndubwana. Tuombe Mungu mengine yasitupite.

@Kaka Godwin. Nakumbuka tulivyolonga ukasema una sherehe ya rafiki. Nikatambua hapo "priority" itakuwa kule maana baada ya "msoto" wa haja kuisaka elimu, unapomaliza wahitaji kila aliye karibu naye. Tuombe mwakani Kaka.

@Da Mija ukweli wako ni sawa na wangu. Nilipoenda kazini jana nikwaulia kwanini tunatengeneza parts za JSF (Joint Strike Fighter) tena kiungo cha gharama saana kuisaidia kuondoka Vertically ilhali kuna hii? Wakasema hii ya sasa iko "efficient" zaidi (itakuwa ni version mpya ya hii hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/06/ubaya-hivi-una-faida.html)
Lakini nami sikuwaza kuwa yaweza fanya ilivyofanya. Hasa ile "shot-kulia" na rivasi yake. Duh

@Da Candy. Waogopa kufa? Ama unaogopa kujiona unakufa? Hahahahaaaaaaa. Ni sehemu ya maisha kuogopa. Kuhusu mafuta inatumia mafuta sana, lakini kile ulichoona kinatoka chini ni maji by the way. Mtaalamu alisema inapofanya vile (kuganda, kurudi nyuma na kuselebuka kiupande upande) inatumia karibu thrust zake zote na hili huzifanya injini kuwa na joto saana. Hapo ndipo wanapolazimika ku-pump maji kwenda kupoza na kisha yatoke. Kwa hiyo licha ya kulamba wese, yale yalikuwa maji. UKISIKILIZA KWA MAKINI UTAMSIKIA AKIELEZA KWENYE VIDEO

@Da Subi. Naenda isoma sasa hivi. Hayo ndiyo mambo yanayonifanya niwe na Phobia ya haya madubwashika. Yaani rubani akichemka ama kama hajafuzu kidogo ni balaa.
Duh.
Ati ume-attach-ije hiyo link humu? Naiba ujuzi (kama kawaida)
Love you all

Bennet said...

Hapa nipo cafe, jamaa wamehama pc zao wamehamia kwangu. nawaambia chukueni adress muangalie wenyewe wao wanang'ang'ania hapa

Simon Kitururu said...

Hapo naona mambo yalikuwa dukinaa!

Albert Kissima said...

Ama kweli ilikuwa ni rubudani ya aina yake. Nayapenda kweli madege na natamani siku moja nisafiri nalo (nitajitahidi hata kama ni safari ya kutoka Kilimanjaro hadi Dar au Mwanza. Hahahahaaaa). Kikubwa zaidi, wakati naangalia hizi taswira, jinsi midege ilivyo hewani, da! Nawapa heshima sana binadamu aliyegundua technologia hii na wote waiendelezao. Hakika ujumbe huu "enendeni ulimwenguni..... .......na MKAIJAZE DUNIA" unatenda kazi yake na unaonekana.

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli inafurahisha ila ni kweli kila mtu una pendo la pekee kwa anachokifanya. Safi sana kakangu na ahsante sana kwa taswira hizi!!

Alex Mwalyoyo said...

Tuko pamoja Mkubwa!
Picha safisana hizo.