Tuesday, May 25, 2010

Ili uokoaji usiwe uuaji katika ajali.....

NIMEKUWA MHANGA WA AJALI NA NIMESHUHUDIA TOKA TUKIONI NAMNA AMBAVYO UOKOAJI WA MAISHA YA MAJERUHI UNAVYOTENDEKA.
Lakini nilipokutana na makala hii ya
Dr Faustine nikaona ni vema kushirikiana nanyi kuweza kupata uelimishaji zaidi.
ENDELEA NA KILE ALICHOSEMA
DR FAUSTINE
Picha toka Maktaba ya Changamoto yetu
....... Ni muhimu sana kukumbuka kinachookoa maisha ya majeruhi si uharaka wa kukimbizwa hospitali bali ni aina ya huduma aliyopata eneo la ajali.
Mara nyingi fikra zetu ni kukimbiza majeruhi hospitali badala ya kutoa huduma ya kwanza pale pale alipo.
Pia uhamishaji/ubebaji wa majeruhi kama ilivyo kwenye picha hizi unaweza kuleta madhara zaidi kuliko kusaidia. Mifupa inaweza kuvunjika, kama mtu alipata madhara ya uti wa mgongo, mtikisiko unaweza kumfanya mtu huyu akapooza kabisa na pia ubebaji usio makini waweza kusababisha kifo.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika eneo la ajali kama yafuatayo:

1: Kuhakikisha kuwa mazingira yanaruhusu kuokoa majeruhi. Hakikisha kuwa hakuna mafuta yanayovuja kwenye gari au hatari ya moto kulipuka.
2: Fanya uhakiki wa haraka wa walio hai na wenye kuihitaji msaada. Marehemu haitaji kuokolewa.
3: Kama majeruhi hajabanwa, jaribu sana kumsaidia pale pale alipo bila kumsogeza.
4: Kama majeruhi atahitaji kusogezwa uangalifu mkubwa utumike na kuhahakisha zile sehemu za maumivu zinalindwa vyema.
5: Hakikisha njia ya kupitisha hewa ya majeruhi iko wazi na hakuna kitu kinachoziba.
6: Hakikisha majeruhi anapumua. Kama majeruhi anapata shida kupumua inabidi asaidiwe kufanya hivyo.
7: Hakikisha majeruhi ana mzunguko mzuri wa damu na havuji damu kwa wingi. Kama majeruhi anavuja damu kwa wingi, ni muhimu kujaribu kuzuia uvujaji wa damu. Mara nyingi waweza kutumia sehemu ya vazi la majeruhi au la mwokoaji kufunga sehemu ya juu ya sehemu inayotoka damu kwa wingi au kugandamiza sehemu hiyo kama haijaathirika kwa ajali.
8: Hakikisha sehemu zilizovunjika zinakuwa "stabilised" ilikupunguza maumivu na kupunguza athari zaidi.


** Kwa kumalizia unapotaka kumsaidia majeruhi kumbuka: A: Airway; B: Breathing; C: Circulation.

Baada ya hapo ndio unaweza kufikiria kumpeleka majeruhi hospitali.

Pendekezo:
Kutokana na wingi wa ajali nchini, ni vyema vyombo vya habari vikasaidia kuelimisha jamii kuhusu hatua hizi muhimu zinazotakiwa kuchukuliwa kuwanusuru majeruhi pindi ajali inapotokea.
Majeruhi wengi wanapata madhara zaidi au kufa kutokana na uokoaji usio makini.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ningependa au furahi kama watu wote wangesoma hapa na kupata elimu hii maana ni mambo MUHIMU SANA sijui hii elimu itawafikiaje watu wengine...nawaza kwa sauti. UPENDO DAIMA.

Anonymous said...

mimi nauliza hivi kaka yangu ulimpata yule dada aliyekusaidiaga ktk hii ajali kama sikosei kunakipindi ulikuwa unamtafuta dada mmoja jina sikumbuki aliyekusaidia ktkt hiyo ajali sijui ni wewe au nakosea tafadhili kama umeshampatatafadhali tujulishe

Mzee wa Changamoto said...

Ndugu yangu Anon.
Kwanza naomba kusema kuwa NASHUKURU SAAANA kwa kuendelea kufuatilia maoni na mahitaji binafsi.
SINA NINALOWEZA KUSEMA KUSHUKURU KWA HILI.
Kwa hakika sijaweza kumpata Renatha Benedicto. Ni mimi niliyekuwa na bado namsaka dada huyo.
Kuna MSAMARIA MMOJA (baraka kwake) ambaye aliniachia maelekezo ya kwenda kumsaka KAWE kanisani lakini niliyemuomba kunisaida hilo hajaweza kumpata.
Hata hivyo alizungumzia wasiwasi kuhusu KANISA lisemwalo hapa. Hakujua kama ni Walutheri, WaKatoliki ama ni wapi?
Lakini bado namsaka na kama unaweza kuwa na tetesi ama kuwa na ushauri wa namna ninavyoweza kumpata. Ntashukuru saaaaaana ukiwasiliana nami hapa ama kwa email yangu binafsi ambayo ni changamoto@gmail.com
NDUGU YANGU. Nashukuru saana kwa ujalifu wako na ni FARAJA KWANGU
BARAKA KWAKO

Anonymous said...

kaka yangu sijamsikia ilanitajaribu kukuuliziaulizia nikimpata nitakujulisha usichoke kumtafuta iko siku ambaye haina jina mungu atakuwezesha utampata km bado atakuweko napia usiachekusali mungu anaweza kukuonyesha mahali utakayo mpatia pole sana na maswahiba yaliyokupata yote ni majaribu yanayotupata ss wanadamu inabidi tumshukuru mungu kwakila jambo kwani yeye ndiye muweza ya yote ubarikiwe sana