Friday, May 28, 2010

Them, I & Them.....SAVE THE WORLD......Luciano

Amani heshima na upendo kwa waungwana nyote.
Nimekuwa nikiwaza namna ambavyo jamii yangu imefika hapa ilipo ambapo kila juhudi za kuisaidia kuondokana na matatizo kama ya rushwa, ufisadi (sina hakika kama kuna tofauti).
Lakini nawaza hizi harakati za kuibadili jamii kama zitawezekana iwapo tunajitahidi kusaka suluhisho la matatizo bila kujua ama niseme kwa kulikimbia suluhisho hilo. Ni lini TUTATAMBUA KUWA NJIA KUU YA KUIBADILI JAMII NI KUWABADILI NA KUWAFUNZA WATOTO /VIJANA?
Ati watoto wanaenzi rushwa na ufisadi na twaamini tunaweza kuja kuwa na kizazi kisichohusudu rushwa?
Leo sitasema sana, bali turejee kwenye MAFUNZO ya LUCIANO katika wimbo huu SAVE THE WORLD upatikanao katika albamu yake ya A New Day ambaye anasema "if you wanna save the world, you gotta save the children. Set an example for the children to follow, make a brighter tomorrow"

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kaazi kweli kweli!! Hakika kazi tuyayo na tena kubwa tu kwani watoto/vijana ni viumbe wazuri sha kwa kuiga. Ijumaa njema nawe pia familia yako!!