Saturday, May 8, 2010

Wakati nawaza wawazayo "wapakwa mafuta"

Hivi hawa "wapakwa mafuta" wanawaza(ga) nini?
"Tired of leaving church feeling like I've just been robbed
2 hours of rambling not much mention of God"
Hii ni nukuu ya wimbo wake Tanya Stephens uitwao WHAT A DAY (urejee kwa undani hapa) ambayo inaendelea kuwa na ukweli katika makanisa yetu ya "kileo"
Binafsi mimi ni muumini. Tena muumini mzuri wa kiKristo ambapo huwa najivunia yale nijifunzayo kanisani mwetu. Na (labda kwa kuwa ni dhehebu), bado kuna muelekeo wa meengi nifunzwayo toka Tanzania mpaka hapa U.S.A. Lakini kama nilivyowahi kusema, linapokuja suala la IMANI, kunakuwa na "upenyo" mkubwa saana wa kila mtu kuhubiri kile aaminicho na wakati mwingine kwa "mtindo" aaminio ndio wafaa kuwakilisha na kuwasilisha mahubiri yao.
Ni haya yanayonifanya kuwaza kama sote twamuamini Mungu mmoja na hata kama wakristo wote wanapelekwa sehemu moja kwa kutumia mahubiri tofauti na hata njia tofauti za kuwafanya wafike mbinguni.
Na "wakati nawaza wawazayo wapakwa mafuta hawa", huwa naishia kujiuliza WALIWAZA / WANAWAZA NINI kuhubiri hivi ama kwa mitindo hii?
Watazame wachache hapa chini kisha uwaze nami
Tuanze na "Nabii" Tito ambaye yeye anahimiza ndoa za mitara na unywaji pombe.


Turejee hapa Marekani tukutane na Rev. Fred Phelps


Yawezekana huyu ana yake ya kumfanya aseme kivyake na kuwakusanya aaminio ni wake. Lakini sasa tuangalie upande mwingine wa huyu "anayekusanya kondoo" wagomvi kwa namna ya kipekee. Angalia chini aina nyingine ya "UTUMISHI" kisha jiunge nami kufikiria "alipokuwa anafikiria kuanzisha hili, ALIWAZA NINI?"


Labda tuwaangalie hawa walioamua "kuwafikia wengine" kwa style ya kipekee kwa namna hii. Hebu tuanze na Pastor Willie Ramos ambaye najitahidi kuwaza anapoandaa "somo" ama Ibada ya siku ANAWAZA NINI?


Ama huyu anayeonekana "kuwakuna" zaidi waumini wake kwa mtindo wake wa kuwafikishia neno la mungu. Ukiweza anzia dk 1:06 na umalizapo jiunge nami kuwaza "ALIWAZA NINI" kuanza mahubiri kwa mtindo huu?


Na vipi kuhusu huyu mhubiri anayehubiri kuhusu ushoga na usagaji?

Najua yako mengi ya kujiuliza kuhusu namna ambavyo hawa waliopewa dhamana ya kulichunga kundi la waumini wanafanya maamuzi yao. Na si kwa yale waongeayo na namna waongeavyo, bali hata kwa namna waruhusuvyo mambo mengine kutendeka chini ya himaya ama maamuzi yao. Labda jaribu kufikiri huyu aliyemruhusu huyu "mwimbaji" kuingia madhabahuni na kuimba aliwaza nini? Labda ilikuwa ni ibada ya "watu maalum", ama ni yeye "aliyejitengeneza" ili kuondoa aibu. Lakini katika hali ya kawaida, unaweza kuwaza kama alikuwa sawia na kama waliomkaribisha waliwaza sawasawa.
Sikiliza uimbaji huu hapa chini


***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

6 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ni mawazo harafu wanamtaja nani sijui

Mija Shija Sayi said...

Siku za mwisho. Na Maandiko ni lazima yatimie.

Yasinta Ngonyani said...

Haki ya Mungu naungana na Da mija hizi ni siku za mwisho. sijui waliwaza nini???

Christian Bwaya said...

Wahubiri wamekuwa motivational speakers wakitumia vichwa vyao wenyewe. Wanayoongea unaweza kuyasikia kokote ila tafauti yao ni eneo la mhadhara husika. Kwamba wanaitwa "wahubiri" kwa sababu tu wanazungumza kanisani.

Faith S Hilary said...

Yaani hizo video zote za mwanzo zimenishangaza kwa kweli yaani I wish you could see my facial expression na kweli "waliwaza nini" lakini nikawa sawa baada ya kumuona rafiki yangu wa Amazing Grace! I just can't stop laughing! looooooool! I need to hire him on a party or something, he will be perfect!

Anonymous said...

Mzee, macho mbona mekundu? Ulikuwa umetoka kujitwika lubisi nini? Pole