Thursday, July 29, 2010

"HAKUNA KAZI BORA KAMA UZAZI NA MALEZI"

Maneno haya yalisemwa naye Dr Ben Carson alipokuwa akimzungumzia mamake.
Tarehe 5 Aprili mwaka jana niliandika makala yenye kichwa cha habari Ni mbegu ndogo iletayo mazao makubwa (irejee hapa)
Na habari hiyo iliyomhusu Daktari bingwa wa upasuaji ulimwenguni Dr Benjamin Carson. Katika makala hiyo, nilieleza kile nilichosikia na kusoma katika toleo la kipengele cha THIS I BELIEVE kipindi cha Morning Edition kirushwacho na Radio ya jamii hapa Marekani ya NPR. Unaweza kusikiliza alichokisema katika kipindi hicho kwa ku-bofya hapa.
Lakini bado nilikuwa miezi kadhaa kabla nami sijawa mhanga wa kazi ama shughuli hii nzuri ya ulezi.
Licha ya kuwa mlelewa na kuona njia njema za malezi toka kwa wazazi na walezi wangu, haikuwa sawasawa mpaka nami nilipoingia jukumu lisilo la hiari la ulezi. Na hapo ndipo nilipoona uzuri, ugumu na ama umuhimu wa malezi bora kwa yule umleaye.
Nakumbuka katika Salaam zangu za siku ya kinamama duniani (hapa) niligusia umuhimu wa kinamama. Nimelikumbuka hili hivi majuzi wakati nawasiliana na Kakangu Kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa kumpongeza kwa kupata mwana. Na kisha nikapitia kwenye kijiwe chake kusoma toleo la ujio wa mwanawe huyo na moja kati ya sentensi alizoandika katika taarifa ya ujio wa mtoto ni ile aliyomalizia nayo akisema "nilianza kumheshimu mwanamke toka zamani ila hii inaongezea heshima kwa mwanamke" Natambua malezi si ya mwanamke pekee lakini kama Kakangu Kamala na hata mimi mwenyewe tunaweza kuongeza heshima na thamani ya wanawake kwa kile wanachotubariki nacho, ina maana tunaongeza mapenzi na msaada kwao na kujishughulisha zaidi katika malezi. Ina maana kwa kuamua kumuona mwanamke kwa namna iliyo bora zaidi, tunaongeza msaada wa malezi kwao na kuboresha malezi kwa mtoto.
Wapo waliotangulia wakasema "harder the battle, tougher the fight, sweeter the victory". Na naamini mchakato mzima wa malezi ndio UTAMU WAKE na kwa waliofanikisha suala la malezi wanaweza kuamini kuwa katika KUWEKEZA KWENYE MALEZI, TUNASAIDIA KUKUZA MWANA NA KIJANA / BINTI ALIYE MWEMA AMBAYE NDIYE ATAKAYEKUJA KUWA MSAADA KWA JAMII.
Na kwa kuwa wanajamii wote wanaanzia utotoni, basi lazima tujue kuwa UZAZI NA MALEZI ni KAZI BORA ZAIDI na ni msaada mkubwa kwa jamii ijayo.
WAKATI NAMKARIBISHA RASMI KAKA KAMALA KATIKA ULIMWENGU WA MALEZI, Naomba uungane naye kusikiliza kibao hiki mwanana cha Darius Rucker kuhusu makuzi na malezi na yanavyopita. Anaonesha ama kueleza namna ambavyo kile tunachoona ni karaha katika malezi ya sasa tutakavyokumbuka baada ya muda mfupi. Na hili ni jingine linalofanya MALEZI KUWA KAZI BORA SAANA MAISHANI

He didn't have to wake up
He'd been up all night
Layin’ there in bed listenin’
To his new born baby cry
He makes a pot of coffee
He splashes water on his face
His wife gives him a kiss and says
It gonna be OK

It won’t be like this for long
One day we'll look back laughin’
At the week we brought her home
This phase is gonna fly by
So baby just hold on
‘Cause it won't be like this for long

Four years later ‘bout 4:30
She's crawling in their bed
And when he drops her off at preschool
She's clinging to his leg
The teacher peels her off of him
He says what can I do
She says now don't you worry
This’ll only last a week or two

It won’t be like this for long
One day soon you'll drop her off
And she won’t even know you're gone
This phase is gonna fly by
If you can just hold on
It won’t be like this for long

Some day soon she'll be a teenager
And at times he'll think she hates him
Then he'll walk her down the aisle
And he'll raise her veil
But right now she's up and cryin’
And the truth is that he don't mind
As he kisses her good night
And she says her prayers

He lays down there beside her
‘Til her eyes are finally closed
And just watchin’ her it breaks his heart
Cause he already knows

It won’t be like this for long
One day soon that little girl is gonna be
All grown up and gone
Yeah, this phase is gonna fly by
So, he's tryin’ to hold on

‘Cause it won’t be like this for long

It won’t be like this for long

It won’t be like this for long

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ati ni nani kama mama?

Kuna wakati Kamala alitaja kuhusu uhusiano usioridhisha kati yake na mamake mzazi. Natumaini kwamba tukio hili litamsaidia katika kuurudisha uhusiano huo. Ile tu mtu kukaa tumboni mwa mama kwa miezi tisa na kuzaliwa ukiwa hoi na tegemezi namna hii ni sababu tosha ya kutokosana na mama. Huwa sioni sababu yo yote hapa duniani ambayo inaweza kunifanya nikosane hata kufikia kutosalimiana na mama - mtu ambaye alizunguka nami kwa miezi tisa mizima na kunitendea kila kitu katika wakati ule ambapo nilimhitaji sana!

Natumaini sijamchokoza Kamala asije akanishukia na msumeno wake wa utambuzi. Hata hivyo najua kwamba kwa sasa analala kwa mang'amung'amu na sidhani kama kwa sasa ana muda na usongo wa "kukereza" watu tena.

Samahani mwenye nyumba kama nimetoka nje ya mada!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ni kweli kwenye kulea kuna mengi ya kujifuza. napitia mengi na sasa nayaona mengi. natamani awe vile ninivyoona ni vizuri au vyema

ila kwa matondo yawezekana usiielewe ishu kati yangu na mama. sijisikii vizuri kuitundika bloguni ila ni cmplex na inanipaga majonzi pamoja na utambuzi wangu. labda juma lijalo naweza kukutumia email ndeefu ili uelewe japo naona kufanya hivyo kunaniongezea majonzi kwani utaishia kunihurumia na kunipa pole zitakazo nisikitisha zaidi kwa kuonewa huruma