Thursday, July 15, 2010

Maalum kwa WAGOMBEA WETU 2010

"Jamaica is a paradise, but for those who were born and raised there is a struggle" Haya ni maneno yalitosemwa / yanayosemwa naye Peter Morgan wa kundi la Morgan Heritage kuhusu vile ambavyo JAMAICA huonekana machoni ama kusikika masikioni mwa watalii ukilinganisha na hali halisi ya maisha ya wazawa wa nchi hiyo. HILI HALINA TOFAUTI NA NCHI YANGU TANZANIA.
Kwa kumbukumbu tuu, ni kuwa huu ni MWAKA WA UCHAGUZI. Mwaka tuonao TABASAMU toka kwa wanasiasa kuliko wakati mwingine wowote ule. Wakati ambao hata mtoto ambaye hajabahatika kuoga kwa siku kadhaa, anapata "kumbatio na busu" toka kwa wagombea. Wakati ambao wagombea hawachoki kupunga mikono na kusalimia watu.
Kwa ufupi, ni WAKATI AMBAO WANASIASA WANAKUWA WANAFIKI KULIKO WAKATI MWINGINE WOWOTE ili kuweza kujipatia kura watakazo.
Lakini kabla hawajaingia kwenye "viwanja" na kuanza KUDANGANYA, napenda kuwakumbusha yale yaendeleayo ndani ya majimbo na nchi yao.
Yaani nawaomba watazame kile kilichopo "ndani" ya majimbo yao. Na hizi zifuatazo ni baadhi ya taswira nilizozikusanya toka katika blogu na tovuti mbalimbali ambazo zaonesha hali inayohitaji kutendewa kazi ama kuboreshwa.
TUANZE NA SEKTA YA AFYA
KISHA SEKTA YA ELIMU Hapa chini ni maliwato ya shule hukoooo Lindi. Hii shule imekuwa na maliwato ya hivi kwa miaka 35
Hili hapa chini ni jengo la bweni katika shule ya sekondari huko Tanga TUHAMIE SEKTA YA MIUNDOMBINU:
LABDA TUCHUNGULIE KWENYE UWEKEZAJI
NB: Picha zote ni mali ya blog na tovuti mbalimbali. Si mali ya Blog ya Changamotoyetu Blog

Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli inasikitisha na inaumiza sana:-(

John Mwaipopo said...

ni wakati sasa wanasiasa wajiulize maswali haya na si kufikiria allowances na posho mbili. kila la heri tanzania yetu

Anonymous said...

This is shocking! Hivi kweli Tanzania tuna umasikini wa kufikia hapa. Inasikitisha sana. Ni lini tutapata viongozi wazalendo? This a shame. Inauma kwamba wananchi wanaumia wakati, watoto wa viongozi wanasome International schools na abroad, wao na familia zao wakiugua watibiwa top private hospitals na abroad. How selfish are these people anyway. Inatia hasira pia.