Lakini uvunjwaji wake wanifanya niwaze kama kuna ulazima wa kujaribu?
Wazivunjao WANAWAZA NINI?
Labda tuanze INDONESIA ambapo kumekuwa na habari ya huyu "MTOTO" ambaye aonekana kuwa mdogo zaidi kumudu uvutaji wa sigara.
Nawaza kinachomfanya avute, alivyoanza, anayemuwezesha kuzipata na hata uvutaji wake unapofanyika kama hakuna waonao haya. Na nawaza kuwa kama anaweza kuvuta kwa "ufundi" kwa namna hii, amekuwa akivuta kwa muda gani? Na kama ana miaka miwili, na aligunduliwa na wazazi wake akiwa na miezi 11, alianza lini na alianzishwaje na nani??
Nawaza tuu kuwa kwa kufikia hivi waliomzunguka WANAWAZA NINI?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Mzee wa Changamoto. Asante kwa kunijulia hali mara kwa mara. Nimerudi kwenye chakula kitamu rasmi sasa. Tuko pamoja.
Post a Comment