
"If all Africa should unite, we'll be strong than any nation..... There will be no more WAR, there we'll be no more apartheid....."
Haya ni maneno aliyoanza nayo Innocent Galinoma katika wimbo wake mwanana UNITED STATES OF AMERICA ambao ndio zungumzo letu la leo kuhusisha fikra za msanii na maisha yetu ya sasa.

Maswali yangu kwa Inno Galinoma ni kuwa
CHANGAMOTO YETU: "Katika Albamu yako KILIMANJARO umeimba nyimbo zenye maswali mengi kwa Afrika na waAfrika (mfano Africans, Kilimanjaro na hata Running). Na katika albamu hiyohiyo umetoa baadhi ya suluhisho ambazo zingeweza kuwa msaada mwema kwa bara letu na waAfrika kwa ujumla kama katika wimbo huu United States of Africa.
Unapoangalia maisha yalivyo sasa ikiwa ni zaidi ya miaka 18 tangu utoe wimbo huo na matatizo uliyoyazungumzia yakingalipo na suluhu ulizoshauri hazionekani kufuatwa japo twajua zingekuwa msaada ama mwisho wa matatizo, UNAJISIKIAJE na hii inaweza kuathiri vipi kuendelea na fani hii?"
Na bila hiyana, Inno alikuwa mwepesi na wa haraka tena mwenye ukarimu kunijibu maswali yangu haya na hii ni sehemu ya majibu yake.

La mwisho, najisikia vibaya sana kuona jinsi baadhi ya wananchi hali yao ya maisha ilivo, I mean, People suffer so much just to live little life or just to survive in Africa, and That is a shame beacause Africa is rich. Unapoangalia mbele utaona wazi ya kuwa Africa inanunuliwa kimpangompango bila ya wanachi kujua kinachoendelea, japo mara moja moja utasikia kiongozi fulani amebakwa yuko mahakamani na magazeti na TV zikitangaza..... Almasi, Dhahabu, Tanzanite zitakuwa zinondolewa Afrika kwenda kwenye masoko ya nje bila ya wananchi kufaidika na chochote.
Nina Dada, shangazi, na mashemeji kibao, lakini sija wahi kumwona hata mmoja wao, amejiremba na Tanzanite."
KUHUSU HAYA YOTE KUATHIRI KAZI ZAKE AMA ZA AINA YAKE:
"ni kweli hii imeathiri sana utunzi na uimbaji wa nyimbo za aina yangu, la kwanza, ni kawaida kwa wasikilizaji hasa wenye umri mdogo na ambao ndio wengi, kutosikiliza nyimbo ambazo zinabeba ujumbe unaogusia maisha au matatizo,au kero za kisiasa ama magonjwa kama ukimwi na kadhalika. Wengi wanataka kusikia nyimbo zinazoburudisha na kuchekesha, kama wote tulivokuwa vijana. Wanataka kusikia na kucheza nyimbo ambazo zinazungumzia mabinti wa jirani, au bling bling, ama migari mikubwa mikubwa ama nyumba kubwa na "usafiri" wa mabinti na zaidi.... iko haja ya kuwahusisha vijana wajao, wenye vipaji na mawazo au fikra za kuburudisha na kuelimisha na kutangaza amani upendo na majambo yanajo husu jamii na mazingira na Tanzania na Africa kwa ujumla."
Sina ninaloweza kuongeza hapa. Blogu ya Changamoto yetu yamshukuru saana Kaka Inno kwa kutushirikisha kilichomsukuma kutunga, kinachoendelea kuumiza moyo wake kutokana na kutotatuliwa kwa matatizo na kile aonacho chaja siku zijazo.
Usikilize wimbo huu kiukamilifu hapa chini.
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
4 comments:
Hongera kwenye ukurasa wako na makala Nawapongeza ninyi!Inayohusiana na ...
Abstraction maandiko na kutafakari
Job well done Mr Bandio...Innocent is one among few musicians wanaothubutu kuongea sense na ukweli kwenye nyimbo zao..bila kujali.Congrats kwa kupata hii exclusive.
Mike Mhagama/LA.
Kaka,
Kila nitembeleapo blog yako huwa napata mambo mengi sana. Nakushukuru kwa hii United States of Africa. Ama kwa hakika ni wimbo wenye akili sana.
Nakutakia Jumapili njema wewe na familia yako.
Kibaraza hiki kina Changamoto Ahsante kwa wimbo United States of Africa. Kila la kheri.
Post a Comment