Saturday, August 7, 2010

Mdundiko.... Ngoma yenye timbwilitimbwili nyingiiii

Photo:Busaramusic.org
Photo: Angalia Bongo
Kwa sisi tuliokulia "kijijini" Dar Es Salaam tunalitambua hili. Mdundiko. Ngoma ambayo kwa hakika ilitufanya wengi kukumbana na mengi.
Mdundiko ulikuwa ukikusanya watu wengi na tukienda mwendo mrefu na katikati ukikusanya watu ambao kwa kuwa wanaongezeka "nje" ya ulipo wewe, unajikuta uko katikati na kama ndio mtoto basi hata namna ya kujisogeza pembeni huwezi.
Na humo katikati unasuguliwa na majasho na vikwapa vya watu na mpaka ngoma inazimwa, unarejea nyumbani (kama hutapotea) ukiwa una harufu itayomfanya mzazi atake maelezo ya kina juu ya utokako. Maana unakuwa unanuka kama zizi. Watu mamia, vikwapa vina "kwalite" tofauti ya kuachia harufu na wengine kuoga ni aleji kwao. Yaani ni mshikemshike tu
Kibaya zaidi ni kuwa TULISHAKATAZWA kuufuata maana watoto wanapotea saana lakini mara zote tukiuona tunajiaminisha kuwa tutaucheza kwa dk chache then tutarudi. Ukija shituka, unafika home wakati wanakula dinner.
Na sheria ya nyumbani ni kuwa kama giza limelazimisha taa ziwashwe, ina maana hustahili kuwa nje
SI BAKORA HIZOOOOOOOOOO
Na kwa wengine hii ikasababisha mengine mengi. Wapo wanaopata wanaowataka (wapenzi wapya) na wapo wanaoachwa kwa kufuata yasiyotakwa.
Kibaya zaidi, wapo waliokuwa wanatelekeza nyumba zao na matokeo yake kundi jingine "linalojiajiri" kuufuata mdundiko dakika chache "wanasafisha" nyumba za watu bila kipingamizi. Maana Mama na wana wote wamekimbilia ngomani
Msikilize George Kanuti Njogopa akikupa uhondo wa kinachoendelea katika mdundiko kwa kubofya hapa chini

Alaaaaaaaaaaaaaaaaa!! Kumbe hakumalizia? Basi fuatilia habari kamili na maelezo katika makala hii tamu na ya kusisimua kwa ku BOFYA HAPA

1 comment:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ngoma ya mdundiko si timbwilitimbwili tu bali usipokuwa makini inaweza pia "kuuchakachua" moyo wako.

Kulikuwa na "jimama" kule Temeke enzi zile nimepanga kule - tipwatipwa, jeupeeeee, guu guu, usafiri wa uhakika, umbo mkatiko - lilikuwa linajulikana kwa kutimbwilikatimbwilika na mdundiko pale mtaani na kuchakachua mioyo ya watu. Ilikuwa kazi kweli kweli...Ngoma ya pwani na mambo ya pwani!!!