NCCR-MAGEUZICUF ZANZIBARNA KADHALIKA
Maneno ya mwanzo yake Nasio Fontaine katika wimbo huu ni ya kuzingatia saana. Na naamini ndio maana ameanza nayo wimbo katika sentensi ya kwaanza kabisa. Anazungumzia kile kisichoonekana katika nyuso za hawa wagombea.
Maswali ama anayojiuliza ama kuyabainisha ndiyo ninayojiuliza.
Mfano1: Hawa wagombea ambao wanakuja na maelezo meengi kuhusu kuikomboa Tanzania walikuwa wapi muda wote wa miaka 5 iliyopita?
2: Hata Rais Kikwete ambaye pengine ndiye aliyeizungukia nchi kwa wingi, hakufika sehemu ngapi ambazo alifka wakati wa kupiga kura na hajaonekana mpaka atakapoingia sasa?
3: Ni kweli MACHUNGU YA NCHI yameanza kusikika ama kusemwa ama kuonekana mwaka huu na zaidi wakati huu ambao uchaguzi "unanukia"?
4: Ni kweli kuwa VIJANA wameona umuhimu wa wao kushiriki kuijenga nchi kule bungeni ama wamegundua kuwa bunge ndio mahala unapoweza kupata pesa kwa kusema ama kutosema chochote?
5: Kwani Dr Slaa anapoondoka bungeni ambako alikuwa kama "one man soldier" na kuingia kwenye Urais, anawaza kuupata ama kuipa Chadema nguvu zaidi ya kupata viti zaidi bungeni?
6: Hivi hawa wanaojifanya "kumwaga sera" wanatambua kile wanachostahili kufanya ili kuikomboa na kuisaidia Tanzania ya leo?
Nasio anasema "EVERY BABY KNOWS THAT TALK IS CHEAP...SOOO CHEAP"
Na ukweli wa mambo ni kuwa hakuna tunaloweza kujua kwa kuwaangalia usoni. Hatukujua kuwa Rais wetu hakujua kuhusu uongozi na kuwa alihitaji miaka ya urais kujifunza urais.
Mwishoni anasema "TIME AND TIME ALONE WILL PROVE THE STORY, AND EVERY EYE WILL SEE....TRUTH WILL REVEAL". Labda tumeanza kuona "time" inavyo-prove the story kwa wale walioshindwa kutenda waliyotumwa na wananchi kwa miaka kadhaa kuwekwa kando kupisha "wapya". Swali ni UPYA WAO na namna watakavyokuwa suluhisho la matatizo ya wananchi
Kabla ya sentenzi iliyopita, Nasio anasema "YOU SEE THEIR ACTION BUT YOU NEVER KNOW THEIR REACTION". Ukweli wake ni namna ambavyo twawaona wagombea wakiwa katika "maigizo" ya kujali wasiojiweza bila kujua wanavyowawezesha kuondokana na hali hiyo. Nimeona walemavu wakiwasindikiza kwenda kuchukua fomu na kujipanga kila waendapo kuhutubia lakini sijasikia MIKAKATI MADHUBUTI YA KUWASAIDIA WENYE UHITAJI MAALUM na kuwaweka katika nafasi ya kutokuwa tegemezi.
Je! Hatutakuwa sahihi kuamini kuwa WANAWATUMIA KUONEKANA WANAWAJALI ilhali ukweli ni kuwa hawaoneshi bayana wanavyoweza kuwasaidia? Basi msomaji nikuache usikilize kibao hiki chake Nasio Fontaine akisema TRUTH WILL REVEAL
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
1 comment:
Kaka nashukuru kwa posti hii. Kwanza nalazimika kuutafuta wimbo huu wa kizalendo wenye kufunza/kuelimisha na pia kuburudisha japokuwa wapo wale wasiotaka hata kuzisikiliza kazi hizi na kuziona ni za kidunia yani zipo nje ya mpango wa Mungu(ajabu ya kweli) ambao sitaki kuwaita waangamiao kwa kukosa maarifa.
Mimi nadhani, wale ambao walikuwa viongozi, tuwaulize wametufanyia nini ambacho wao, pamoja na sisi tunajivunia nacho, kabla ya kumpa/kuwapa nafasi nyingine. na sisi tujiulize kama tulikuwa chachu ya maendeleo au tulikuwa ni kikwazo.
Hawa wapya, wanaotaka uongozi kwa mara ya kwanza, wana sababu. Lakini wananchi hatuna budi kuwauliza nini sababu ya wao kugombea na kwa nini hawakuamua kumsupport kiongozi aliyekuwepo kabla ili aendelee, au kwa lugha nyingine tuwaulize ni kwa nini wameamua "kuwapinga" wale viongozi waliokuwa wanazishikilia nafasi kwa sehemu ambazo haziko wazi.
Post a Comment