Friday, August 20, 2010

Them, I & Them.......AFRICANS.....Innocent Galinoma

Inno awapo kazini. I looove his work
Leo ndio mwanzo wa KAMPENI za uchaguzi wa mwaka 2010. Uchaguzi ambao utatambua mustakabali wa waTanzania kwa miaka 5 ijayo. Miaka ambayo inaweza kuleta MABADILIKO kwa pande zote. CHANYA na HASI. Na ni wakati ambao twahitaji kuwakumbusha WAGOMBEA kuwa AFRIKA YETU ITAAMKA NA KUAMSHWA NA WA-AFRIKA WENYEWE na ni wao wanaoweza kuwa sehemu kubwa ya maendeleo kwa kuyachochea.
Katika kukumbushana haya, leo naomba kuwaelimisha na kibao hiki cha Innocent Galinoma kiitwacho AFRICANS
"tell the children the truth right now, right now; what's going on with their economy, rain is falling but there's no food why, where is justice, where is equality, why there is murder, poverty and blood everywhere, where is education, medication for my children?......tell me the truth right now" ni maneno toka kwake Innocent Galinoma Mfalingundi anapomalizia wimbo wake Africans. Kila mara ninaposikiliza kibao hiki (ambacho nimekisikiliza mara nyingi saana) najiuliza maswali mengi ambayo yameanzishwa na msanii ambaye ninaheshimu kazi zake kutokana na ujumbe wake na uwakilishaji wake (kuanzia lugha mpaka midundo kulingana na mahadhi atumiayo).Africans ni moja kati ya nyimbo ambazo ujumbe wake ni m'bichi leo kama ulivyokuwa wakati unatoka mwanzoni mwa miaka ya tisini. Katika kibao hiki, Inno anauliza mengi kuhusu Afrika na waAfrika akitukumbusha juu ya Upendo, Jasho na hata nguvu kazi zinazowekezwa barani kwa tumaini la kupata matokeo mema, lakini bado kinachojionesha dhahiri ni uasi na kukandamizwa kwa waafrika na kibaya zaidi vikifanywa na WaAfrika wenzetu ("..only this time the downpressor man Yeah!!, happens to be my own brother..")
Ni yale ayaonayo ambayo ameyaweka wazi katika wimbo huu yanayonifanya nishangae kama wale wenye mamlaka na madaraka wanatambua maswali ambayo wanapaswa kujibu kwa watoto wa Afrika ambao wanakabiliwa na matatizo haya sugu yasiyoonekana kuwa na mwelekeo ama tumaini la kutokomea ndani ya kizazi chao huku waheshimiwa hao wakiendesha na kuishi maisha mwanana. Ni hao hao ninaoamini anawashangaa kwa kuwakandamiza waAfrika wenzao na kujitengenezea maisha mazuri kwa mgongo wao. Swali kubwa analouliza Inno ni kwamba kwanini tusiishi kama Mungu alivyopenda tuwe? Tumekuwa watu wa visingizio vya kuwepo kwa rushwa, umaskini na mauaji kila mahali lakini ukweli utabaki kuwa tunashindwa kujiuliza twaelekea wapi. Anahimiza namna Mungu alivyotaka tuishi kwa "One Love, One Aim , One Destiny for everyone"

Nikiwa na baadhi ya wanamuziki waliorekodi wimbo wa HAKUNA kumuenzi Justin Kalikawe. Kutoka kulia (kwa msomaji) ni Ras Inno Nganyagwa, King Kirumo, mimi, Inno Galinoma, Jah Kimbuteh na wadau
Inno Galinoma ni kati ya wasanii wenye uwezo mkubwa saana wa kuwakilisha ujumbe-mkombozi kwa watu wa rika, imani, itikadi na asili mbalimbali kwa kutumia muziki anaoumudu vema. Kazi zake kama Kilimbanjaro ama Running zaweza kuwa kithibitisho kingine cha namna anavyoweza kuiweka jamii katika taswira halisi ya kile azungumzacho kiasi cha mtu kujihisi unaona liimbwalo.
HESHIMA KWAKO INNO NA SASA NI CHANGAMOTO YETU KUTEKELEZA YALE UTUELIMISHAYO.
Blessings
Picha hisani ya www.bongoland2.blogspot.comBofya hii player hapa chini usikie kipaji cha Inno kwenye kuwakilisha jamii

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.IJUMAA NJEMA

1 comment:

Maisara Wastara said...

"tell the children the truth right now, right now; what's going on with their economy, rain is falling but there's no food why, where is justice, where is equality, why there is murder, poverty and blood everywhere, where is education, medication for my children?......tell me the truth right now"

1. Kuna Ardhi, mito, mabonde na mvua za kutosha, lakini tunadanganyana na kilimo kwanza kwa njia ya propaganda (hakuna maandalizi ya kutosha)

2. Kuna madini na rasilimali za kila aina, miti wanyama na viumbe adimu duniana lakini wananchi hawanufaiki nanvyo.

3.Kuna ujambazi wa kutisha kila mahali hapa nchini, lakini Polisi wetu wanakuja na majibu mepesi kw amaswali magumu. WHY!

4.Elimu yetu inachechemea, na hakuna jitihada zozote za kuikwamua zaidi ya blah blah!!!

5. Matibabu yetu katika hosipitali za serikali zinatia kichefuchefu, hakuna dawa wala madaktari tunadanganywa na wanasiasa kuwa kutakuwa na zahanati kila kata klumbe ni maneno ya jukwaani tu.....