Friday, August 27, 2010

Them, I & Them....WASH AWAY TEARS......Gramps

"JAH shall wash away all the tears from my eyes. In times when the storm and the tides are raging high. We know we shall win and we'll survive....JAH SHALL WASH AWAY ALL THE TEARS"
Wachimbaji 33 waliokwama mgodini San Jose, Chile.
Kati ya habari ambazo zimeonekana kutawala vichwa vya habari ulimwenguni, ni kuhusu MAAJABU NA MASIKITIKO yawahusuo wachimbaji madini wa nchini Chile.
Nasema MAAJABU kwa kuwa wachimbaji hawa 33, wamegundulika kuwa hai baada ya kukaa siku 17 umbali wa futi 2300 chini ya ardhi. Ni jambo la kufurahisha, kufariji na kumshukuru MUNGU kwa uhai wa watu hawa ambao kwa siku hizo 17 walikuwa na makopo manne ya samaki aina ya Tuna kwa kila mmoja na mpaka kufikia leo yasemekana wamepungua wastani wa takribani paundi 22 (kilo 10) kila mmoja. Lakini pia nasema MASIKITIKO kwa kuwa licha ya kupata tumaini la kuwa wameonekana na kujulikana kuwa wako hai, bado wataalamu wanasema inaweza kuchukua kati ya miezi 3 hadi 4 kuweza kuwafikia. Yaani wameambiwa kuwa jitihada zafanyika ili wawe wametolewa chini huko kabla ya Krismas.
NI WAKATI MGUMU SAAANA.
Mgumu kwa wachimbaji na pia kwa ndugu zao ambao baada ya kusikia kuwa ndugu zao wote wapo hai, walimshukuru Mungu, kusherehekea na kisha kuanza maandalizi ya kuwapokea. LAKINI SASA WATASTAHILI KUSUBIRI KWA MIEZI MINGUNE MINNE.
Binafsi, habari kuwa nitastahili kukaa mgodini kwa miezi mingine minne, ingenifanya niwe jasiri kwa namna mmoja na pia kunivunja moyo kwa namna nyingine. Video ifuatayo yaonesha namna ambavyo maandalizi ya kuanza kuchimba shimo lenye kipenyo cha inchi23 (takribani tairi la wastani la baiskeli) na uchimbaji huo utakaoenda polepole, utachukua miezi kadhaa


Wakati tukiwakumbuka, kuwawaza na kuwaombea ndugu zetu hawa, naungana na wenye imani wote kukumbusha kuwa kwa sasa uwezo wa kibinadamu unaonekana kutowafikia huko walipo. Na pia watukumbushe kuwa licha ya kuwa na vitendea kazi viingi ulimwenguni, lakini bado kuna wakati ambao maisha yetu na yale ya tuwapendao huwekwa mbali na kimbilio pekee tunalokuwanalo ni MUNGU.
Kwa ndugu hawa walio machimboni, kwa ndugu zao wanaosubiri, kwa ndugu woote walio na matatizo duniani na ndugu wa ndugu zetu wenye magumu, nawakumbusha kuwa MUNGU PEKEE NDIYE AFUTAYE MACHOZI YA MAGUMU YETU.
Tumsikilize GRAMPS MORGAN wa Morgan Heritage akiimba WASH THE TEARS.

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duh, ila wengi tumekwama katika migod faluani fualni pia

Yasinta Ngonyani said...

Pole kwa wanandugu,watoto,wake, marafiki na wote wahusika MUNGU ndiye muweza wa yote.

emu-three said...

Ni kweli hapo ni dua kwa wingi, kwani muumba pekee ndiye anaweza yote