Sunday, September 26, 2010

MAKULILO SCHOLARSHIP SHOW

Nimepokea ujumbe toka kwa mdau Makulilo Jr. Ujumbe wa maana kwa wale wote walio na ambao wanaendelea kutaka kujua mengi kuhusu masuala ya Scholarship.
Kaka Makulilo anakualika akisema

"Nimeanzisha MAKULILO SCHOLARSHIP SHOW kwenye mtandao wa YOU TUBE ambapo nitakua nafanya recording ya "vipindi" kila wiki kuhusu mambo ya scholarships. Hii namini itasaidia kwa watu wengi kujibu maswali yao na kurahisisha mbinu za upatikanaji wa scholarships. Show hiyo inapatikana hapa kwenye account hii http://www.youtube.com/makulilofoundation
Tembelea link hiyo upate video clips za Show sasahivi.

Naomba maoni ya wadau nini nifanye kuboresha show hii. Kwa sasa show hii ina lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwani huduma yangu inasaidia watu wote wa Nchi Zinazoendelea japo msisitizo upo kwa Watanzania wapate nafasi hizi kwa wingi.

Kwa maswali au maoni, niandikie hapa makulilo@makulilofoundation.org

MAKULILO, Jr."

www.makulilo.blogspot.com
www.scholarshipnetwork.ning.com
www.makulilofoundation.org
www.facebook.com/makulilo.scholarships

No comments: