Ni MSIMU mwingine wa "waheshimiwa" kufurika ndani ya New York "kujadili" mambo mbalimbali kuhusu DUNIA. Kinachonisikitisha ni kuwa WANAKUSANYIKA KUJADILI LAKINI HAWASIKILIZANI. Pia wamegeuza "uwanja" uitwao Umoja wa Mataifa kuwa sehemu ya "mipasho" ambapo kila ajaye anasema lile ambalo sina hakika kama wanakuwa WANAWAKILISHA FIKRA ZA WATAWALIWA WAO.
Lakini baya zaidi ni kuwa WANAJITAHIDI KUSAKA UMOJA KWA KUTENGANA. Yaani akilini mwao wameshajua ni nani watamsikiliza na nani hawatamsikiliza. Wameshajua ni safari ya kumshutumu ama kumtukana ama kumlaumu nani hata kabla hawajaanza safari.
Jana tumeshuhudia (kwa mara nyingine) baadhi ya wajumbe wakiondoka vitini kumkacha Rais wa Iran alipohutubia. Nikasikiliza sehemu ya hotuba ya Rais huyo kisha nikawaza "HIVI HAYA NDIO MAWAZO YA WANANCHI WA IRAN? HIVI HAYA NDIYO WALIYOMTUMA KUSEMA. AMA?" Lakini nikawawaza walioondoka kwa "KUSUSA" kumsikiliza (japo ninaamini walienda kumsikiliza na kumuangalia mahotelini ama popote walipoenda kujikusanya) kuwa "HIVI NI KWELI KUWA HAWAMSIKILIZI KABISA AMA NI 'DANGANYA TOTO'? NA KAMA HAWAMSIKILIZI, WATAJUAJE KUWA AMEBADILIKA? KAMA WANAMSIKILIZA, NI TOFAUTI GANI KATI YA KUMSIKILIZIA KWENYE JENGO NA KWENYE VYOMBO VYA HABARI?"
Nikawaza na kuwazua kisha nikahisi VIONGOZI WA NCHI ZETU NI WANAFIKI KULIKO TUNAVYOWADHANIA.
Lakini si twajua kuwa hayajaanza leo haya?
Kumbuka nilichoandika kwenye makala ya "NI MIPASHO TANGU ENZI ZILE MPAKA SASA..." ambapo nilikumbushia mambo kadhaa hapa chini nikianza na nukuu yake Bushman aliyesema
"United Nation should be dealing with equal rights, it is the only chance it can give us INTERNATIONAL PEACE, they only pretend to be what they're not. One day, one day, i know there'll be PEACE. There will be peace on earth" Dwight Bushman Duncan
Nilimsoma Castro na speech yake ya masaa 4 na nusu. Nikamsikiliza Bush alipotoa speech kuhusu Saddam. Nikamsikia Chavez "alipomwaga radhi" mbele ya Umoja huu huu wa mataifa. Kisha Ahmadinejad naye akaweka sera zake. Jana tulikuwa na Ghaddafi akimwaga news bin news.Napenda kujua kama hawa viongozi huwa wanakwenda "Umojani" na hoja za kitaifa ama pale ni kwenda kunangana wakijua ulimwengu unawaangalia?
Nina hakika kuna namna ya kujiuliza hili kwani japo halijatokea na wala halitegemei kutokea kwa Rais wangu, nimetokea kujiuliza kama Rais kama Kikwete huwa anawajulisha wabunge (ambao wanastahili kuwa wawakilishi wa wananchi) kuwa anaenda Umoja wa Mataifa hivyo akusanye maoni na kujua MAHITAJI NA HOJA HALISI ZA MTANZANIA ama?
Najiuliza tuuuuu, hivi huwa wanatumwa ama wanaagizwa???? Ama wanasema waonavyo wao?
Wanalofanya hawa ni KUONGEA na kuongeleshwa bila kuhakiki kama wasemayo ni AKISI ya wananchi wao. Wanasahau kuwa MATENDO HUSEMA ZAIDI YA MANENO.Msikilize Bushman katika wimbo huu TALKATIVENina hakika kuna namna ya kujiuliza hili kwani japo halijatokea na wala halitegemei kutokea kwa Rais wangu, nimetokea kujiuliza kama Rais kama Kikwete huwa anawajulisha wabunge (ambao wanastahili kuwa wawakilishi wa wananchi) kuwa anaenda Umoja wa Mataifa hivyo akusanye maoni na kujua MAHITAJI NA HOJA HALISI ZA MTANZANIA ama?
Najiuliza tuuuuu, hivi huwa wanatumwa ama wanaagizwa???? Ama wanasema waonavyo wao?
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
No comments:
Post a Comment