Friday, September 3, 2010

Mimi najifunza kitu. Wewe je?

Nilimsoma saana nikiwa nyumbani. Wengi humsema kwa namna wamsemavyo nami sipendi kila asemacho wala kuandika, lakini HAKUNA UBISHI kuwa ni kati ya watu ambao niliposoma habari ya maisha yake kwa mara ya kwanza mwanzoni wa miaka ya 2000, nilitambua kuwa NAMI NAWEZA.
Hapa chini kuna sehemu anasema "There are people with idea but no money, but there are people with money but no idea....... you have to take a risk"

13 comments:

Anonymous said...

I thought ni mtu wa maana kumbe ni Erick Shigongo - mtu ambaye ametuharibia vijana wetu kwa magazeti yake ya ngono???? In God We Trust, In God We Can na upuuzi mwingine wakati huo huo anaandika exclusively juu ya ngono, ngono, ngono...His money stinks!!!

Halafu he trashed the late beloved Amina Chifupa for his political gains. And if you don't know, HE WAS THE OWNER OF ZE UTAMU - the notorious blog that caused a lot of chaos. And you have the audacity to put him here on the blog that I love as a role model? Role model for what? Shame on both of you!!!!!!

There is NOTHING good to learn from this guy. Are you also planning to follow in his footsteps and launch a sex tabloid? When? HEARTLESS MJASIRIAMALI!

Mzee wa Changamoto said...

Great view ANON.
Mimi sipangi kufuata nyayo zake, na wala sikubaliani na kila alichokifanya.
Yaonekana BAADA YA KUFANIKIWA ndipo alipokuja kutenda atendayo. Napingana na sehemu ya maisha na maamuzi yake lakini ujasiri aliokuwa nao wakati ameamua ku-take risk na kuhamia Dar na kusaka aliyoamini ni sahihi ndio ninaouongelea hapa.
Hakuna mtu anayeweza kukubaliana na yeyote kwa asilimia mia moja. May be hata 90. Lakini kuna kitu ambacho ukikifanya ama kuchukua toka kwa mtu utanufaika.
Binafsi ile courage aliyokuwa nayo kupambana na fikra za awali za umaskini ndio niizungumziayo
Kuhusu Ze Utamu, nimekuwa naipinga haijalishi ni nani amekuwa mmoliki. Na sitaweza kuungana na yeyote katika hilo hasa kwa kuwa aliandika yasiyo sahihi na ya kupakazia.
Kwa hiyo nakubaliana nawe kuwa kuna MABAYA ambayo vyombo vyake vimefanya na nakubaliana nawe kuwa kuna mengi ambayo si ya kuiga, lakini kuna ambalo kama una nia ya kusonga mbele unaweza kuchukua kimoja toka kwa mtu na kusonga mbele. Kwani ni nani asiye na mabaya? Ama ni mabaya gani yasiyo na uzuri upande wa pili?
Ninakubaliana nawe kuwa WAKATI TUNAJITAHIDI KUJIFUNZA NA KUIGA TOKA KWA WATU, TUKUMBUKE KUEPUKA KUIGA KILA KITU KWANI WATU HAWA HUTENDA MAMBO MENGINE YASIYOFAA AMBAYO YANAIATHIRI JAMII
Labda ningeweka "dakika" za kile ambacho ningependa mtu atambue kuwa nilijifunza na kwa kutofanya hivyo, nilikosea na kuonekana kukubaliana na kila kitu maishani mwake.
Shukrani kwa muda wa thamani kusoma na kutoa maoni

Anonymous said...

It is me anony. again.

Good points. But sometimes what you do trumps everything. I doubt if there is anything good that we can learn from Adolf Hitler. Or Kapteni Makamba ambaye alibaka na kupiga mimba mwanafunzi and now he is our national leader.

I agree with you on some points but there are some actions in our lives that trump our position to stand up and be a role model. Na haya aliyoyafanya Shigongo, in my view, fall into this category.

Amekulia katika umasikini and he followed his dreams but at what cost? How many people were hurt by the UTAMU? How many kids have been hurt by his stupid sexual tabloids? NO, HE CANNOT BE A ROLE MODEL TO ANYBODY!!!

Mzee wa Changamoto said...

Ok Anon.
Great to have you back
Kama hakuna kitu twaweza kujifunza kutoka kwa Shigongo, kuna kitu cha kujifunza kuhusu watu kama yeye.
Umeniajulisha mengi ambayo sikuyajua (japo sina hakika nayo). Lakini mstari wako kama "there are some actions in our lives that trump our position to stand up and be a role model." ni pointi njema ambayo NAFARIJIKA KUJIFUNZA.
Na siamini kama mimi nawe tungeweza kuwa na mawasiliano na mafunzo kama haya kama isingekuwa post hii.
Wapo wanaopinga ANONS kwenye blogs lakini naamini uwepo wao kwa namna moja ama nyingine unatufunza. Ninaamini umekuwa comfortable kusema ukweli na maarifa haya kama anon na si vinginevyo. Na hii ni faida ya wale tuwaonao hawafai
Sasa kuna la kujifunza. Binafsi sijajifunza kuhusu BIASHARA YAKE YA MAGAZETI, bali alivyoweza kuamini wazo la biashara. Wengine wanaweza kuamini muziki, wengine uinjilisti, wengine siasa nk.
Kile kinachofuata baada ya kufuata ndoto zao ni ego. Na hapo ndipo tunapotakiwa kujitenmga nao. Siigi kila kitu (hata toka kwa baba yangu).
Lazima tujifunze kuwa kwa mema tunayotenda, kunakuwa na point tunachemka na hapo ndipo wengine wajitenge nasi.
Iwe siasa ama lolote.
Ukisema HITLER wapo wanaomzungumzia kama mmoja ya watu waliothamini mbwa kuliko mtu yeyote. Nimeliona hili kama mfano kwa wapenda wanyama. Unadhani atataka umuulize la ziada? Hapana.
Kwa hiyo kila kitu kina faida na ubaya na kama kuna uwezekano wa kunyambua na kunyofoa just faida na kuondokana naye, then do it. Kibaya ni KUIGA badala ya KUJIFUNZA.
Na hata kwa MABAYA usemayo juu yao, tunaweza kujifunza namna ya kuepukana nayo "next time"
Kumbuka makala yangu iliyouliza kama UBAYA HAUNA FAIDA (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/06/ubaya-hivi-una-faida.html) na mtazamo wangu kuwa "Hakuna kibaya kisicho na uzuri...... Yategemea umeachia wapi kuoanisha na tukio" rejea hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/09/hakuna-kibaya-kisicho-na-uzuri.html
Na kwa mabaya ambayo unazungumzia kuhusu watu kama Shigongo, na kwa mtazamo na maelezo mapya niyapatayo, NINAELIMIKA KUANGALIA KWA UNDANI ZAIDI katika kila ninayemfuatilia ama kufurahishwa na sehemu ya elimu yake
NA KWA HILO NAJIFUNZA.
Shukrani kwa kuzidi kunielimisha na tuzidi wasiliana.
Blessings

Anonymous said...

Mjadala mzuri. Hiyo ya Hitler kidogo made me laugh. Pengine suala ni mtu anakuwa role model kwa nani? Kwa jamii? Hitler ni role model kwa Skin heads, Aryan Brothers and other racist organizations, Rednecks na wengineo lakini KAMWE hawezi kuwa role model kwa kwa jamii na humanity. Natumaini hata wewe huwezi kuweka picha za Adolf Hitler katika chumba cha watoto wako huku ukiwaambia kwamba ni role model wao japo naye grew up in poverty, barely went to school (katika kitabu chake cha Mein Kampf he butchered the German language); and he rose to become the most prominet figure in human history - but in a wrong way.

Nina wasiwasi pia kama utaweka picha ya Erick Shigongo in your daughter's room ili awe role model wake. Akikuuliza utamwambia nini? He came to Dar es salaam without money then he launched ZE UTAMU and sexual tabloids (hiding under Ulokole umbrella) until he got rich? What message will you be conveying? To get rich kwa njia yo yote ile? No!

Yes none of us is perfect but, as I said on my previous post, not all of us can be role models and good public figures. Ingekuwa kwenye true democratic countries huyu asingethubutu hata kugombea huo Ubunge huko kwa Wasukuma wenzake Buchosa. JK naona kamfanya msemaji mkuu wa CCM kule Buchosa and I believe he is going to get a title may be D.C or R.C. What a shame.

Lakini this is OK in our country. That is why people like Lowassa, Chenge and others with dirty hands are still doing OK. Things are changing but we still have a long way to go.

I know uko makini sana and you love Tanzania ndo maana kidogo nimeshangazwa na wewe kumuweka Erick Shigongo hapa eti kama role model wetu na tujifunze kwake. Kama hatuwezi kujifunza kutoka kwa watu waadilifu na ambao wamepata pesa zao kwa njia za halali basi tumepotea na tunajenga jamii yenye njaa na inayotukuza na kushabikia wizi na ukosefu wa maadili. If this is the case, we are lost and we don't know where we are going!

Erick Shigongo is NOT and WILL NOT be a role model for our youth no matter how compelling his past is.

Should we also praise drug dealers who rise from poverty and become rich? If not, wana tofauti gani na Shigongo mwenye magazeti ya ngono, ZE UTAMU na upuuzi mwingine????

Tuendeleze mjadala kwa heshima hii hii. I am kind of liking this kwani I am also learning a lot about you, your blog and...

Mzee wa Changamoto said...

Ndugu yangu ANON. HESHIMA NDICHO KITU NIPENDACHO NA KUKITOA ZAIDI. NASHUKURU KWA KUKITHAMINI NA KUKIENDELEZA HAPA HUKU TUKIELIMISHANA
NAAMINI SAANA KATIKA HESHIMA NA SHUKRANI KWA KUIENZI


Kuhusu HITLER, niliisoma hiyo shule nami kama wewe NILICHEKA. Lakini upande wa pili nikakubaliana na suala kwamba "shujaa wako ni gaidi wa mwingine" NI KWA KUWA HATA SIKU MOJA DUNIA HAITAKUWA NA MTAZAMO MMOJA WA KITU kwani kuna ambao wanachukia kuona kingine kikipendwa.
Umeonesha wasiwasi kama nitaweka picha ya Eric Shigongo chumbani mwangu nami nataka kutoa wasiwasi kuwa SITAWEKA.
Sina hakika kama kilichonifanya nimsikilize chaweza kumfaa mtoto wangu.
Nililojifunza ni kuwa wapo watu wanaweza kuwa mashujaa ama maadui kwa kile wanachofanya wakati husika na mara nyingi kile cha mwisho kupingana na kile cha awali huvutia watu wanaokubaliana naye. Sina hakika na imani yako, lakini mimi nimehudhuria ibada za "walokole" na namna mtu anavyotaja madhambi mengi aliyofanya na yalivyokuwa ya kutisha, na sasa AMEMPOKEA BWANA, utaona jinsi ambavyo watu wanaoamini kuwa wana "dhambi ndogo" zaidi ya huyo wanavyoona nguvu ya Mungu. Ina maana aliye na dhambi zionekanazo kuwa kubwa akibadilika na kushuhudia aliyowahi kutenda, anavuta wengi na kuonekana ni "mfano" wa mabadiliko.
Lakini pia hata wale wanaowaasi watu na kuwageuka hutumika kama "shujaa" wa nini kibaya chaendelea upande wa pili. SI UNAONA KWENYE SIASA??????
Lakini pia NINAKUBALIANA NAWE unaposema "not all of us can be role models and good public figures." Huu ni ukweli na inasikitisha jinsi nionavyo watu wanahangaika kuusaka huo u-role model. Tatizo ni kuwa katika kufanya hivi, (kama alivyoimba Ziggy Marley) kuwa "we lose ourselves just to try to find who we are".
Kuhusu ulilozungumzia kuhusu "nchi ya demokrasia ya kweli", naamini mambo mengi yasingetokea kwani sio tu yeye asingeweza (kama ni kweli anafanya) hayo usemayo ya kuendesha mitandao kama Ze Utamu.
Ninaposema kama amefanya ninamaanisha kuwa sina hakika na sijasoma mahala popote kuwa amekutwa na hatia kwa hilo. Kwa hiyo ni katika hili nisionekane namtetea, bali sina hakika tu.
Pia umesema "Should we also praise drug dealers who rise from poverty and become rich? If not, wana tofauti gani na Shigongo mwenye magazeti ya ngono, ZE UTAMU na upuuzi mwingine???? "
Nafikiri we shouldn't PIAISE THEM. Ila kuna kitu cha kujiuliza ni kipi twaweza kujifunza toka kwa drug dealers.
Ni kwanini wana ujasiri wa kusaka njia za kufanikiwa licha ya "magumu" yanayowakabili? MAGUMU KWA MAANA YA KUPINGWA NA JAMII.
Lakini napenda kusema kuwa kuna makwazo ama obstacles ndogo ndogo ambazo ziko kwenye maisha yetu ya kibiashara ambayo sio tu yanakabilika, bali hayahathiri uhai wetu. Sasa kuna kitu ambacho tunatakiwa kujifunza kwa hawa watu. Ni lazima tuwaulize kwanini ama ni vipi hawaogopi mkono mrefu wa sheria? Tukijua namna wakabilianavyo na ugumu huo mkubwa, tunaweza kuwafunza wajasiriamali kutokata tamaa wanapokutana na makwazo madogodogo. Lakini cha kuepusha ni kuhakikisha kuwa hatuwafanyi ama hatutengenezi wauza madawa wapya baada ya kuwapa UJASIRI.
Kwa hiyo katika kila tufunzacho watu katika kuikabili hali ngumu, kuna kitu cha kuepuka ili kuhakikisha tuna-deliver kile tudhamiriacho.
Namaliza kwa kusema kwa sentensi uliyoisema kuwa "Things are changing but we still have a long way to go."
NASHUKURU KWA MICHANGO NA CHANGAMOTO ZAKO.
Najifunza mengi na naamini mjadala unazidi songa kwa wema.
Karibu na Shukrani tena

Anonymous said...

Ni Anony again na sina maneno mengi sana safari. Nitatoa ufafanuzi wa kile ninachodhani kwamba ni backbone ya huu mjadala.

"HAKUNA UBISHI kuwa ni kati ya watu ambao niliposoma habari ya maisha yake kwa mara ya kwanza mwanzoni wa miaka ya 2000, nilitambua kuwa NAMI NAWEZA"

Pengine swala lililozua hii debate ni "NAWEZAJE?" Nakubaliana nawe kwamba kila life story ya mtu ni compelling and touching. Ile kuzaliwa tu tukiwa hoi na full tegemezi namna ile is compelling. Hata life story ya Shetani as told in the Bible is very compelling: kuwa malaika mkuu kule mbinguni, kuasi na kisha kutupwa hapa duniani; and he never flinched. He is still fighting to the end huku akijua his destiny is not good. Isn't this perseverance to the end??? Hata ma-serial killers walioua watu wengi have compelling life stories. Walipataje ujasiri wa kufanya hivyo? Hawakuogopa kushikwa na kunyongwa? And so are the drug dealers kama ulivyosema.

Life story ya Shigongo yes is compelling na inatuonyesha kwamba YES WE CAN but the real question is TUNAWEZAJE? Kwa kuharibu kizazi kizima kwa magazeti ya ngono huku tukitumia ulokole? Kwa kuanzisha blogu ya kudhalilisha watu wengine ili kujipatia umaarufu? Hiki ndicho ninachopinga; na ndiyo maana nikasema "Kama hatuwezi kujifunza kutoka kwa watu waadilifu na ambao wamepata pesa zao kwa njia za halali basi tumepotea na tunajenga jamii yenye njaa na inayotukuza na kushabikia wizi na ukosefu wa maadili"

Kuonyesha watu that we can is not an issue kwa sababu kila mtu can do that, the real issue is TUNAWEZAJE? Si kila mmoja wetu can stand up na kusema kwamba ni role model wetu na kwamba ana kitu cha kutufundisha kama kipengele cha TUNAWEZAJE kimeegemea kwenye NEGATIVE. Ndiyo maana I believe kwamba ingekuwa kwenye nchi za wenzetu NO BODY will take people like Shigongo seriously. Ni kwa sababu hii ningali bado nashangaa kidogo kwa mtu makini kama wewe kumuweka Shigongo hapa ili atufundishe kitu. He lost his right to teach us anything by failing the TUNAWEZAJE part - which I believe is more important and is the one that real sets us apart.

Tukumbuke kwamba it is the TUNAWEZAJE part (and not the TUNAWEZA part) that makes people great and role models. And Shigongo fails miserably!!!

Mzee wa Changamoto said...

Kwako Ndg Anon
Nadhani maoni yako ya mwisho YAMEELEZA KIINI cha pale ambapo mimi nawe tumekuwa tukijaribu kuangalia uhalali wake. Yawezekana kweli kuwa mimi niliegemea kwenye TWAWEZA na kuachia hapo nikiamini kuwa ukishajua kile kilicho sahihi ndani mwako na ambacho chaweza kuwa baraka na faida kwako na kwa jamii yako, ni wakati wa kuachana ana aliyekupa fikra na ujasiri na kisha kusonga mbele kutimiza ndoto sahihi na halali.
Nawe mwenzangu umekwenda even deeper kuonesha kuwa kuweza ni kwa kila mtu ila TUNAWEZAJE ndilo la kuangalia.
Binafsi kama nilivyosema kuwa nimekuwa nikisema FIKIRIA UJASIRI AMA UBUNIFU WA MTU kisha uutekeleze katika yale mema yaliyo ndani mwako, lakini umenifungua macho kuwa si kila mtu anaweza kutenganisha hayo, na si kila mtu katika jamii ataachanishwa na "ALIWEZAJE" yake ambayo yaweza kufunika kabisa "ALIWEZA" yake.
Je naamini uko sahihi???
KWELI KABISA. NI UPEO AMA KIKOMO CHA FIKRA AMBACHO SIKUGOTA AMBAPO UMEGOTA WEWE.
Je!! Ni sahihi kwa mimi kumuweka hapa Erick Shigongo? Labda waweza ona si sahihi lakini NIMEJIFUNZA MEENGI AMBAYO SINA HAKIKA KAMA NINGEWEZA KUJIFUNZA BILA KUWEKA POST HII, na pengine nilichojifunza sasa kimeniepusha kufanya hili (kwa maana ya kutokuwa makini kutenga ALIWEZA NA ALIWEZAJE) mahala pakubwa zaidi, kwa mtu ambaye ana "ALIWEZAJE" mbaya zaidi na ambaye angefanya wengi wasinielewe (tofauti na wewe uliyenielewa na kisha kunielewesha)
Je!! Nitaiacha hii pst na kuwakaribisha wengine kuona ulivyoangalia jambo hili kwa JICHO LA NDANI? ABSOLUTELY.
Naamini maarifa na uchambuzi wako hapa unaweza na utawafaa wengine kama ambavyo umenifaa mimi.
Again, karibu tena na tena na nimefurahia uwepo na ushiriki wako.
Natumai kila kifunzwacho hapa ni manufaa kwani ama kitaepusha mabaya zaidi na / kuboresha uelimishaji zaidi.
KILA SIKU TWAKUA KIFIKRA KWA KUWA KILA SIKU KUNA JAMBO LA KUJIFUNZA. NA HII NDIO ELIMU TUHITAJIYO

Zaidi ya yote asante saana kwa maoni yako ya mwanzo ambayo licha ya kuonesha kuwa aliyepo aliku-set off, lakini ukaeleza usichopenda kuhusu mtu huyu kwa HESHIMA ukitambua kuwa hata bila kufanya hivyo hakuna ambaye angekujua. Kwa hilo NAKUHESHIMU SANA
Baraka kwako ndugu yangu

Anonymous said...

Ni mimi tena.

Kwanza niseme THANKS kwa jinsi mjadala huu ulivyouendesha na unavyouendesha. Blogu ni yako and you would have just shut me off and delete my comments. Thanks kwa kuheshimu maoni yangu na kuyaacha hapa. That says something about who you are. You are young but una wisdom sana tu. Ukizeeka naona itakuwa balaa!

Ndiyo - inabidi tutenganishe the TUNAWEZA na TUNAWEZAJE part kama kweli tunataka kuleta influence nzuri kwa watoto wetu na jamii kwa ujumla. Siyo drug dealer ambaye amekulia katika umasikini na sasa ana Rolls Royce nne na maghorofa kila mji eti tumruhusu atufundishe kitu na kuwa role model wetu - HAPANA!. Huyu TUNAWEZAJE part inakuwa imempotezea haki hiyo.

Hali kadhalika mwanasiasa aliyetokea kwenye umasikini mkubwa na leo hii kapata uwaziri, akachota mabilioni ya dola za wananchi na kutajirika sana. Hataweza kuwa role model wetu japo ni kweli kaweza lakini ile KAWEZAJE part inamhukumu.

Kwa wakati huu wa utandawazi nadhani ni muhimu kufanya hii distinction kwani ndiyo hasa itakayotupambanua who we are na tunataka kujenga jamii ya namna gani huko tuendako.

Mwisho napenda kusema kwamba nimejifunza mambo mengi kutokana na hoja zako FIKIRISHI and as you have been saying all along - tufundishapo ndipo tufunzwapo au pengine ni-reverse na kusema tufunzwapo ndipo tufundishapo. What I am saying here is that - hakuna mshindi wala mshindwa katika mjadala huu (na mingine) kwani wafanya mjadala wote hufaidi. Na aingiaye kwenye mjadala akitaka kushinda basi ni mjinga.

Much RESPECT to you and I will continue to be a LOYAL mdau of this thought-provoking blog I call CHANGAMOTO YETU.

Jah Man!!!!

Mzee wa Changamoto said...

Thanx again Anon.
Naamini tutaendelea kuelimishana saana katika mambo mbalimbali.
Nitawaonesha watu MAFUNZO ya kufunzwa ukifunza ambayo nimeyapata hapa
Blessings

Fadhy Mtanga said...

Nakumbuka kuna mahali kaka yetu Prof Matondo aliwahi kuandika kuhusu Mubelwa Bandio....alisema, umemfundisha kuwa hekima haipatikani kwenye mvi tu.

Anon karudia jambo hilo hilo.

Nami nisiharibu sifa hizo. Ila nisema unazistahili. Namna ulivyoendesha mjadala huu, wengi tungeshindwa na pengine kuishia kushambuliana. Anon naye ameonesha uungwana sana tofauti na ma-anon wengi ambao huficha majina yao ili kumshambulia mwenye blog..

Kuhusu Shigongo, nilisoma maelezo kwa kirefu sana kuhusu yeye kwenye blog ya da Chemi baada ya kifo cha Amina Chifupa.

Kwa kuwa wakati wa kuelekea uchaguzi, Amina alipotangaza nia, nilizisoma makala zake zilizokuwa zikimshambua Amina pale kolamu ya Napasua Jipu, sikushangaa sana.

Sitaki kusema mengi maana wengi wamekwishasema sana. Ila madhara ya mmomonyoko wa maadili yatakitafuna kizazi hiki chote na kijacho.

Naomba tu nami nikope maneno ya kaka mkubwa Ziggy Marley, "tunajipoteza wakati tunajaribu kujitafuta."

Unknown said...

HII NI CHANGAMOTO YETU KWELI KWELI...INAFIKRISHA!.

Unknown said...

HII NI CHANGAMOTO YETU KWELI KWELI...INAFIKIRISHA!.