Friday, September 3, 2010

Them, I and Them......JERUSALEM, SOLDIER

Ni mwisho wa wiki ya mwanzo wa mwezi. Na kama ilivyo ada kwa kila Ijumaa, twajiunga kusikiliza, kutafakari na kisha kuhusisha ujumbe katika muziki wa Reggae na habari zitokeazo katika wiki husika.
Na leo si tofauti.
Moja kati ya hatua ambazo serikali ya Marekani imeweza kufanya kwa wiki hii ni kuanzisha kile ambacho (iwapo kitafanikiwa) kitaweka msingi imara wa amani katika nchi za mashariki ya kati.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Natanyahu na Rais wa Palestina Mahmoud Abass wakiwa na Rais Barack Obama wa Marekani kuelekea mazungumzoni.
Photo Credit:
REUTERS
Wiki hii Rais Barack Obama wa Marekani anafanya mazungumzo yatakayowakutanisha ana kwa ana viongozi wa mataifa ya Palestina na Israeli. Mazungumzo haya yana tumaini la kufanikisha kufikia makubaliano ya kuleta amani ya ukanda wa Mashariki ya kai ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. NI HATUA KUBWA na kama itafikiwa ukingoni na kufanikiwa, itaanzisha UKURASA MPYA WA AMANI baina ya mataifa haya ambayo kwa miaka nenda rudi yamekuwa yakipigana na kusababisha vifo vya maelfu ya watu wasio na hatia. Itakuwa taswira njeema sana kuona ndugu wa mataifa na dini mbalimbali wakiishi pamoja na kuabudu kwa uhuru, kama alivyoimba Alpha Blondy katika wimbo wake JERUSALEM akiona mustakabali utakavyokuwa akisema "You can see Christians, Jews, and Muslims living together and praying AMEN. Let's gives thanks and praises"
Sikiliza kibao hiki hapa chini

Na pia waweza kufuatilia mashairi yake hapa chini

Lakini pia, Rais Obama wiki hii ametangaza kumalizika kwa operesheni za mapambano ya kivita nchini Irak na kusema kuwa sasa "jukumu jipya la Marekani nchini Iraq ni kutoa ushauri na msaada kwa vikosi vya usalama vya Iraq.". Vifaa vya kivita vya mwisho vikivuka mpaka wa Iraki kuingia Kuwait.
Photo Credit:
Natalie Cole/AFP/Getty Images and Maya Alleruzzo / AP
Hii ni hatua kubwa kwa wanajeshi na wananchi wa Marekani kwa kuwa vita hii imegharimu zaidi ya maisha ya watu nchini Irak. Lakini bado ATHARI ZA VITA zitaendelea kuliandama taifa hili kwa kuwa hata wanajeshi warejeao nchini, wanaendelea "kuandamwa" na fikra za yale waliyoyaona, wanakuwa wakorofi, wakatili na wengi wanajiua na kuua wenza na familia zao. Hii ni hali ya kusikitisha hasa kwa takwimu zioneshavyo kwani ni dhahiri kuwa licha ya kushinda ama kushindwa vita, wanajeshi walioshuhudia mapambano bado wanaendelea kuwa na HATIA mioyoni mwao ambapo mwezi Aprili mwaka huu, makala toka mtandao wa AmryTimes.com iliripoti kuwa wanajeshi (waliokuwa vitani) 950 hujaribu kujiua kila mwezi na 18 hujiua kila siku nchini Marekani.
Hii namba ni kubwa mno na inatisha.
Na hili (la askari kujiua kutokana na HATIA mioyoni mwao) lilisimuliwa vema kabisa miaka 7 iliyopita naye Phillip Lucky Dube katika wimbo wake SOLDIER ambaye alisimulia alivyokuwa amekaa mbele ya askari aliyekuwa tayari kujilipua kwa HATIA ya yale aliyotenda vitani ambako alikwenda na kufanya hivyo kwa kuwa tu alielekezwa na "JENERALI". Askari anakaririwa akisema "not a day goes by I don't see them in my dreams, not a day goes by I don't hear them screaming in my ear. Begging for mercy, pleading innocent. Since my heart is made up to be as coldas the barrel of this gun I hold, I would pull the trigger anyway .I was a soldier, following instructions from a man we have known as the general"
Sikiliza kibao hiki hapa chini

na kama wapenda kusikiliza huku ukifuatilia mashairi, basi BOFYA HAPA KWENYE TOLEO LA AWALI LA WIMBO HUU
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA