Saturday, October 9, 2010

Shimo la uokozi lawafikia wachimbaji wa Chile

Wachimbaji 33 wa chile waliokwama zaidi ya nusu maili mgodini tangu August 5 mwaka huu. Sasa shimo la uokozi limewafikia na uwezekano wa kuanza kutolewa ni mkubwa saana.
Siku ya Ijumaa ya August 27 niliandika hapa kuwahusu na kuweka ujumbe wa wimbo wa Gramps Morgan aliyeimba "JAH shall wash away all the tears from my eyes. In times when the storm and the tides are raging high. We know we shall win and we'll survive....JAH SHALL WASH AWAY ALL THE TEARS.In this time of destruction, we must hold on firm, we got to get along.....WE KNOW WE MUST WIN THE FIGHT.....WE KNOW THAT JAH IS THE BEST OVER TRIALS AND TRUBULATIONS"
Na ndivyo "ndugu" hawa 33 walivyofanya. Waliungana, waliheshimiana, walichagua viongozi wa kuwasaidia kimaamuzi, ki-imani, kimatibabu na msemaji. Walikuwa kama wana "serikali" yao mgodini.
Hivi ninavyoandika, taarifa za faraja kwa wengi ni kuwa lile shimo la uokozi ambalo lilielezwa kuwa lingewafikia wachimbaji walionaswa kwenye machimbo huko chile, limefika mahala walipo. Sasa matumaini ni kuanza kuwatoa shimoni kuanzia siku ya Jumatatu usiku ambapo hii imeonekana kuwa mapema saana kuliko ilivyotarajiwa awali.
Ikumbukwe kuwa watu 33 walikwama machimboni baada ya mgodi huo kufunga njia August 5 mwaka huu. Walikaa kwa majuma matatu wakiwa na chakula haba mpaka walipokuja kutuma ujumbe kwa waokozi waliokuwa wakichimba mashimo kujaribu kutafuta walipo na ujumbe huo uliopokelewa kwa shangwe ulisema wote 33 wako pamoja na ni wazima. Na ni hapa ninapoamini kuwa kuna wakati ambao HAKUNA MWANADAMU ANAUYEWEZA KUWA NA UKOMBOZI AMA MSAADA WA NAMNA YOYOTE ILE, BALI MUNGU MWENYEWE. Kwa waliokwama na kwa faraja za familia zao.
HII CHINI NI KUMBUKUMBU YA MCHAKATO WAO na habari kamili juu ya taratibu zitakazotumika kuwaokoa, watakavyotengwa na kushughulikiwa mmoja mmoja baada ya kuletwa ardhini, watakavyosaidiwa kiakili na mengine mengi waweza kuzisoma hapa CNN


Narejea wimbo wa GRAMPS MORGAN niliounukuu hapo juu kuwa ni "MUNGU PEKEE ATAKAYEWEZA KUTUFUTA MACHOZI PALE TUWAPO KWENYE DHORUBA KALI NA MAWIMBI MAKUU"

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Huu ni muujiza kabisa. Natumaini kwamba kila kitu kitakwenda sawa kwa mapenzi ya Mungu na wachimbaji hawa wataokolewa.

Kwingineko tunayo mengi ya kujifunza kutokana na juhudi za Chile katika kukabiliana na majanga kama haya. Tuliona maajabu wakati ule wa tetemeko la rdhi na sasa janga la hawa wachimbaji wa madini. Mpaka Wamarekani wenyewe wanashangaa.

Ingekuwa sisi sijui ingekuwaje. MV Bukoba ilipozama ilikuwa kasheshe nguo kuchanika na inavyoonekana hakukuwa na mtu aliyekuwa anajua nini la kufanya. Kukiwa na moto au majanga mengine zimamoto wetu huenda bila maji ali mradi ni kasheshe tupu.

Hebu soma hii makala kutoka gazeti la Habari Leo uone ninachokizungumzia hapa: http://www.habarileo.co.tz/safu/?n=10508

mumyhery said...

Jamani!!! Mungu awasaidie watoke salama, sijui na yule mama aliejifungulia huko chini sijui anaedeleaje na mwanae