Friday, October 1, 2010

Them, I & Them.....GOOD THINGS.....Lucky Dube

"There will be a time in your life when you' ll need me the most
but I won' t be there."

Kwenye ukurasa wangu wa "usokitabu" niliwahi uliza NI KWANINI BINADAMU TUNAKUWA WANAFIKI hata pale ambapo tunajua ukweli ama mwisho wa tuwazacho?
Nilitoa mfano wa BIMA YA MAISHA ambayo licha ya ukweli kuwa ni BIMA YA KIFO, bado hakuna anayetaka kukubali ukweli na kuiita hivyo. Kwao ni BIMA YA MAISHA ambayo huitumii maishani bali ukifa.
Tazama sasa kwenye kile kiitwacho KUTAFUTA AMANI. Wale wenye majukumu wanaamua kujikita kuzungumzia namna ya kupata amani ilhali wanapuuza HAKI NA USAWA. Hakuna asiyejua kuwa hakuwezi kuwepo amani kama hakuna HAKI NA USAWA.
Lakini si kwenye "mauzo ya sera" pekee kunapotokea haya, hata kwenye maisha yetu ya kawaida twaona namna ambavyo watu wana/ tunakwepa majukumu yetu muhimu na ya lazima kuwaambia tuwapendao kuhusu ukweli wa maisha.
Ni mara chache utaweza kumuona mzazi akiongea na mwanae namna ambavyo maisha yanaweza kuwa atakapofariki. Hawawi ama hatuwi wawazi kusema namna ambavyo tungependa wale tuwapendao waishi.
Lakini hili si alilolifanya PHILIPS LUCKU DUBE ambaye amemuonya yule ambaye ampendaye akimwambia kuwa kuna wakati utakaponihitaji lakini hutaniona. Lakini anaamua kumpa usia wa maisha hivi sasa.
Msikilize hapa katika kibao hiki kifupi na kizuri alichokiita GOOD THINGS.

There will be a time in your life when you' ll need me the most
but I won' t be there.
There will be a time in your life when you won' t need me at all
But I won' t be there.
But while I' ve got the chance, I' m gonna tell you what I know
About this world we' re living in.
It may seem so beautiful from where you are
It may look so innocent in your eyes
But let me tell you , It' s not a bed of roses



Chorus: (x3)
Good things come to those
Who got out and made them happen
They don' t come to those who wait


I can sit here and teach you every trick in the book
But at the end of the day , It is your life


Chorus: (x3)
Good things come to those
Who got out and made them happen
They don' t come to those who wait


You don' t have to worry
The future is in your hands


-----till fade ------


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Halil Mnzava said...

Brother,nimeupenda ujumbe wa leo.
Ubarikiwe.

EDNA said...

Kaka umenena,ijumaa njema kwako pia.