Thursday, October 28, 2010

Utachagua kwa UTASHI, UFUASI AMA UHITAJI???

Photo: BONGO CELEBRITY.com
Umeshajiuliza utamchagua (ama kwa wasio nchini ungemchagua) nani kati ya waonekanao hapo juu kuwa rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika jumapili?
Hapa sisemi kuchagua kutokana na jina ama chama, namaanisha SIFA za mgombea.
Ama ulishajiuliza kuwa unataka kiongozi ajaye awe na utekelezaji wa lipi na lipi na awe na ILANI inayotekeleza vipi? Ama tulisubiri waje na UONGO WAO ndio tuanze kujipanga jinsi ya kukubaliana nao? Ama tulisubiri waje na pesa ndio tuangalie namna zinavyoweza kutufaa? Tulisubiri waje kutuambia matatizo yetu ilhali wao hawakai kwetu? Ama waje na takwimu njema zisizoeleza tulivyo na kisha kutuaminisha kuwa tunawahitaji wao badala ya kuhitaji suluhisho la matatizo yetu?
Je!! Ulibahatika kumuuliza yeyote maswali haya?
OMBI LA KWANZA LA BLOGU HII KWA MWANANCHI NI KWENDA KUPIGA KURA. NI HAKI YAKO NA "SAUTI" YAKO KATIKA YALE YAJAYO.Photo: BONGO CELEBRITY.com!
Na japo siku zimekaribia, bado nahisi wengi hawana majibu na hili lanipeleka kujiuliza kama
TUNACHAGUA VIONGOZI WETU KWA UTASHI AMA UHITAJI?
Tuwasikilize Morgan Heritage wanavyozungumza kuhusu wanasiasa katika wimbo wao POLITICIANS wanapouliza "why should we trust in politicians and why should we vote every election? When there is no place for WE, you and me, in their "secret-society" they call us MINORITY"
. I CALL THESE PEOPLE....... POLI-CHEAT-EANS

Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

2 comments:

Simon Kitururu said...

Nahisi yoyote apigaye kura atachagua kwa UTASHi, ufuasi na UHITAJI.

Kwa kuwa nawasiwasi kila mtu anautashi hata kama hukubaliani nao.


Na nawasiwasi kama umpigiaye kura ni KIONGOZI hata ukane una kaufuasi.:-(

Na haki ya nani kama FISADI bado unauhitaji hata wa kuhakikisha mambo yaendelee hivyohivyo ili UFISADI na kama masikini ya julikana una UHITAJI.:-(


Nawaza tu kwa sauti!

emu-three said...

Mhh, mimi nitachagua kwa nini vile? Ooops, kiukweli nilishajua nani wa kumchagua hata kabla ya kampeni, ingawaje wale nisio na utashi nao, ooh, nisiwahitaji...oh...lakini mimi sio mfuasi wa chama chochote, nachagua kwa nilivyofanya uchunguzi wangu...mkweli na mnafiki utamjua mapema!