Ni zaidi ya maonesho.......
Ni mjumuiko wa waTanzania na utambulisho wa ujasiriamali wa waTanzania, kwa waTanzania.
Usiku wa kuamkia leo, kulikuwa na kile ambacho kilitajwa kama uzinduzi rasmi wa BLOGU YA VIJIMAMBO uliofanyika katika ukumbi wa Mirage Hall mjini Hyattsville, jimbo la Maryland Marekani. Hii ni blogu changa lakini inayofanya vema saana ambayo inamilikiwa na Dj Luke Joe. Blogu hii ambayo ilianza Januari 31 mwaka huu, iliandaa uzinduzi wake rasmi ambapo mgeni wa heshima alikuwa ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar na pia ilihusisha "maonesho" na maelezo ya bidhaa toka kwa wadau wahusikao na jamii ya waTanzania hapa nchini (kama Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika), mwanamitindo maarufu nchini Tanzania mama Asia Idarous na wajasiriamali wengi sana waTanzania wafanyao shughuli zao hapa nchini.Mara baada ya kuwasili ukumbini. Balozi Maajar alipata nafasi ya kutembelea meza zote za maonesho na maelezo na kuchukua mawasiliano ya wajasiriamali hao, huku akisisitiza kuwaunganisha katika mtandao mmoja kupitia ubalozi katika kufanikisha lengo lao.Baadae alihutubia mjumuiko huo mkubwa wa waTanzania na wadau wa Tanzania na kuizindua rasmi blogu ya Vijimambo kama asikikavyo na kuonekana kwenye video hii ambapo mbali na mambo mengine, Balozi Maajar
1: Aliahidi kuweka ukurasa wa kutangaza kazi za wajasiriamali waTanzania waishio hapa Marekani.
2: Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya waTanzania kama njia pekee na kuu ya mafanikio 3: Alieleza umuhimu wa mitandao ya kisasa kama blogu
4: Alitoa ushauri kwa Dj Luke (ambao kwangu ni ushauri kwa bloggers wote)
Na hizi chini ni taswira mbalimbali zilizonaswa na camera ya CHANGAMOTO YETU zikimuonesha Balozi Maajar akipitia meza za maonesho na maelezo ya wadau mbalimbali waTanzania waliopo hapa.
Kisha ukaja wasaa wa maonesho ya mitindo ya mavazi ya mbunifu Asia
MUHIMU::PICHA ZOTE MALI YA CHANGAMOTOYETU BLOG
5 comments:
Asante kwa taarifa.
Meza ya "Changamoto Yetu" iko wapi? Mbona zile tisheti za "The Way you see the Problem is the Problem" sizioni?
Mmmh!
Mzee wa Changamoto, taarifa yako hii ni nzuri sana. Imenifungua macho. Kumbe waBongo wa upande wenu huo wanajituma katika ujasiriamli namna hiyo. Safi sana.
Nampa hongera sana DJ Luke. Ameonyesha mfano wa kuigwa, kuwakusanya watu namna hiyo kushiriki katika shughuli murua namna hii.
Hao wanaouza vitu vya nyumbani wanafanya kazi nzuri na muhimu sana, maana ni njia ya kuongeza ajira kule nyumbani na kuingiza kipato kwa Taifa. Kinachohitajika tu ni kumpata mtu atakayewadhibiti mafisadi, ili wakome kuchota hivi vijisenti.
Hongera kwa kazi nzuri, ilipendeza sana, picha nzuri sana, hongereni wana-blog
TWASHUKURU KWA KUTUPA TUKIO HILO MUHIMU! Kweli imetufumbua macho ingawaje bado sisi `bongo-blogs' inakuwa kama `window shopping', wakati wenzetu ni sehemu ya biashara! Oh, sijui tu(ni) fanyeje!
Post a Comment