Wednesday, November 10, 2010

Ujinga mkuu ni kuwa MJINGA WA UJINGA WAKO

Nafananisha "tittle" hiyo na nukuu yake Saint Jerome (374 AD - 419 AD) aliyesema "It is worse still to be ignorant of your ignorance." Hakuna ubishi kuwa kati ya vitu ambavyo hatutaki kujifunza, ama niseme kati ya vitu ambavyo ni "DONDA NDUGU" nchini Tanzania, basi ni KUTOJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA TULIYOFANYA.
Naamini kuwa ufanisi wa BUNGE na SERIKALI ya Tanzania UNADIDIMIZWA na mambo mengi ikiwemo KUTOANDALIWA KWA WATAWALA / VIONGOZI TULIONAO. Labda hata kina Mwl Nyerere hawakuandaliwa lakini walikuwa na kipaji na hata moyo na nia ya kuongoza na walikuwawaadilifu.
Tumeona namna ambavyo watu wasio na ujuzi katika SAYANSI YA SIASA, UONGOZI na hata KIPAJI CHA UONGOZI wakijiwezesha kupata nafasi na kisha kuchaguliwa kuchukua nafasi mbalimbali na hasa za UUNGE nchini mwetu, lakini kibaya zaidi ni kuwa watu hao hao wanateuliwa kushika nyadhifa kubwa ndani ya nchi yetu bila ya kuwa na kile kinachoaminika kuwa utoshelezi a nafasi wazikwaazo. Kwa maneno mengine ni kuwa HAWAANDALIWI.
Leo hii kwa kuwa siasa na hasa ubunge umekuwa "dili la uhakika / msimamo", tunaona madaktari, wauguzi, waandishi, wanamuziki, mawakili na wengine wasio katika mfumo wa siasa (na ambao pengine hawajaingia katika mfumo huo) wakiamua kuzikacha nafasi zao kwa wingi zaidi kuwahi pale palipo na pesa...BUNGENI.
Ni kweli kuwa wapo wanaokuja kuwa viongozi bora, lakini ni nani anayewafunza hawa wapya "waliovamia fani"? Ama ndio zilezile kauli za kuwa "miaka mitano ya kwanza ilikwa ni ya kujifunza"? Nilipokodolea macho RATIBA YA SHUGHULI ZA BUNGE NOVEMBA 2010 (irejee hapa) sikuona mafunzo ya awali kwa WABUNGE WAPYA. Sikuona kile ambacho wengi huita ORIENTATION kwa wabunge wapya na hata warejeao ili kujua nini cha kufanya katika kutimiza KWA UFANISI kazi waliyotumwa na wananchi wao. Matokeo yake ndio yaleyale tuliyosikia mwaka 2006 kwa Mbunge kutolewa bungeni "kutokana na kukiuka kanuni ya Bunge, kipengele cha mavazi", kanuni (ninayoionayo ya kitumwa na isiyoendana na mazingira yetu Tanzania) ihimizayo kuvaa suti na glovu. Cha kushangaza ni kuwa baada ya tukio hilo, Mbunge wa Koani, Haroub Said Masoud (CCM), aliomba mwongozo wa Spika akisema zaidi ya asilimia 50 ya wabunge katika kikao hicho walikuwa wageni, lakini (kama livyo ada yao kwa ahadi),Spika alipokea mapendekezo hayo, na kusema Katibu wa Bunge ataandaa semina hiyo. Kisha kina "anon" wakaanza kubwabwaja kumsema m'bunge huyo badala ya kuuliza ni vipi bunge lilimtegemea m'bunge huyu kijana na m'changa atambue miiko ya bunge kama hajaandaliwa? Ni vipi bunge lilitegemea yeye (na wengine) waijue mipaka / kanuni / miiko hiyo ya bunge kama hakuna anayewapa mwongozo kamili, sahihi na RASMI???ACHANA NA MAVAZI, ACHANA NA KUONDOLEWA BUNGENI.
Hivi ni WABUNGE wangapi wanaojua kuwa WAAJIRI WAO NI WANANCHI NA SIO ILANI ZA VYAMA VYAO????
Ni wabunge wangapi wanaojua kuwa katika chaguzi za majimbo yao, wamependwa ama kuchaguliwa wao kwa kuwa ni SULUHISHO la matatizo ya wananchi wao na si kwa kuwa wananchi wengi wa hapo wanapenda chama lichogombea?
Ni wangapi ambao wanatambua kuwa wao ni SAUTI HALISI YA WANANCHI na sio "ujazo' wa kura za kupitisha, kupinga ama kuadhibu kile kionwacho ndivyo ama sivyo na wanachama wa chama awakilishacho?
Ni wangapi ambao wanaamini kuwa HAWALAZIMIKI KUUNGANA NA CHAMA CHAO katika maamuzi, kama maamuzi hayo yanawakandamiza ama kutowanufaisha wananchi wao?
Ni wangapi ambao wanajua kuwa hapo ni kama SHULE na wamalizapo muhula wanatakiwa kurejea NYUMBANI walikochaguliwa wakiwa na ripoti ya matokeo ya mtihani wao wa uwakilishi?
Ni wangapi wanajua wajibu halisi wa kuwashirikisha wananchi wao kile walichojadili bungeni, kukusanya maoni ya wananchi juu ya walilojadili na kisha kurejesha pongezi ama pingamizi la baadhi ya mambo ambayo wananchi wanaona hayawafai
Nina hakika ka wabunge wengi hawatekelezi haya na hasa hili la mwisho. Na wamekuwa wakikacha hili kwa miaka nenda miaka rudi, na HUU NI UJINGA. Na kutotekeleza hili ni UJINGA WA UJINGA HUO.... Na ni hili linalosikitisha zaidi kuwa tunakuwa wajinga wa ujinga wetu.Jambo ambalo ni HATARI na ndio UJINGA MKUU.

JICHO LA NDANI ni kipengele kinachozungumzia mambo mepesi na yaliyo ndani mwetu, ambayo yakiangaliwa vema na kwa tafsiri ama tafakari njema yanaweza ama ndio suluhisho kwa matatizo yetu. Kwa matoleo yaliyopita katika kipengele hiki, BOFYA HAPA

3 comments:

emu-three said...

Hili ni tatizo kubwa hapa kwetu, kutaka kitu kwa nadharia, hujakijua vyema, lakini unadai unakijua. Nauliza hivi unaweza kuwa dakitari bila kuusomea huo udakitari? sasa kwanini katika nyanja nyingine, hasa hizi za siasa, uongozi watu wanachukulia juu kwa juu kuwa ianwezekana hata kama hukuiendea shule!
Ngazi ya kama `uspika' bungeni ni ngazi nyeti, na hapa ilitakiwa zana ya usiasa iondolewe ili awekwe mtu ambaye kweli `anaiweza' kweli hana `uchama au ubaguzi au aina yoyote itakayoligawa bunge!
Mchakato kama huo kwangu mimi ulihitaji muda! sijui labda ni kazi rahisi kuliko mimi ninavyodhania!
Labda...na hii labda ndio hiyo tunawapata viongozi ilimradi ni chama changu
Ahsante kwa mada hii

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa mada hii natafakari nitarudi tena.

Yasinta Ngonyani said...

nanukuu "Hakuna ubishi kuwa kati ya vitu ambavyo hatutaki kujifunza, ama niseme kati ya vitu ambavyo ni "DONDA NDUGU" nchini Tanzania, basi ni KUTOJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA TULIYOFANYA." mwisho wa kunukuu:- Watanzania tu-watu wa ajabu sana mambo mengine yasiyo na maana ni rahisi sana kuiga lakini ukija kwenye mambo mahimu hapo ni bado kabisa tumejifunga hatujafunguka sijui kwanini?