Saturday, November 20, 2010

WALIOGOMEA MIDAHALO....Wengi wao ama wana UJINGA, ama wamejawa DHARAU

ONYO: USISOME HAPA KAMA
1: WAKASIRIKA KABLA YA KUFIKIRI
2: UNAAMUA KISHA UNAFIKIRIA ATHARI
3: HUPENDI KUJUA UKWELI HATA KAMA UKWELI NDIO UPENDO

"Speak the truth and speak it over. Love God and leave, is my only destination." NASIO
Tafsiri ya UJINGA niliyonayo ama niliyoambiwa (na ambayo naisimamia) ni ile isemayo kuwa mjinga ni MTU ASIYEJUA, NA ANAJUA KUWA HAJUI. Kwa tafsiri hii, ina maana UJINGA ni hatua moja bora kutoka UPUMBAVU na iliyo rahisi kuirekebisha kwani aliye mjinga anaweza kurekebishika akiamua kuufanyia kazi ujinga wake.
Ina maana kwa tafsiri hii ya Ujinga, naamini kuwa wabunge wa CCM (ambao waligomea midahalo) walitambua wazi kuwa walitakiwa kueleza sera zao kwa wananchi na kuzipambanisha ili kuweza kuwapa nafasi wananchi kutambua aliye bora kwao. Lakini KWA AMRI TOKA LUMUMBA (makaoni mwa chama), tena toka kwa watu ambao hawajui mahitaji ya asilimia kubwa ya wananchi, wagombea hawa WAKAKACHA midahalo kwa kisingizio cha kuwafuata wananchi huko walipo. Suala si kuwafikia, bali ni KUWAPATIA ALIYE BORA KWA MATATIZO YAO. Na nina hakika wale WALIOOGOPA midahalo walikuwa hawajui namna ya kuwakomboa wananchi wa na walijua fika kuwa hawajui (rejea tafsiri ya ujinga) na kwa kuwa wao hawakuwa pale na hawako pale kumfaa mwananchi zaidi yao wenyewe, wakaona wafanye lililo bora kwao nalo ni kupanga mikakati ya kuchaguliwa hata kama hawatakuwa na manufaa kwa wananchi wao kama wale ambao wangepambanisha nao sera.

Kinachokera zaidi ni namna WANAVYOJIDAI kupata "ushindi wa kishindo" na kusingizia kuwa ushindi huo watokana kukubalika kwao. Hawa watu wanajisifia kufaulu bila kufanya mtihani. Ama kwa uhalisia zaidi niseme wanajivunia KUSHINDA KWA "KUTAZAMIA".
Nafarijiwa na Nasio Fontaine ambaye katika wimbo wake DANGEROUS (usikilize mwisho wa post hii) aliimba akisema "...i heard your speeches,... your empty promises (promise is a confort to a fool), but now that i know, your words are dangerous"
Lakini siamini kuwa wabunge wote wako hivyo. Siamini kama wote hawakuwa na suluhisho la matatizo ya wananchi. Siamini kuwa wote walikuwa hawapendeki. Siamini kuwa wote ni WAJINGA. Ila kwa wale wasio na sifa hizo mbaya hapo juu, na ambao wangeweza kuwadhihirishia wananchi kuwa wao ndio wanawafaa na wakaamua kutofanya hivyo basi hakuna ubishi kuwa WAMEWADHARAU WANANCHI WAO

Wameona hakuna haja ya kutekeleza haki ya kikatiba ya wananchi kwa kuwapa nafasi ya kuchuja kile waaminicho na wafikiriacho ukilinganisha na wenzao. Hii si dharau kwa wananchi tu, bali kwa nchi.
Na kama nilivyoonya hapo awali, usisome hapa kama huna KIFUA cha kuukubali ukweli. Na huu ni ukweli toka katika upande wa wahitaji, upande wa wasio na tumaini na upande ambao ulikuwa na imani na watawala hawa. Kama alivyosema Lucky Dube kwenye wimbo wa SOLDIRES FOR RIGHTEOUSNESS kuwa "We are the soldiers for righteousness. And we are not sent here by the politicians you drink with. We' re sent by the poor. We' re sent by the suffering. We' re sent by the oppressed"
Ni ukweli huo ambao twauona na kuusimamia sasa. Ni wakati wa kuwawajibisha waheshimiwa mliongia madarakani na naamini hakuna ubishi kuwa KWA KILA JEMA MTAKALOTENDA TUTAWAPONGEZA NA KWA KILA BAYA MTAKALOTENDA TUTAWAKOSOA. Kama isemavyo fulana hii hapa chini, tunasimama katika kilicho sahihi na si kuendekeza "mapinduzi" ya wasiojua uhitaji wa wahitaji wao.
Labda niwe wazi kuwa, sasa ni wakati ambao tutaanza KUWEKANA SAWA na kurekebishana hasa katika kipengele (label) hii ya POLITICS FIX (kama ambavyo nataraji mnirekebishe) na hii itakuwa ni njia moja muafaka na muhimu katika kulikomboa taifa.
Na kwa WABUNGE VIJANA, wale wapya ambao mlionekana kuwa na "UJANA WA MAWAZO" mtambue kuwa kuwepo kwenu hapo kumekuwa tumaini kubwa kwa wengi, kwa hiyo kushindwa kuwakilisha vema na kujikuta mnaingia katika "MFUMO WA UZEE WA MAWAZO" ULIOWACHOSHA WANANCHI mtajishushia imani kwao. Japo wapo ambao mmeshaanza hilo.
Mfano mzuri ni mwanablogu ninayeheshimu kazi zake aliyegeuka kuwa m'bunge Dr Faustine wa Faustine Baraza ambaye sasa ni m'bunge wa Kigamboni, alikuwa mkosoaji mkubwa wa matendo ya serikali na chama, aliandika kuhusu ziara za Rais na mambo mbalimbali, lakini alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge akaamua kuifunga blogu ambayo aliitumia kuanika uozo wa "WENZAKE WA SASA." Ukurasa wake huu hapa ulio na kumbukumbu za aliyokuwa akiyasema akiwa nje sasa umewekewa KUFULI. Nilipomuuliza katika ukurasa wake wa Facebook alinijibu kuwa alikuwa amebanwa na mambo ya kampeni lakini angeurejesha hewani punde. HAKUTIMIZA AHADI YAKE. Sasa kafungua ukurasa mpya ambao naamini utaendana na matakwa ya watawala wake kuliko wananchi aliokuwa akiwatetea kwa dhati.
NI WAKATI WA KUWEKA MBELE MASLAHI YA WANANCHI NA SI CHAMA
Tumsikilize Nasio akitukumbusha kuwa THEIR WORDS ARE
DANGEROUS

NA HIVI NDIVYO NIONAVYO TATIZO. NAMI NATUNZA HAKI YA KUKOSEA NA KUKOSOLEWA.LABDA NAMNA NIONAVYO TATIZO NDILO TATIZO

2 comments:

Jeff Msangi said...

Well said Mubelwa.Tatizo la viongozi wetu ni kila kukicha kuendelea kufanya mambo kwa mazoea...business as usual.Ndio maana hata kwenye hotuba bado unasikia maneno kama amani na utulivu,ushindi wa kishindo nk.Kuna kuchelewa kusoma alama za nyakati bado.

SN said...

Wazee, nimerudi "mjini"!

Naona Mubelwa umeamkia nilipoamkia mimi. Sasa, bado una imani na 'system' au tuendelee kuamini tutafanikiwa; kama sio sisi basi watoto wetu wataendelea na harakati?

Hiyo 'muvu' ya Mbunge wa Kigamboni hata mimi ilinishtua. Msela wetu tulikuwa tunapigana vikumbo kuipa Serikali mawazo 'mbadala', lakini ndio shughuli zimembana mno. Yaani jamaa tayari yuko 'bize' kuliko Zitto et al?

Mzee, nasubiri 2015 kwa hamu! Na katika kipindi hiki chote tutakuwa tunaendelea kuwapa wahusika mawazo 'mbadala'.