Monday, December 27, 2010

Mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa Balozi wa Tanzania

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar

Nawakaribisha watanzania wote waishio Washington DC Metro(DMV) katika mkutano wangu wa kwanza rasmi na watanzania.
Madhumuni ya mkutano huo yatakuwa yafuatayo:-
(i) Balozi kujitambulisha rasmi kwa Watanzania washio katika eneo la Washington DC Metro.
(ii) Kuchagua na kuunda kamati ya muda itakayoandaa katiba mpya ya jumuiya na hatimaye kuitisha na kusimamia uchaguzi mkuu wa Jumuiya mpya ya watanzania waishio Washington DC Metro.
(iii) Masuala mengineyo muhimu yatakayojitokeza yanayohusu watanzania waishio hapa Washington DC Metro.

TAREHE:
Januari 29, 2011
MAHALI:
Hollywood Ballroom - 2126 Industrial Pkwy, Silver Spring-MD 20906
(Sehemu ya maegesho ipo yakutosha)
MUDA:
Saa 10.30 jioni (Tafadhali zingatia muda)

Ili kukamilisha maandalizi ya mkutano huo, unaombwa kujiandikisha Ubalozini kwa kuandika jina lako kwenye "kiungo" hapo chini.Sehemu hiyo ni salama(secure)na taarifa zako zitalindwa.
Maelezo yako ni kwa lengo la kufanikisha mkutano huo nakujenga takwimu kuhusu Diaspora ya Watanzania. Taarifa zote zitahifadhiwa kwa siri.
Ahsanteni.
Mwanaidi Sinare Maajar
BALOZI
BOFYA HAPA ILI KUJIANDIKISHA KUHUDHURIA.

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Safi sana. Ni mwanzo mzuri kwa Balozi wetu mpya. Natumaini pia kutakuwa na utaratibu hata wa sisi Watanzania tulioko huku mbali kuweza kujiandikisha na kutambuliwa kwamba nasi tupo. Ni vizuri kuwa na data kamili kuhusu idadi ya Watanzania walioko huku kwani hii itarahisisha mawasiliano wakati wa dharura na harakati zingine kama vile michango n.k. Mzee wa Changamoto, nenda ukaniwakilishe mimi binafsi huko mkutanoni. Mungu Aendelee kuibariki nchi yetu nzuri!

Mzee wa Changamoto said...

Naam mwalimu. Ntakuwakilisha vema. Ninalowaza ni kama kuna swali lolote ambalo unapenda nimuulize Mheshimiwa Balozi (naamini muda ukiruhusu atanipa nafasi ya kuuliza maswali baada ya mkutano)
Kama unalo basi nitalisilisha vema
Asante kwa kuendelea kuwa SHABIKI NA MHITAJI wa UMOJA BAINA YETU