Saturday, December 25, 2010

PRIDE FM Live....Zawadi yangu ya NOEL

Ndio nimekuwa "nikilia" saana kusikiliza radio za nyumbani. Na nimekuwa shabiki mkubwa wa kusaka na kutangaza radio za Tanzania zitangazazo moja kwa moja
Na leo nilipopata salaam za krismasi toka kwa Kaka Ramadhani Lutambi wa Pride Fm nikakuta maelezo ya kuiskiliza MOJA KWA MOJA. Nami nikayafuata na sasa KRISMASI yangu inanogeshwa nao.
Jiunge nao kwenye mtandao hapa http://www.878pridefm.com/index.html ama kusikiliza live kwa kwenda hapa http://www.streamfinder.com/internet-radio-station/26969/pride-fm-radio/ kisha bofya MP3 LISTEN ama unaweza ku-double click anwani http://208.43.81.168:8874/stream?.wma ambayo itafungua Windows Media Player na kukuunganisha live.
Mara nyingine hufungua ki-windows kuuliza kuhusu "local server" nawe wa-click Yes na you're good to go

Asante kwa wana PRIDE FM kwa kutujali tulio mbali. Baraka kwenu nyote

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli ni zawadi nzuri kwa walio mbali. Asanteni sana.

Jeff Msangi said...

Kaka,
Asante kwa habari hii.Kama alivyosema Da Yasinta,ni habari njema.Upweke wa ughaibuni hususani nyakati za sikukuu huwa ni mkubwa sana na vitu kama hivi bila shaka husaidia kupunguza upweke.

Jambo moja tu;hivi kwanini wameiita hii station "Pride"?Ni jina tu au ina husiana na "pride" ya nchi za magharibi ambayo mara nyingi humaanisha wale ambao wameamua kwa makusudi kwenda tofauti na maamuzi ya Muumba kwa upande wa jinsia?