Rais Laurent Gbabgo (kulia) na Rais Alassane Quattara. Wote maraisi wa Ivory Coast
Photo credit:theage.com.au
Kama kuna mambo yanayoendelea kuchukua nafasi ya juu katika habari za kimataifa ni mchakato unaoendelea nchini Ivory Coast.
Bado nchi hiyo ambayo ikingali inauguza vidonda vya vita vya wenyewe kwa wenyewe, sasa hivi wale waliogombea kinyang'anyiro cha marudiano cha uraisi wameendelea kujitangaza kuwa washindi na kuendelea kupanga mikakati ya kusonga mbele na serikali zao. Rais Laurent Gbabgo na mpinzani wake Alassane Ouattara wote wamekula kiapo kama maRaisi wa nchi hiyo na kila mmoja yuko kwenye harakati za kuanza "kuitumikia nchi". Hawa wote wamesema wanataka KUIJENGA nchi kwa umoja na upendo ambao haujaonekana wakati wa kuisaka nafasi ya kuijenga nchi hiyo.
Hivi ni vipi tunaweza KUIJALI NCHI iwapo hatuwezi kukaa chini kutambua uhalali wa aliyeshinda? Iweje kila mmoja awe mshindi wa zaidi ya nusu ya kura katika uchaguzi mmoja? NCHI MOJA INAKUWA NA VYOMBO VIWILI VIKUU VYA MAAMUZI YA UCHAGUZI AMBAVYO VINAPINGANA JAPO VYOTE VYAAMINI NI HALALI. Nchini Ivory Coast, kuna Baraza la Katiba na Tume ya Uchaguzi. Baraza la Katiba linaloongozwa na mshirika wa karibu wa Rais Gbabgo limemtangaza kuwa mshindi ilhali Tume ya Uchaguzi imemtangaza Quattara kuwa mshindi. NA WOTE WAMEKULA KIAPO CHA KUONGOZA NCHI.
Nawaza...
Ni nchi gani waipendayo?
Ni upendo gani walionao kwa nchi ambao hawawezi kuuonesha baina yao?
Wanasema vipi kuwa watajenga nchi moja na imara iwapo wao hawana umoja baina yao?
Ndipo ninaporejea kwenye swali la Nasio kuwa "WHERE WE BELONG"?
Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa Luis Marino Ocampo alipokuwa Nairobi Kenya. Anaonekana akiwa na Rais Mwai Kibaki (kulia) na Waziri Mkuu Raila Odinga (kushoto)
Photo Credit:CNN.com
Nako Kenya tumesikia kuwa washukiwa wakuu wa vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu uliopita wametajwa. Lakini kutajwa huko kumekuja na "gharama tarajiwa" ambapo Kenya ijayo yaonekana kuanza kusukwa na mkanganyiko wa nani wa kuwajibika na kuwawajibisha watu hawa? Ni serikali ama mahakama ya kimataifa? Na pia suala la "mchezo mchafu" katika kuzuia baadhi ya watarajiwa kugombea mwaka 2012
Kinachoshitua ni namna ambavyo majina haya yameleta kuungwa mkono na kupingwa.
Lakini maswali ni yaleyale...
KWANINI UKOROFI NA HUJUMA HIZI ZIFANYWE NA WAAFRIKA WENZETU?
WANAWAZA NINI WATENDAPO HAYA?
WANALIWAZA VIPI BARA HILI NA WATU WAKE?
Kwa kuwa ni Ijumaa....wacha turejeshe burudani, mafunzo na ukombozi wa kiakili katika muziki wa Reggae kwa kuungana naye Nasio Fontaine katika kibao hiki anachouliza kuhusu AFRIKA, waAFRIKA na uAFRIKA... Ameiba ki-Afrika katika kibao hiki WHERE WE BELONG
Intro....
African (Zulu)
Vocal riffs (ancenstral callings)
Dae Dn, Dae-e-yeah! Yeaheh!
Long live Ithiopia
Oh ho uuh!!!
Blackaman, Blackman
Where is your country?
Where is your King?
Ho! Ho! Ho! Where is your Nation?
Where is your GOD?
Chorus
You fe look upon land Ithiopia,
Where we belong?
You fe look upon the land of Nubia,
Where we belong?
You fe look upon the land of Africa,
Where we belong?
You fe look upon land of Ithiopia
Where, where we belong?
Who uuhh!
Blackaman, Blackman
There is NO JUSTICE,
BLIND MAN AND ALL CAN TELL YA
There is NO PEACE
Hoh! Hoh! Hoh!
There is NO FREEDOM
While LIVING IN CAPTIVITY,
So don't mek (let) them fool ya
Chorus
You fe look upon land Ithiopia,
Where we belong?
You fe look upon the land of Nubia,
Where we belong?
You fe look upon the land of Africa,
Where, where, where, we belong?
You fe look upon land of Ithiopia
Where, where we belong?
Blackaman, Blackman
Where is your country?
Where is your King?
Ho! Ho! Ho! Where is your Nation?
Where is your GOD?
Chorus x4
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
ni kweli wanaipenda nchi yao na wananchi wao
Ijumaa njema Mheshimiwa!
Kamala una uhakika?
Kuna tatizo kubwa kwa viongozi wa Afrika na pengine ni katika kujaribu kutimiza matakwa ya wakubwa wa nje waliowaweka madarakani, wakubwa wanaogharamia majeshi na silaha, wakubwa wanaogharamia kampeni za gharama kubwa wakati wa uchaguzi, wakubwa wanaomwaga mamilioni ya dola kila mwaka kwa lengo la kumiliki utajiri wa bara hili lililojishona katika paradoksi ya kuwa bara tajiri sana lakini masikini sana pia.
Wikiendi njema huko Maryland. Natumaini barafu kidogo imeachia.
Post a Comment