Monday, January 31, 2011

Yaliyonenwa katika mkutano wa Mhe. Balozi na waTanzania wa Washington DC

Balozi Maajar akizungumza na umati wa waTanzania uliohudhuria mkutano huo
Jumamosi ya Jan 29, 2011, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar, alikutana na waTanzania kwa ajenda kuu mbili. Kwanza ni kujitambulisha rasmi na pili, kushuhudia kuundwa kwa kamati ya muda itakayoshughulikia upatikanaji wa Katiba mpya ya Jumuiya hiyo. Baada ya kujitambulisha, Mhe Balozi alishuhudia kupatikana kwa kamati hiyo ambayo imepewa miezi miwili (na wajumbe wa mkutano) kuwa na rasimu ya katiba. Zifuatazo ni hotuba zilizotolea siku hiyo. Kwanza ni hotuba kamili ya Balozi Mwanaidi Maajar kwa wanaJumuiya ya waTanzania waishio maeneo ya WASHINTON DC.
Amegusia mambo ambayo yanaifaa jamii nzima ya Tanzania kwenye DIASPORA na mengi aliyozungumzia si kwa watu wa DC METRO tu, bali popote walipo.
Amegusia pia SUALA LA URAIA WA NCHI MBILI. Msikilize

Baada ya hotuba ulifuata uchaguzi wa Kamati ya kuandaa katiba itakayotumika kuchagua viongozi wa, na kuongoza JUMUIYA YA WATANZANIA HAPA DC.
Kamati iliyoteuliwa kuanya kazi hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo akitoa hotuba fupi kwa niaba ya kamati. Hotuba hiyo kamili hii hapa chini.

Baada ya hotuba hiyo, Mhe Balozi naye alikuwa na neno kwa kamati hiyo kuhusu nafasi ya kukutana na vitendea kazi katika Ubalozi.Hotuba aliyoitoa ni hii hapa chini

Sehemu ya umati uliohudhuria mkutano huo.

7 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Asante sana kwa taarifa. Huyu Mh. Balozi anaonekana yuko tofauti na watangulizi wake ambao hatukuwahi hata kuwasikia. Tunahitaji kumuunga mkono na kumpa ushirikiano wetu wa dhati.

Unknown said...

wengi wa mabalozi waliopita walikalia majungu na kuwagawa watu huku wakifanya pati hewa na kudai maelfu ya dola kutoka serikalini...

Unknown said...

Sijui, lakini labda...ni mwanzo mzuri japo inatia moyo kwamba si kila kiongozi ama alie na nafasi anafaa kuongoza.

Yaliyopita si...tugange yajayo maana kuna fundisho kwa kila udhaifu.

Emmanuel said...

Suala hapa ni jinsi gani pia watz wa hapa tutamshape huyu mama katika mwanzo wa kazi yake. Tanzania ya leo na ya baadaye inahitaji kuanza upya mikakati yote ya maendeleo, kijamii na kisiasa. Kama ataelewa hili kama alivyosema na watu wakaacha siasa pembeni na kufanya majukumu ya msingi tutafika

malkiory said...

Nasikitika huyu mama ameungana na Nyalandu kwa kauli yake ya kusema watanzania hulalamika kwenye blogs. Hii kauli imekaa kisiasa mno,pamoja na mazuri yake ninachokijua mimi ni kwamba huyu mama pamoja na Kalaghe wa Uingereza wanabebwa sana na vyombo vya habari,hasa blogs kama ile ya jamii kulinganisha na mabalozi wengine.

Sasa hii habari ya watu kulalamika kwenye blogs anaitoa wapi? hajui uhuru wa vyombo vya habari? haujui kuhusu haki na uhuru wa kusema na kuandika!

emu-three said...

Twashukuru kwa taarifa hii

malkiory said...

Nilisoma kichwa cha habari balozi wa JK chanzo cha kuvurunda Dowans. Tembelea linki hii na ujionee kuwa huyu mama si mwema:http://4.bp.blogspot.com/_1fXMXYztr0w/TVAZBfUIT6I/AAAAAAAAhuk/LiNIOXjoN2Y/s1600/msela1.jpg