Wednesday, February 23, 2011

Kizazi...Nini kipimo chake? Wakati, Mazingira ama Nyenzo?

Photo Credits: Jack Graham Blog
Labda wapo wanaoshangaa kuwa mtu na mzazi wake wanahesabika kuwa watu wa vizazi tofauti licha ya kwamba wote wako hai.
Wengine wanakubali kuwa wao na wazazi na wazazi wa wazazi wao ni vizazi tofauti licha ya kwamba wote wako hai.
Lakini wapo ambao pengine bila kufikiria wanaamini kuwa kila UZAO ni KIZAZI.
Na pia wapo ambao wanaamini kuwa yachukua miaka mingi kutoweka kwa kizazi kimoja kwenda kingine.
Kwani kila siku si tunasikia muziki huu wa "bongo flava" ukiitwa muziki wa kizazi kipya? Hata kama anayeuimba amevutiwa na muziki miaka michache iliyopita baada ya kumsikiliza "mkongwe" ambaye (kwa tafsiri "yao") si mtu wa kizazi chao?
Hujasikia wasanii wakirudia nyimbo za miaka kadhaa iliyopita na kusema wamezirudia katika MUZIKI WA KIZAZI kipya katika harakati za kutenga kizazi cha "remix" na MUZIKI HALISI?
ACHANA NA HAYA....
Juzi tukiwa shuleni katika kujadili KIJANA NA TEKNOLOJIA, binti mmoja akasimama na kuchangia akisema "maisha yangu yote sasa ni elektroniki. Ndio kalenda, kumbukumbu, miadi, barua, simu, sauti nk. Vyote nafanya kwenye simu yangu ya Iphone." Hapo mie nikawa natikisa kichwa kukubaliana naye. Kisha akasema KWA KIZAZI CHA SASA HUWEZI KUISHI BILA NYENZO KAMA IPHONE.
Hapoooooooooooooooo sasa....Sikusubiri "kunyoosha mkono"
Nikamuuliza kuwa anaamini kuwa kila pembe na mtu / kijana wa rika yake anaijua Iphone achilia mbali simu hata ya kukoroga?
Nikamuuliza anaposema KIZAZI CHA SASA anamaanisha katika nyumba, kijiji, mkoa ama jimbo analoishi ama anamaanisha ULIMWENGU MZIMA?Ni kweli kuwa binti huyu wa miaka 18 wa hapa Maryland yupo kwenye kizazi tofauti na binti ya jirani yetu mwenye miaka 18 pale Bushasha? Kama wana umri sawa, si wako kizazi kimoja? Lakini kama hawatumii nyenzo moja kutokana na mazingira, ina maana mazingira ni kigezo? Na je, ni kweli kuwa "Uncle" nanilii anayetumia kompyuta saana pale Bongo atakuwa katika kizazi sawa na haka kabinti ka hapa kwa kuwa nyenzo zainawaweka kwenye "usawa" wa matumizi?
Ndipo nilipopata wazo la kuja kuuliza hapa kwamba KIZAZI....KIPIMO CHAKE NI NINI? NI WAKATI, MAZINGIRA, AMA NYENZO?Labda nikuonyeshe tu kuwa.....................Hawa hapa chini
Photo Credits: Broadcasting Corporation of China
Ni wanafunzi wa elimu ya awali kama ilivyo kwa hawa hapa chini.
JE!! Japo wanaweza kuwa na umri unaolingana ama kukaribiana, unaamini wako katika KIZAZI KIMOJA?Kwani kizazi ni nini?
Innocent Galinoma aliuliza "what is life? Is life a gift, or a test, or a punishment for my people?"
MSIKILIZE

JUST THINKING OUT LOUD.

3 comments:

emu-three said...

Kwangu mimi kizazi ni mabadiliko yote, ya muda, mazingira na watu wenyewe!
Kipimo chake ni kuwa muda fulani umeisha, miaka kadhaa, na wametoka kwa babu hadi mjukuu,au sio hicho ni kizazi.
Kizazi cha babu redio ilikuwa ndio kitu babu kubwa sasa mmmh, computa nk...mabadiliko ya mazingira na teke-linalokujia! Y
Ni hayo tu mkuu, naandika harakaharaka maana nipo kwenye computa ya mutu, bosi habanduki mezani kwangu!

Rachel Siwa said...

kwangu mimi kizazi kitabaki kuwa kizazi,basi kuna mabadiliko ya maendeleo kati ya vizazi vya sasa na vyazamani kulingana na wakati!.

ngoja niishie hapa na nipo pamoja kuendelea kujifunza zaidi!.

Goodman Manyanya Phiri said...

Mandhari nzuri sana uliyechagua, Mkuu, pia na kunikaribisha naamini ninavyopiga hodi kwenye blogu yako. Leo ndio mara ya kwanza nimeingia "The Way You See The Problem..."


Ni ukweli kabisa kwamba karni hii bado wapo binadamu wenzetu wanaoishi "katika" karni mbili au tatu zilizopita ukizingatia suala la nyenzo.


Pamoja na ile hali yao kama ile ya watu wazamani, hatuwezi lakini 'kuwafukuza' kwa kudai eti wao siyo wa kizazi chetu.


Ingawaje hawana nyenzo kama yule mwanafunzi mwenye IPHONE, nao wanafaidi kwa namna moja au yingine kutokana na maendeleo ya ulimwengu wa kisasa kiteknolojia.


Mfano, mwaka huu wa 2011, yakitokea mafuriko katika sehemu yao, ndege au HELICOPTER labda yenye AUTOPILOT inaweza kupelekwa huko kwao kuwakomboa, kitu ambacho kisingewezekana enzi za mwaka 1711!


Nje ya tundu. Jana nilishangazwa na Mama-mtoto niliporudi kazini naye kuniambia mama (umri 70) tuliepanga nyumbani kwake hapa Atteridgeville Pretoria alikulia kwenye mazingira ya kutisha au kushangaza kiasi kwamba alianza kuona nyanya akiwa na umri wa miaka 40!

Mkate, kwa kuadimika, walikuwa hawali kabisa isipokuwa kwa siku ya CHRISTMAS (25 Dec) tu kila mwaka ikiwa sasa kama kitamu (A TREAT) naye anajigamba alikuwa kila CHRISTMAS hiyo mkate mzima (A WHOLE LOAF)anaubomoa nakuumaliza kabisa akiwa peke yake!


Huyo basi ndio kizazi chake mama-yangu-mzazi aliyekuwa kwenye umri huohuo wa 40 amekwisha choka na nyanya nyingi na kuwa mtumiaji wa TOMATO SAUCE badala ya nyanya kavu!


Kwa maoni yangu, "kizazi" maana yake ni wale watu waliokuwa kama mifano ya kuigwa kwa wakati huo, watu wanaojulikana kama TRENDSETTERS, ROLE MODELS ETC. (au watu wenye uwezo fulani ki wastani)