Monday, February 21, 2011

Namba moja na Mbili zangu...Si "REMIX"

Ndioooo...Enzi zetu za UZEE WA UJANA....Yaani ni "Enzi zijazo". Upo hapo????
Sina hakika kama ni sahihi kwa wimbo unaorudiwa "UPYA"na msanii kuitwa REMIX, lakini ninafurahi kuona baadhi ya wasanii wana uwezo wa kutunga huku wakiona mbali kwa kuweka MUENDELEZO wa nyimbo zao.
Ni jumatatu, ambapo mara nyingi huwa tunapata nyimbo za kale kuhusiana na maisha ya sasa. Lakini kwa siku ya leo, naomba nikushirikishe nyimbo kadhaa (ambazo zaweza kutokuwa za kale sana) lakini zenye muendelezo mwema wa "hadithi" inayoimbwa.
Na hizi si nyimbo pekee zenye muendelezo, lakini ndizo nilizoona vema kushiriki nanyi.
Tunanze na Vijana Jazz Band.
Katika wimbo wao PENZI HALIGAWANYIKI (sehemu ya kwanza) wanazungumzia RUHUSA aliyopata Mume kuoa mke wa pili, lakini anaonekana kuvunja ahadi hiyo na kuhamishia penzi lote kwa mke wa pili. SIKILIZA

Katika sehemu ya pili, wanaimba juu ya muonekano mpya alionao mke aliyeachwa kiasi cha kutamaniwa na mume wa zamani.
SIKILIZA

Kisha tuhamie kwa ROGATI HEGGA almaarufu kama KATAPILA

katika wimbo FADHILA KWA WAZAZI aliimba sehemu ya kwanza akizungumzia NIA YA KUWALEA WAZAZI.
MSIKILIZE

Lakini kwa bahati mbaya, wazazi hao wakafariki kabla hajatimiza nia hiyo. MSIKILIZE

Na mwisho tumsikilize MUUMINI MWINJUMA
ambaye akiwa na African Revolution na Double M Sound alitoa wimbo wa Mgumba sehemu ya kwanza na ya pili.
Sehemu ya kwanza ilikuwa ni kuhusu kukosa mwana kwa mwanamama huyu, MSIKILIZE

Na sehemu ya pili ilikuwa ni matokeo ya "nani alikuwa mgumba kati ya mume na mke"
MSIKILIZE

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

7 comments:

Simon Kitururu said...

Hivi kweli kuna muziki wa kale kama ni muziki tuusikilizao sasa?

Hivi jana sio zamani?

Nawaza tu kwa sauti!:-(

Yasinta Ngonyani said...

nimefurahi maana hii miziki ni ya kale lakini ukiisikiliza sasa ni mitamu muno. Simon nawe!!!

malkiory said...

Mubelwa: Asante kwa hizi rekodi, hasa kibao cha ya penzi haligawanyiki imenikumbusha mbali enzi za marehemu Eddy Sheggy. Huyu bwana sauti yake ni nadra sana kuonekana katika ulimwengu wa sasa wa muziki.

Anonymous said...

yani kaka umenipa raha ndani ya roho kwa Vijana jazz wanapamba moto.sio mchezo penzi haligawanyiki.miziki ya sasa kazi kufagilia majina ya watu tuu.
Mwanawane Ubarikiwe.....Shazy

emu-three said...

Raha, raha sana ukisikiliza miziki iliyopigwa enzi hizo, na inakukumbusha mahala au tukio fulani...mmh , ni juzi juzi tu, leo tunaiita miziki ya zamani, ama kweli umri unakwenda!
Mkuu nashukuru sana kwa kunipigia debe wadau mbalimbali kuja kunitembelea kwenye blog yetu ya `diary yangu', Ahsante sana!

Rachel Siwa said...

kaka Mubelwa asante sana kwa burudani mwanana,yaani ukisikiliza nyimbo za zamani kunakitu unakumbushia kwa wakati huo!!!!!!
kaka nawe mmoja wa wanamuziki wasio vuma lakini wamo!!!!!!

Mija Shija Sayi said...

Vijana jazz imenikumbusha mbali sana mwenzenu.. imenikumbusha Redio Tanzania na vipindi vya mchana mwema, chaguo la msikilizaji na jioni njema, enzi hizo Mwanza yaani siamini kama yale maisha ndiyo hadithi tena...

Halafu Katapila na Mwinjuma wamenikumbusha Bonanza la Readers.. Yaani wee acha tuu!

Asante mzee wa Changamoto kwa kunitengenezea siku yangu.