Monday, March 7, 2011

Za kale vs Maisha ya Sasa.....MASAFA MAREFU

TABORA
NAMANGA
BUKOBA
Naamini sote tunaweza kuangalia picha zetu za namna ambavyo tulikuwa tukisafiri miaka kumi na tano ama iliyopita na namna ambavyo maisha ya safari wakati ule yalivyokuwa na kutofautisha na sasa. tofauti ni kubwa.
Binafs wacha nizungumzie safari nefu ambazo nilikuwa nikisafiri. Safari nilizo na uzoefu nazo na ninazozikumbuka vema na ambazo nikilinganisha na sasa naona mabadiliko. Nakumbuka safari ya Dar-Mwanza kwa terni ilivyokuwa na namna ambavyo ilikuwa ikiandaliwa, amaa kweli. na kufika Mwanza ni kuingia kwenye meli kisha mpaka Bukoba (ambako ndiko asili yetu). Kwa siku hizo kadhaa mnazokuwa safarini, hakukuwa na mawasiliano ya karibu. Kumbuka ni kabla ya kuenea kwa simu za viganjani na sasa simu za kisasa mabazo zinaweza kukufanya uwe na mtu aliye mbali kama vile mko "beneti".
Nyakati za zamani kidogoilikuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kusafiri kwa mwezi mzima na kwa muda wote huo anakuwa hana mawasiliano na familia yake ama na watu aliowaacha nyuma. ilikuwa kawaida na watu hawakuona kama ni mapungufu. WALIYAKUBALI MAZINGIRA.
Leo hii ni jambo la kawaida kwa mtu kujua fulani yuko wapi kwa wakati gani. Kuona hata maendeleo na mabadiliko ya safari kwa njia ya picha na video. MAISHA YA SASA YANAZIDI KUTUTENGA KWA KUTUWEKA KARIBU, na ni wakati ambao pengine ukaribu tunaopewa ama kujengewa na ndio unaosababisha umbali wa hisia na uhalisia wa maisha.
Tumeweka imani katika VIFAA na kusababisha kuamini matumizi yake kuliko nia na dhamira zetu
NIREJEE KATIKA MUZIKI...
Leo tunao wana Tancut Almasi Orchestra na kibao hiki cha MASAFA MAREFU ambacho kinazungumzia hali halisi ya zama hizo.

Nilipomaliza kutayarisha post hii nimekutana na video hii ya THE KILIMANJARO BAND almaaruf kama WANA NJENJE walipoimba wimbo huu jukwaani. ITAZAME

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

5 comments:

Simon Kitururu said...

Mkuu umenigusa sana na kauli yako hii:``MAISHA YA SASA YANAZIDI KUTUTENGA KWA KUTUWEKA KARIBU´´.

John Mwaipopo said...

Kitururu unajua mubelwa ana utundu fulani wa kiswahili haujatafutiwa istilahi yake.

nimeamshwa kuchangia baada ya kumuona mshabiki katika video ya wana njeje akimtunza John Kitime shilingi 10000. inaonyesha jinsi gani mshabiki huyo asivyojua sauti za gitaa zinatengenezwaje. 'amesokomeza' hiyo noti katika vidole vinavyotafuta utamu pengine akidhani gitaa linashikwa kama jembe. yote ni katika kukunwa pengine

emu-three said...

Maisha ni safari ndefu, na kila hatua kuna mabadiliko, sihdani hatua ile uliyoipita inaweza ikawa sawa na hatua unayoinua sasa. Kwa kiwiliwili kinaweza kikawa kimechoka, au kikawa kimeingiwa na mori zaidi.
Mabadiliko ni muhimu na tunayaona hasa ya teke-linalotujia, wengine wanasafairi kwa treni za umeme, anaishi mwanza anafanyia kazi mtwara, sisi naona hiyo bado ni ndoto!
Vyovyote iwavyo binadamu kichwa chake kimeaa hazina, na asilimia ndogo sana inayotumika ...huenda itafika wakati mtu anawaza tu, na kinatokea alichokiwaza...!
Waliolala waacha waendelee kulala , kwa akina Dowansi wapo wengi, ukiamuka kila kitu hakuna, sijui tutawaambia nini vizazi vyetu vinavyokuja!
Ni wazo tu mkuu!

Goodman Manyanya Phiri said...

Mtu kwa kweli unahitaji angalau wiki moja kwa mwaka unakwenda kijijini bila CELLPHONE, kampyuta au kifaa chochote kile ila upate nafasi ya kuongea na yule jamaa anayeishi ndani yako tena umwulize kabisa: KWELI VIFAA NINAVYO AU MIMI NIMEGEUKA KIFAA CHA VIFAA VYANGU?

Rachel Siwa said...

Kweli iliuwa msafiri ni jasiri!

@kaka Mubelwa hicho kitu cha Tancut!!maana [baba S] anazitafuta sana,je unazo za kutosha?tafadhari [baba P]Tuwasiliane mbona kwa mtandao sizipati? au wewe ni ile ya Akiba haiozi!!!

Asante ndugu yangu mswahili!!!!!!

msalimie wifi [mamap]