Tuesday, April 12, 2011

AKUMBUKWE KWA LIPI?

Unakumbuka KUMBUKUMBU HII YA KIFO CHAKE?.
Sasa kwa mtazamo wako, miaka 27 baada ya kifo chake.....
NINI LA KUKUMBUKWA KUHUSU EDWARD MORINGE SOKOINE?
UNADHANI ANAENZIWA KAMA INAVYOSTAHILI?

7 comments:

emu-three said...

Huyu angelikuwepo, nafikiri neno mafisadi lingekuwa msamiati mgumu!

Yasinta Ngonyani said...

Ni swali nzuri kwani nakumbuka alipokufa nilikuwa kachiki bado na sikumbuki nini njema alilofanya ila nasikia alikuwa waziri mwenye busara na hekima na naamini kweli sasa hakungekuwepo kama kulivyo...hapa najaribu kufikiri kwa sauti kwa yale niliyoyasikia na kuyasoma...

Goodman Manyanya Phiri said...

Barabara ya kutoka Dakawa kwenda Morogoro pamejengwa MONUMENT kumkumbuka Sokoine. Sijasoma ya kutosha kuhusu maisha au kifo chake bali nasikia tu kwamba hakuwa ndumakuwili na alichukia hayo mambo kama ufisadi.

Swali langu (tena la uchokozi na kuchemsha bongo) ni hili:

Je, tunajuaje alikuwa mkweli na yeye hapo baadaye, kama mnafiki, angebadilika tu kuwa naye mfisadi?

Kwa hiyo, tuseme ni wazo tu kuwa alikuwa mtu mzuri. Anaejua uzuri na upungufu wake ni roho yake na Mungu wake. Labda kidogo pia waandishi waliobobea kwa kufanya utafiti na maandishi juu ya maisha ya huyo shujaa.

Mimi binafsi kwake nimejifunza haya mawili:

1. HE WAS BORN BEFORE HIS TIME, ALSO REMARKABLE THAT HE DIED 12 APR 1984 ON THE EVE OF NYERERE'S 62ND BIRTHDAY!

2. Ukiwa mwanamapinduzi, usijionyeshe haraka-haraka wewe ni rangi gani (TRUE COLOURS) la sivyo unaweza kupata ajali ya gari kuwawacha waliohai sisi tukijiuliza "ajali kweli au majaliwa kwa mafisadi?"

nyahbingi worrior. said...

Kaka Bandio mzima?Habari za siku nyingi kaka.

Kweli Sokoine ni kiongozi wa kuigwa na wengi,watoto wetu waambiwe ukweli kuhusu ukweli,ukweli hukusu maisha na kifo cha kiongozi sokoine.

Unknown said...

Mi ninachokumbuka kwake nisimulizi ya kifo chake jinsi kilivyoumiza na kushangaza wengi japo inasemwa alikuwa kiongozi wa kweli aliyekuwa anajali maslahi ya Taifa.

Hii ni kwa mujibu wa simulizi za waliokuwa wanasimuliana.

malkiory said...

Kama siyo kifo chake basi leo ufisadi ungekuwa ni msamiati Tanzania.

Rachel Siwa said...

Kwangu mimi nitamkumbuka kama aliyekuwa kiongozi wa WaTanzania,Mengi nayasikia lakini siyajui!
Niliona Wazazi wangu wakifadhaika na kuhudhunika kwa sababu ya kifo chake.