Friday, April 15, 2011

Them, I & Them....SHE IS STILL LOVING ME

"Oh she's truly mine, and most of what she does makes me feel so good inside. Shes the right one for me,..." Morgan Heritage Utamu wa maisha unatokana na namna unavyoweza "kutamusha" uchungu wake. Ni pia katika UVUMILIVU ambao unasifika kuwa mvumilivu pale unapoweza kuvumilia yale ambayo wengi wanaamini HAYAVUMILIKI. Yaani pale unapoenda zaidi ya mategemeo yao katika kutenda ambalo wengi hawaamini kama utaweza kulitenda. Na katika kutenda huku, wengi huvumilia na kuacha njia waitakayo katika kutimiza nyingine ambayo ina faida zaidi ya yao binafsi. Mara nyingi nimekuwa nikiandika kuhusu SIASA na MAISHA na (kuonekana) kuweka kando wale wanaonifanya niwe na muda, akili na utulivu wa kuandika hayo. Sipo peke yangu, mtu yeyote anayefanya kazi, anakuwa na msaada (chanya ama hasi) unaomuwezesha kufanikiwa kwa kiwango alichofanikiwa. Ni hapa ninapokumbuka uleee msemo kuwa "katika mafanikio ya kila mwanaume, kuna uwezeshaji wa mwanamke". Kwangu mimi hili liko sahihi. Kwa wengi wetu, ili tuweze kufanikiwa katika harakati, kuna sehemu ya muda ambao tunauweka kando. Muda wa kuwa na wapendwa wetu, wa kuwa na wasaidizi na / ama familia zetu. Mwaka 2001..
Ni kile ambacho kwa kiingereza wanaita SACRIFICE. Na hili si jambo jepesi kukubalika na wengi katika familia, lakini inapotokea mwenza wako katika familia akalikubali, na kuvumilia makwazo, kero, hamu ya kuwa nawe kwa zaidi ya unavyopatikana, uchovu unaokuja nao, msongo wa mawazo (stress) unaoweza kutokana na harakati zinazozidiwa na muda wa kupumzika, kwa hakika yapaswa kujivunia hili. Binafsi naendelea kujivunia "milima na mabonde" ya maisha ninayopanda na kushuka pamoja na mke wangu mpenzi. Si wakati wote (kama ilivyo kwa mwanadamu yeyote) ninaweza kuwa sahihi katika yote, lakini hata pale ninapokwenda halijojo huwa "tunapata pa kutokea" na kwa hilo ndio maana nimependa Morgan Heritage waliposema "She's my one and only, I ain't going no where, I aint gonna leave my lady for no one" Miaka 10 baadae....
Wasikilize The Morgan Heritage katika wimbo huu SHE'S STILL LOVING ME kutoka katika albamu ya Three In One

She's still lovin' me though I caused her so much pain
I've done my share of wrong (my share of wrong) Time and time again
She's still lovin' me and I can't deny, oh no no no no
since she been in my life (in my life) everything's been going fine
And I proudly say to world yea

Bridge:
She's my one and only and I aint going no where, I aint gonna leave my lady for no one
She's my one and only And I aint going no where, I aint gonna leave my lady

Oh she's truly mine, and what of what she does Makes me feel so good inside.
Shes the right one for me, ya make no mistake
And I say theres no apology
(Gramps what do you say bout ya lady)

She's still loving me yeah through the trials and pain
Oh i played around still she held it down (yes she did)
She's still loving me, even thought I made her cry
Caused her many sleepless nights and I had to make it right

Bridge:
She's my one and only and I aint going no where, I aint gonna leave my lady no no no
She's my one and only I aint going no where, I aint gonna leave my lady

Cause she's truly mine, and most of what of what she does Makes me feel so good inside
Shes the right one for me, ya make no mistake And I tell the world theres no apology

Repeat Bridge till fade...

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

5 comments:

Albert Kissima said...

Kaka, nimelipenda bandiko hili. Lina mhamasisho chanya wa maisha.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mahyoge waitu, omukama ababele mugendelele kandi mushokangane akatooke kanule.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mahyoge waitu, omukama ababele mugendelele kandi mushokangane akatooke kanule.

Yasinta Ngonyani said...

Nanukuu "Binafsi naendelea kujivunia "milima na mabonde" ya maisha ninayopanda na kushuka pamoja na mke wangu mpenzi." MWISHO WA KUNUKUU:- Unayo kila haki ya kujivunia mpenzie kwani kama watu wanapendana kwa dhati huo ndio upendo..na upendo pia pia ni pale mtu mmoja anapojitolea kufanya kila kitu hata kama ni kufa na kupona kwa ampendae. Muwe na amani katika familia yenu na Mwenyezi Mungu atawala nyumbani mwenu wakati wote.

Goodman Manyanya Phiri said...

Made in heaven!