Friday, April 29, 2011

Hivi ni KWANINI.....??

Haya sasa. Siku ya siku ilifika. Hatimaye "wapendanao" wakafunga ndoa. Lakini wakati bado watu wanawaza kuhusu HARUSI na mapokopoko mengi sana. Lakini kwangu haikuwa kuhusu HARUSI, bali kuhusu NIA YA KUITAZAMA HARUSI HII. Nakumbusha kuwa NIMESEMA HARUSI NA SIO NDOA.
Sasa ninalowaza ni kuwa KWANINI WATU WENGI WALIFUATILIA HARUSI HII?
Kwa mujibu wa tovuti ya OneIndia.com, mamilioni ya watu walifuatilia harusi hii. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, "many television networks are offering commentary and video from London. It is estimated that about 2 billion people will watch the Royal Wedding live on TV and another 400 million people on the internet." Hii idadi si ya masihara. Ni watu wengi sana. Hata tovuti ya Hollywood Reporter imesema hapa, kwamba harusi ya wapendanao hawa IMEVUNJA REKODI ya wafuatiliaji wa mtandaoni.
SASA.........kama
-Ilishajulikana kuwa wataonana.
-Walishajulikana Bwana na Bibi Harusi.
-Hakukuwa na tetesi kuwa kuna uwezekano wa jambo la ajabu kutokea.
-Gharama za harusi hii haziwezi kufikiwa na wengi (kwamba waliangalia kuiga).
-NI KWANINI MAMILIONI YA WATU WALIFUATILIA HARUSI HII?
Ni kufuata MKONDO wa vyombo vya habari vinavyojali idadi ya watazamaji / wasikilizaji / wafuatiliaji?
Kuna ambalo walitaka kujifunza katika ndoa hii?
Kwa kutazama harusi hii (ambayo kuna baadhi ya wafanyakazi waliochukua mapumziko kuifuatilia), kuna ambalo wanandoa ama maharusi watarajiwa wanalotegemea kujifunza?
AMA??
Nawaza kwa Sauti tu!!!

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

2 comments:

Mija Shija Sayi said...

Nina hakika kabisa hakuna aliyeifuatilia harusi hii kwa nia ya kujifunza jambo bali kufurahisha macho tu. Angalia mambo yaliyokuwa yakiongelewa sana na vyombo vya habari, unakuta ni gauni la bi harusi litakuwaje, busu la kwanza la harusi litakuwaje na mengine meeengi yasiyohusiana na mafunzo yoyote katika jamii.

Naomba nami niungane nawe katika swali lako.."HIVI NI KWA NINI.....??"

Yasinta Ngonyani said...

Sipo kabisa nyuma nanyi kaka Mubelwa na Dada Mija "HIVI KWA NINI? SI HARUSI TU HATA VIFO VYA WAFALME NA MARAISI NA WASANII HUWA VINAVUMA SANA KWANINI?