Tuesday, April 26, 2011

Una uhakika ni ndoto si ufunuo?

Photo Credits: The Esoteric Blog
Naanza kwa kujiuliza tofauti ya ndoto na ufunuo. Maana najua wapo wafunuliwao wakiwa usingizini. Lakini ina maana kama yale waliyoofunuliwa hayatatokea machoni ama kusikika masikioni mwao wataendelea kuona huo kama ufunuo ama ndoto? Hapa ntahitaji msaada kidogo maana twatofautiana uelewa juu ya hili ama haya. Ninalomaanisha ni kuwa kama halijatokea kwako ama hujalisikia laweza kuendelea kuwa ndoto kwako, lakini kama ulishalisema kwa mtu na akaliona likitendeka huko aliko anaweza kuona ni ufunuo.
Sasa tukirejea kwenye CHANGAMOTO ZETU zitukabilizo kila siku, unadhani ni mangapi unayaota usiku ama ulalapo na unashindwa kuyatendea kazi? Sisemi kuwa uendeshwe na ndoto na majinamizi yakutumbayo usiku maana najua si yote ama zi ndoto zote senye nia ama mtazamo mzuri, lakini ni kweli kuwa hakuna haja ya kutilia maanani yale mema tuotayo? Je kuyasimulia?
Lucky Dube alisema "Have you ever see the dream walking? Have you ever hear the dream talking? ....You are THE MASTER of your dream, if you pull the right string it will be talking to you, if you pull the right string it will be walking to you. You're the ONLY OE who knows what it is...YOU'RE HOLDING THE KEYS TO YOUR DREAMS. Don't hesitate, grab the chance before it's too late .... reach out and touch your dream" Akimaanisha (kwa tafsiri yangu) kuwa si vibaya kuangalia njia sahihi na muafaka ya kutimiza zile uonazo kama ndoto zako na kuna ukweli kuwa upo uwezekano ukafanikiwa. Lakini ni kama utachukua hatua hiyo ya kutekeleza hayo kwa wakati muafaka. Namkumbuka mmoja wa wahubiri niliowahi kuhudhuria ibada zake aliyesema "your mental picture will determine your actual future". Sasa hapa naunganisha na ile tafsiri kuwa tunaota yale tuwazayo. Ina maana tunawaza kwanza kisha tunaota. Kwa hiyo ina maana kuwa kwa namna moja ama nyingine hayo tuotayo (narudia tena si yote) yapo ndani mwetu. Au nimekosea? (Una haki ya kukosoa pia)
Ni wimbo huo huo ninapousikiliza nikakumbuka yale niliyowahi kuota nikiwa bwana mdogo na ambayo yamekuja kutimia baada ya juhudi na misaada ya wengi na kujiuliza kama nisingeweza kusaidiwa na kujishughulisha ningeweza kutimiza? Ina maana zilikuwa ndoto ama nilifunuliwa maisha yangu yajayo?
Tunapoanza mwaka ujao na tuwe makini katika kuupanga. Kumbuka yale upendayo ambayo umekuwa ukitamani, kuota na kujaribu kuyatekeleza lakini hukupata nafasi ya kujaribu. Yape muda na mipango sahihi ya kuyatenda na yawezekana yakabadili maisha yako.
Msikilize hapa chini akizungumzia namna ya kugusa ndoto zako.

KILA LA KHERI

2 comments:

emuthree said...

Ndoto au ufunuo, mfano umeota kuwa unachinja watu...au umeota kuwa wewe ni umeiba, au umeota kuwa unakufa...whatever...unaota vitu vibaya, utasemaje...? hakika utadharau na kusema kuwa hiyo ni ndoto tu. ila ota unapata vitu vizuri...utaipamba hiyo ndoto na kuiita ufunuo...kama sikosei
Ni hayo tu mkuu. Nashukuru kwa darasa lako, TUPO PAMOJA!

Goodman Manyanya Phiri said...

Hoja yako nzuri sana.

Imani na EXPERIENCE yangu ni kwamba ukiwa mkweli, mwenye upendo hata katika hasira zako; ukiwa Mchamungu na mwenye dhamira safi, BASI NDOTO ZAKO MBAYA NA NZURI NI UFUNUO MTUPU.

Ndio maana unatakiwa kulinda dhamira yako daima na usifanye hata kimoja gizani usingependa watu wakuone unakifanya ingekuwa mchana.