Thursday, April 21, 2011

What if we "what if(s) positively? (II)

Pengine swali la kwanza ni "What if Mubelwa angeandika heading hii kwa kiswahili?" Na ningejibu kuwa yawezekana usingevutiwa nayo, AMA isingeweza kuleta maana nitakayo, LABDA usingethubutu hata kusoma maana yawezekana umeshtushwa na kichwa hiki cha habari au YAWEZEKANA unasoma kwa kuwa unataka kuelewa yamaanisha nini kwani ni kama haieleweki.
SAAAFIII.
Ndilo lengo kukufanya usome maana ukiangalia uwezekano wa maswali mengi, utagundua kuwa yatakuwa ni "negatives" zaidi.
Lakini hapa lengo si kueleza sababu ya kichwa cha habari. Hapa nataka kuuliza mawili matatu juu ya hali halisi ya utata ambayo imekuwa ikituyumbisha katika maisha yetu. Ni ile hali ya kuogopa na kuhisi kitu kisicho cha mafanikio kitatokea katika kile ambacho mtu anataka kufanya. Kuwa na ile hali ya kutanguliza kushindwa katika mipango mipya na ni hali hiyo ambayo inatukatisha tamaa na kutukwamisha wengi. Kuna mtu aliniambia "your mental picture will determine your actual future" na ni katika hili tunapojijengea maanguko kwenye mipango yetu mipya kwa kuuliza "what if" isipofanikiwa? Labda tujiulize ni mara ngapi tumetaka kufanya kitu kisha tukaamua kuacha kwa kuambiwa hatutafanikisha ama kujiambia wenyewe "itakuwaje nisipofanikisha?" Tusilojua ni kuwa kwa kutofanya ama kuanza kufanya vitu hatutakutana na CHANGAMOTO zilizo muhimu katika kukua, kukomaa, kupevuka na kuendelea kwetu. Ina maana kwa kutofanya yale tupendayo tukihofia kutofanikiwa tunajifungia milango ya kuendelea kwenye maisha yetu na hilo linafanya wengi wasiopenda kujaribu ama wanaoshindwa kujaribu kwa kuhofia majibu mabaya ya "what if?' kushindwa kutimiza ndoto zao kwa kufanya kazi wasizo na mwito nazo, jambo linalowafanya wakose ubunifu unaostahili na kisha kuifanya kazi kutokuwa ya furaha kama ambavyo ingestahili. Hili linayafanya matokeo ya kazi kutokuwa katika kiwango kinachotakiwa na kusababisha jamii kutopata "matunda" halisi ya kazi hizo. Kakangu ALBERT KISSIMA aliwahi kuuliza SWALI HILI na sina uhakika ni wangapi waliweza ama wangeweza KULIWAZA KWA U-CHANYA wake? Aliweka Chemsha Bongo HAPA akiuliza "Utachukua uamuzi gani pale mlinzi wako wa usiku anapokusimulia ndoto aliyoota usiku wa leo na anakutaka uahirishe safari yako kwani safari yako kulingana na ndoto yake inaonyesha basi utakalosafiria litapata ajali na watu wote watapoteza maisha? Fikiria kuwa umeahirisha safari na kweli ajali ikatokea,kwa maana kuwa ameokoa maisha yako. Utamfukuza kazi au utaendelea kuwa naye?"
Natambua kuwa jamii ingenufaika kama kila mtu angeweza kufanya kile apendacho na ni rahisi kufanya hivyo tukiacha kukatishana tamaa kwa kutilia mkazo na kuulizana "matokeo hasi" (negative results) za kile tutakacho kufanya. Mtambuzi Shabani Kaluse aliwahi kuzungumzia juu ya hofu ya kesho kuwa kama dubwana la kutisha (irejee hapa)
Sasa naamini twatambua kuwa kuna maswali ya kujiuliza katika harakati zetu za kuikwamua jamii, na swali langu ni "what if we 'what ifs' positively"? Nadhani itasaidia kuwafanya watu waamini katika ndoto zao na kufanikisha mengi kwenye jamii.
Ni mtazamo tu BINAFSI kwani kwa niaminivyo mimi, BINADAMU WOTE NI WABINAFSI. Ndivyo ninavyoamini mimi na ninaweza kukudhihirishia hili. Mbinafsi wa kwanza ni mimi ambaye kwa u-binafsi wangu naamini sote tutakuwa sawa iwapo tutahesabika kuwa sote tu wabinafsi (faida kwangu), na m-binafsi wa pili ni yule ambaye kutokana na kutaka kuwa bora kuliko baadhi yetu, atakuwa m-binafsi kupinga kuwa si sote tulio wabinafsi kwa kuwa haamini kuwa yeye ni kama sisi. Yaani yeye ni tofauti. (faida kwake). Hivi what if we what ifs positively kuhusu ubinafsi wangu na wako?
Tuonane "Next Ijayo"

3 comments:

Simon Kitururu said...

NImependa kweli mahubiri ya leo Mkuu!

Na asante kwa kunifikirisha!

emu-three said...

Mkuu unanipa shule ambayo inanipa mwanga fulani kwa kisa fulani...mmh, ngoja, lakini sijakimaliza hiki nataka kile...USIJALI MKUU, NASHUKURU KWA SHULE HII , ...HAPA KWAKO NAPAITA SHULE YA CHANGAMOTO!

naomimwakanyamale said...

Waw....THAT was meant for me!